Riwa
Platinum Member
- Oct 11, 2007
- 2,607
- 3,079
Wana jf wenzangu naomba mnifahamishe ni siku gani mwanamke anaweza kupata mimba,siku ya ngapi baada ya kutoka kwenye period?
Wanawake wengi wana mzunguko wa mwezi wa siku 28, japo kuna wengine wachache wana mzunguko mrefu wa siku 30 na wengine mzunguko mfupi wa siku 25 au 26. Katika mizunguko yote hiyo, yai huolewa (ovulation) siku ya kati ya mzunguko ina maana siku ya 14 kwa mzunguko wa siku 28, siku ya 15 kwa mzunguko mrefu na siku ya 13 kwa mzunguko mfupi. Manii za mwanaume zinaweza kuishi mpaka siku tatu, kwa hiyo iku za hatari kwa mwanamke kupata mimba kwa mizunguko yote mitatu ni kuanzia siku ya 11 tangu AANZE kupata hedhi, mpaka siku ya 18.