Dada haya hapa ni maelezo ya sindano uliyotumia kwa kifupi
Depo-Provera
Depo-Provera ni dawa ya uzazi wa mpango kwa njia ya sindano, (kuzuia mimba). Depo-Provera, wakati mwingine pia hutumika kwa ajili ya matibabu ya matatizo mbalimbali ya masuala ya uzazi.
Ina homoni iitwayo medroxyprogesterone ambayo inajulikana kama progestagen,
sindano hii ni kinga dhidi ya mimba kwa kuzuia ovulation (Kutotoka kwa yai katika ovary) . Sindano hii pia hukinga dhidi ya mimba kwa muda wa miezi mitatu kuanzia siku ile ulipochomwa.
Wakati wa kumaliza kwa dozi ya sindano hii ya kuzuia mimba, itachukua muda kabla ovulation na hedhi kuanza tena. Hii ina maana kwamba pia inachukua muda pia kupata mimba. Ni kati ya mwanamke na mwanamke, lakini mara nyingi itakuwa ovulation ianze miezi sita hadi nane baada ya chanjo ya mwisho. kwa hiyo inakubidi uwe na subira. ila ni vizuri kufanya mapenzi na mumeo siku ya 12-17 toka siku unapata hedhi, hii itakuwa rahisi kushika mimba, kwa ni wakati yai linatoka kwenye ovary )ovulation period), na kama mlipumzika kwa mda huo bila mapenzi basi hata mumeo takuwa ametengeneza mbegu za kutosha kukupa mimba. ukiona bado hushiki mimba nenda wewe na mumeo wote mkapime, tatizo la weza pia kuwa kwa mumeo. siku njema na kila la kheri!!!