The secretary
JF-Expert Member
- Jan 14, 2012
- 4,148
- 2,537
kama huwezi kujali, hebu weka kalenda yako hapa ya kuanzia January mpaka March,
yaani January ulianza Period lini na kumaliza lini, kwa kwa Feb na March hivyo hivyo, tukusaidie kupata Mimba,
lakini angalizo lazima lizingatiwe kuwa Mwenzio naye yupo sawasawa kwa maana ya mbegu zake zina uwezo wa kutungisha mimba (Japo ni uwanja mpana)
Kama umeolewa ningekushauri mshirikiane kwa karibu sana na mume wako. Sio lazima mara zote tatizo liwe kwa mwanamke, kuna nyakati wanaume pia wanaweza kuwa ni/na tatizo katika mchakato mzima wa kurutubisha (fertilize) yai.
Madokta wameshaacha mgomo, nenda tu ukawaone moja kwa moja na mume wako mwende nae!, usitanie tatizo kwa kutaka matibabu ya bure hapa!
Jan 14.feb 15,march 14
Tayari tuna mtoto
indano ya aina gani umechoma! zipo za aina nyingi, kama unakumbua weka hapa jibu utapata! pia si kila ufanyapo mapenzi unapata mimba. jaribu kutegeshea mumeo siku ya 12 mapka 16 tangu upate siku zako, utaona majibu haraka. msifanye kila siku kwani mbegu zitakuwa chache na hafifu!
Mpenzi wako atakuwa mgumba jaribu kubadili mme uone kama haujadaka.
hiyo sindano uliyochoma,sometimes inachelewesha kupata mimba.kuna dada namfahamu alichoma hiyo sindano,alikuja kupata uja uzito kwa mara ya 2 baada ya miaka 12
we nadhani hazimo kichwaniMpenzi wako atakuwa mgumba jaribu kubadili mme uone kama haujadaka.
usishtuke,sindano 2 ulizotumia nadhani sio nyingi.ipo siku utapata tuMbona mnanitisha
Dipopuvera
Dada haya hapa ni maelezo ya sindano uliyotumia kwa kifupi
Depo-Provera
Depo-Provera ni dawa ya uzazi wa mpango kwa njia ya sindano, (kuzuia mimba). Depo-Provera, wakati mwingine pia hutumika kwa ajili ya matibabu ya matatizo mbalimbali ya masuala ya uzazi.
Ina homoni iitwayo medroxyprogesterone ambayo inajulikana kama progestagen,
sindano hii ni kinga dhidi ya mimba kwa kuzuia ovulation (Kutotoka kwa yai katika ovary) . Sindano hii pia hukinga dhidi ya mimba kwa muda wa miezi mitatu kuanzia siku ile ulipochomwa.
Wakati wa kumaliza kwa dozi ya sindano hii ya kuzuia mimba, itachukua muda kabla ovulation na hedhi kuanza tena. Hii ina maana kwamba pia inachukua muda pia kupata mimba. Ni kati ya mwanamke na mwanamke, lakini mara nyingi itakuwa ovulation ianze miezi sita hadi nane baada ya chanjo ya mwisho. kwa hiyo inakubidi uwe na subira. ila ni vizuri kufanya mapenzi na mumeo siku ya 12-17 toka siku unapata hedhi, hii itakuwa rahisi kushika mimba, kwa ni wakati yai linatoka kwenye ovary )ovulation period), na kama mlipumzika kwa mda huo bila mapenzi basi hata mumeo takuwa ametengeneza mbegu za kutosha kukupa mimba. ukiona bado hushiki mimba nenda wewe na mumeo wote mkapime, tatizo la weza pia kuwa kwa mumeo. siku njema na kila la kheri!!!