Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

mbarikiwe sana jmn kuweka hii topic stick.... Mhariri ni topic ipi iyo ulompatia TOTS SHALO?? ni hii ya kungurumweupe au ingine niwekee
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ngonalugali, sikubaliani na maelezo yako!

Ukweli ni kwamba, mbegu za kiume (yaani Y) ni nyembamba kwa umbile na ni faster ukilinganisha na zile za kike (yaani X).

Hii ni kwa sababu ya ukweli kwamba, 'wembamba' wa umbo la mbegu za kiume huziwezesha kuogelea kwa urahisi kuliko zile za kike katika yale majimaji ya uke wa mwanamke. Hii inamaana kwamba, kama yai la mwanamke litakuwa tayari kwenye sehemu ya kurutubishia (yaani kama mwanamke atakutana kimwili na mwanaume siku ile ya mimba) basi mbegu moja tu ya kiume itakayotangulia kulifikia yai itaweza kurutubisha na kisha yai huvaa koti gumu ambalo huyazuia mamillioni ya mbegu zingine za kiume zilizochelewa pamoja na zile za kike zisiingie ndani ya hilo yai badala yake hubaki nje ya yai zikisubili kufa. Mtoto wa hii mimba ni wa kiume, yaani YX.

Kama mwanamke atakutana na mwanaume siku 3 kabla ya siku ya mimba (fertile day) basi kuna uwezekano mkubwa wa kuzaliwa mtoto wa kike, yaani XX. Hii ni kwa sababu zile mbegu za kiume zitaogelea kwa kasi kubwa lakini zikifika kwenye sehemu ya kurutubishia hazitalikuta lile yai kwa sababu litakuwa halijafika sehemu yake. Zitasubili kwa siku mbili kisha zinakufa! Mbegu za kike zitaogelea polepole mpaka ile sehemu ya kurutubishia kisha zitakaa hapo kwa siku 3 zikilisubili lile yai lifike. Likifika tu ndani ya hizo siku 3 basi mbegu moja tu ya kike itakayochangamkia tenda italirutubisha yai hilo na kutengeneza mtoto wa kike, yaani XX.

Kama itatokea kwamba mbegu zaidi ya moja zitafanikiwa kulirutubisha yai, basi yai hilo litagawika katika vipande vyenye idadi sawa na mbegu zilizorutubisha na kupata watoto mapacha wasiofanana! Kwa mfano, kama mbegu 2 zitarutubisha yai basi watazaliwa mapacha wawili wasiofanana. Na kama mbegu 6 zitarutubisha yai, basi watazaliwa mapacha 6 wasiofanana; kitu ambacho hata hivo ni nadra sana kutokea, yaani mapacha 6.

Kama mbegu moja itarutubisha yai halafu muungano huo ukawa na idadi ya chromosomes zinazozidi kiwango kinachotakiwa, basi yai hilo litagawika sehemu mbili zilizo sawa na kupata mapacha wawili wanaofanana na ambao ni wa jinsia moja kufuatana na mbegu ipi kutoka kwa mwanaume ilirutubisha yai, ya kiume au ya kike.

ahsante ndugu Kungurumweupe me ndo nimejifuza leo...tena umetoa maelezo mazuriiiii...big up
 
nimeelewa sana hili somo aisee...Ila sasa mwenzi wangu alikuwa na cycle ya kawaida ya siku 28 Ila ghafla mwezi huu kableed baada ya siku 15,ina maana gani hii wadau?
 
Hello, mimi huwa nakaa sana vijiweni saa zangu za mapumziko baada ya kazi, na mara nyingi huwa naongea issues nyingi sana na washikaji. Na kama kuna issue ambayo nimeona imeleta ubishani sana, huwa nakuja kuileta huku.

Tulikuwa tukijadili jambo moja hivi, kwaba, ni lini mwamke anaweza akapata mimba? Mimi kwa uelewa wangu niliwaambia ni siku ya kumi na tatu au kumi na nne after menstrocycle. Wengi walibisha, pamoja na kwamba hizo ndo prabable days za ku conceive. Wengi wanasema hata siku nyingine zinaweza, ila mimi kulingana na uelewa wangu, nilikuwa naelewa hivyo kwasababu watoto niliopata sijui kama nilifanya hizo siku au la, nilikuwa nadukua tu mara kwa mara mwezi mzima.

Walinibana swali moja kwamba, unaanza kuhesabu lini, yaani utaanzia siku gani kuhesabu hadi zifikie siku hizo hapo juu, unaanza kuhesabu siku ya kwanza ya bleed ndo siku ya kwanza au siku ya mwisho wa bleed ndo siku unayoanza kuhesabu? Mimi niliwaambia ni siku ya kwanza unapoanza kubleed.

Naomba kama kuna madaktari humu watoe elimu hapa kwasababu najua watu wengi wataelimika hapa, na wengi wanaweza kuepuka hata mimba zisizo na malengo.

jamani mi mpenz wangu mbna hayupo ktk kundi lolote hapo kwan ye huona period after 30 dayz kuanzia 13/14 na kuziona tena mwezi ujao tarehe sawa na hzi.......msaada tafadhari
 
Wakuu,

Naomba nijibu maswali ya Yassin kama ifuatavyo:


Swali
la kwanza la Yassin: Kama inabidi iwe siku ya 14 or 15 sasa si kila mtu angekuwa na birthday hizo siku 2???


Jibu:
Watu wote hawawezi kuwa na birth day siku ulizozitaja pekee kwa sababu kila mwanamke ana kalenda yake inayoanza tofauti na ya mwingine hata kama wote wakiwa na menstration cycles zenye urefu unaofanana e.g 22 days. Hata kama itatokea kwamba wanawake wawili wakawa na menstration cycles zenye urefu unaolingana, e.g 22 days, halafu hawa watu wakaanza ku-bleed siku moja e.g 01/sept/08 halafu wakapata mimba siku moja e.g 08/sept/08 (yaani siku ya mimba for this case), kamwe haitatokea wakajifungua siku moja kwa sababu, pamoja na kwamba tunafahamu mtoto huwa anakaa miezi 9 tumboni, lakini wajawazito wengi huwa wanatofautiana idadi ya siku za kubeba mtoto tumboni! Wengine huwa wanatimiza exact 9 months, wengine hujifungua chini ya miezi 9, na wengine hujifungua zaidi ya miezi 9 (yaani miezi 9 na week 1 au 2)


Mfano hai: Kama Lorain na Asha wote wawili wana cycles za urefu wa siku 22 kila mmoja, basi Lorain anaweza kuianza cycle yake tarehe 1/sept/08 na akapata mimba 8/sept/08, wakati Asha akawa pengine anaianza cycle yake tarehe 9/set/08 na akapata mimba tarehe 16/sept/08. Pamoja na kwamba wote wana cycles zenye urefu unaolingana(yaani siku 22) lakini safari ya cycle ya kila mmoja wao inaanza siku tofauti na ya mwenzake! Hii ndiyo sababu tosha ya wao wawili kukosa uwezekano wa kujifungua siku moja (same birth day)!


Swali
la pili la Yassin: Kwa nini sasa unahesabu kuanzia mbele kurudi nyumba?

Jibu: Kwanza hapa tunataka tuwe na a single/systematic/uniform counting, ili tulahisishe maisha kama kawaida yetu wanadamu! Ndo maana wanasayansi wa zamani walipendekeza tuhesabu siku 14 kuanzia ile siku bleed inapoanza! Kweli hili walifanikiwa lakini ni kwa wanawake wale tu wenye cycle ya siku 28. Walisahau kwamba hii siku ya mimba huwa inasogea mbele kama cycle itarefuka zaidi ya siku 28, na husogea nyuma kama cycle itakuwa fupi chini ya siku 28. Hapa ndipo wengine ikatubidi tufikilie upya jinsi ya kupata that single/systematic/uniform counting! Na hapa ndipo counting back 15 days inapopata umuhimu wake! That's all!

To conclude therefore, Counting back 15 days from the end becomes the only reliable solution for all women, and it replaces the traditional one of counting forward 14 days from the first day of bleed!



Hebu tujikumbushe tena maswali yetu:



Swali: Je, nifanye nini ili nizae mtoto wa KIUME:

Jibu: Ili mwanamke aweze kuzaa mtoto wa KIUME, inabidi alale na mwanaume siku ile ya mimba (fertile day), ambayo ni siku ya 15 unayoi-pin point when counting backward from the last day!


Swali: Je, nifanye nini ili nizae mtoto wa KIKE:

Jibu: Ili mwanamke aweze kuzaa mtoto wa KIKE, inabidi alale na mwanaume siku 3 kabla ya ile siku ya mimba (yaani siku 3 kabla ya ile fertile day)! Hii inaondoa uwezekano wa mbegu za kiume kulirutubisha yai, kwani mbegu zote za kiume zitakuwa zimeshakufa ndani ya siku mbili za mwanzo na kuziacha zile za kike zikidunda kwa siku moja zaidi zikilisubili yai lifike ili zigombanie kulirutubisha! Kumbuka kwamba, ni mbegu moja tu inahitajika kurutubisha yai. Endapo itatokea mbegu zaidi ya moja zikalirutubisha, basi yai hilo litagawika sehemu zenye idadi sawa na mbegu zilizorutubisha ili kutengeneza mapacha wasiofanana kwa sura, na pengine jinsia pale inapotokea mbegu za kike na za kiume zimechangia kulirutubisha yai!

Swali:
Je, kama menstration cycle yangu ni siku 15, nifanye nini ili nipate mtoto wa kike?


Jibu:
Ili mwanamke mwenye menstration cycle ya siku 15 aweze kuzaa mtoto wa KIKE, inabidi alale na mwanaume siku 3 kabla ya siku ile ya bleed (yaani siku 3 kabla ya ile siku anayoanza kutokwa damu ya hedhi)! Kwa mwanamke wa kundi hili inabidi tukumbuke kwamba, siku yake ya mimba ndiyo siku hiyo hiyo anayoanza ku-bleed!


NOTE:
Majibu yote matatu tuliyoyaona hapo juu na katika posts zilizotangulia yana-aply kwa wanawake wote wenye uwezo wa kuzaa, yaani wasiokuwa na utasa [/B]!
hujani convice kuhusu cunting kuanzia mbele kurudi nyuma hujaniconvice kabisa,bado traditional inafanya kazi tena sana tuuu,hata kama awe na MCY ya 30 wewe take 30-14,kwa hiyo mzunguko wake ni 16,ina maana siku ya 16 ndo fertile.+or-3.
 
Somo zuri ila sijaelewa. Nahitaji labda tuition. Ngoja nisome tena kwa umakini zaidi.
 
naomba kujuzwa iwapo mpenzi wako kamaliza bleed leo ,kesho yake ukakutana nae kimwili kunauwezekano wa kupata mimba au la
 
Kuhusu hili lina ukwel wowote mfano nimemaliza cku zangu za period (siku 5) nikafanya napenzi siku ya 6 hadi ya 10 kuna uwezekano wa kupata mimba? Naomba kusaidiwa
 
kama mwanamke amefanya mapenzi siku 3 au 4 au 2 au hata 1 kabla ya bleed yake anaweza kupata mimba?kwa anaejua anijuze maana hcho k2 knaubixhi xana hapa kijiwen!
 
naomba kuuliza mbegu zinauwezo wa kukaa mwilini mwa mwanamke kwa muda wa siku ngap? kabla ya kutunga mimba??? namaanisha mwanamke akifanya mapenzi siku ya 12 mbegu zinauwezo wa kukaa mpaka siku ya 14 zije zirutubishe yai mimba itungwe??
 
naomba kuuliza mbegu zinauwezo wa kukaa mwilini mwa mwanamke kwa muda wa siku ngap? kabla ya kutunga mimba??? namaanisha mwanamke akifanya mapenzi siku ya 12 mbegu zinauwezo wa kukaa mpaka siku ya 14 zije zirutubishe yai mimba itungwe??

mbegu zinauwezo wa kukaa ndani ya mwili wa mwanamke ndani ya masaa 48 hadi 72 xawa na cku 2 hadi 3 hvyo kuna hatari ya kupata mimba ukfanya mapenz cku ya 12 kam maelezo yako hapo yanaeleza kuwa cku ya 14 mwanamke yupo tayar kurutubixha.hvyo ucjaribu kaa nae mbali,ngoja tuone na wataalam zaidi wengine watakavyoelezea hali hii,huo n kwa ufaham wng nlioutoa kutoka kwa daktari mmoja ivi.thanks
 
Aise nashukru saana ila kuna ugumu wake make mpaka wanawake huwa hawajui siku zao za kubebe ujauzito
 
Back
Top Bottom