PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Mkoani Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tarimba Gulam Abbas, amesema Jimbo la Kinondoni linahitaji watu wa kufanya kazi na siyo watu wa kujifunza kufanya kazi, akiwataka wananchi hao kumchagua ili kufanya kazi.
Akizungumza na wananchi Jimboni humo Oktoba 27, 2025, Katika Mkutano uliofanyika Viwanja vya Vegas, vilivyopo Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni, amesema jimbo hilo linahitaji mtu mwenye nguvu ya kusikilizwa katika Bunge, kwaajili ya kuwatetea wananchi wake.
Soma: Tarimba: Kiongozi wa nchi lazima aheshimiwe, asidharauliwe, sisi tupo kumlinda
"Jimbo hili si jimbo la mzaha, si jimbo la watu kuja kujifunza kazi, jimbo hili ni la watu waje kufanya kazi, tunataka mtu ambaye akisimama bungeni, wabunge wenzake wanasimama wanamsikiliza", amesema Tarimba.
Tarimba amewataka wananchi wa eneo hilo kuwachagua viongozi ambao awali walifanya kazi walizoahidi na ambao watahudumu tena kwa miaka mitano ijayo katika kufanya maendeleo.