Mbunge wa Jimbo la Kinondoni na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Abbas Tarimba, amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni taasisi imara isiyoweza kuyumbishwa na mtu yeyote mwenye nia ovu ya kukipasua.
Akizungumza katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma, Tarimba alisema kuwa wananchi wamekielewa chama hicho kuwa msingi wa maendeleo ya haraka, hivyo mtu yeyote atakayeonyesha dalili za kukipasua chama hicho atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa wanachama.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Chama hiki kipo ndani ya mioyo yetu. Yeyote yule akionesha ishara za kutaka kuipasua CCM, tutampasua yeye kwanza. Tuko tayari kwa lolote lile," amesema kwa msisitizo.