PreGE2025 Tarimba: Yeyote yule akionesha ishara za kutaka kuipasua CCM, tutampasua yeye kwanza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hamuwezi mkajazana ccm halafu muwe na mawazo sawa, huo utakuwa ni utaahira, lazima pawepo na watu wenye mawazo tofauti na kinzani na mkiwapasua mtakuwa mnatenda makosa ya kijinai
 
Nguvu ya ccm ni kuendelea kukubalika na umma wa wananchi kwa kua kinapigania maslahi yao. CCM inapokua na viongozi fisadi isifikiri wataendelea kukubalika. Wajue siku umma wa wananchi wakiwachoka vitisho kama vya tarimba havitasaidia. Wananchi wataitosa. Siku hiyo kina tarimba watajikuta miti yote inateleza. Uhuni kama kuuza bandari, loliondo, mikataba kua siri kwa kuficha ufisadi hadi wazalendo kwenye system waibue yana mwisho.
CCM ikiongozwa na mafisadi itatemwa nguvu ni umma wa wananchi sio vigogo fisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…