Uchaguzi 2020 Tarime Mjini: Jackson Kangoye ampa masharti kumuunga mkono Kembaki, amtaka amrudishie gharama alizotumia kwenye kura za maoni

Uchaguzi 2020 Tarime Mjini: Jackson Kangoye ampa masharti kumuunga mkono Kembaki, amtaka amrudishie gharama alizotumia kwenye kura za maoni

Musachawenyu

Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
84
Reaction score
109
Katika hali ya kushangaa, jana Jackson Kangoye alimuita Michael Kembaki na kumpa masharti ya yeye kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu ngazi ya ubunge katika Jimbo la Tarime Mjini.

Jackson alimpa masharti Kembaki ya kwenda yeye binafsi bila wapambe wake. Lakini Kembaki alipokwenda akimkuta Jackson akiwa na wapambe wake.

Na siku hiyo ya jana kabla ya kumuita alifanya sherehe kwake, akachinja ng'ombe mmoja na kualika wajumbe nyumbani kwake ili kumuonyesha Kembaki kuwa ana nguvu.

Ikumbukwe Jackson Kangoye alikuwa mshindi wa kwanza na alihonga pesa nyingi, hadi laki 4 kwa mjumbe mmoja, hivyo ana maumivu na hasira kuwa alipoteza pesa nyingi.

Akiongea na wapambe wake alisema kuwa kama hatarudishiwa pesa zake bora uchaguzi uahirishwe na mchakato uanze upya (hapo hajafafanua namna ya kurudia mchakato upya).
 
Hawa ni wa chama kipi? Unatoa uzi uki-assume kuwa wana JF wote tunawafahamu. Hatuwafahamu.
Ni hao jamaa.
JamiiForums-1995350078_390x520.jpg
 
KAMBAE na KANGOE woote kama vipi tupilia mbali wekeni mbunge sahihi.
Huyo mmoja bado yuko ile CCM ya kina Membe hayuko na wakati pia sijui TAKUKURU wako wapi kwa hilo?
 
Back
Top Bottom