Tarime Mjini nako moto unaendelea

Tarime Mjini nako moto unaendelea

Mara nyingi ukizuia kitu fulani, unajenga hali ya watu kukitamani. Utaona watu watakavyokuwa wakifuruka kwenye mikitano ya CHADEMA. Watajaa kwa kuamini watasikia mambo mapya ambayo wamenyimwa kuyasikia kwa miaka 4.

Mikutano ya CCM itadoda kwa sababu watu wamekuwa wanawasikia wakati wote. Wanajua hakuna jipya watakalolisikia.

Wananchi watataka kupata maoni yoka kwa wapinzani juu ya ypte ambayo CCM imekuwa ikiwaambia jwa miaka 4.

CCM watakuwa na nini cha kuwaambia watanzania ili kuwapa hamasa mpya, zaidi ya reli, bwawa la umeme, ndege, vipande vya barabara za kwenye miji, ujenzi wa masoko na stand? Siyo kwamba mambo hayo ni madogo ila walikwishayasikia mara nyingi. Hulka ya binadamu ni kupenda kusikia mambo mapya.

Hulka ya binadamu, ni kutafuta anachokikosa. Kwa sasa, Watanzania wanachokikosa zaidi ya kitu chochote, ni uhuru na demokrasia yao. Serikali ifanye vyote lakini ikawanyima wananchi uhuru wao, wakati wote itashuhudia kukosa uungwaji mkono wa wananchi walio wengi.

Maputo pale Wareno walikaa zaidi ya miaka 500. Walitengeneza kila kitu, lakini wananchi hawakuyaona hayo yote. Waliingia kwenye mapigano na kuharibu hata vilivyokuwa vimetengenezwa ili kuwa na maamuzi juu ya maisha.
 
Halafu nimegundua kitu kimoja zile karatasi za kula pale kwenye yule mgombea wa kijani anaeutaka ufalme,kunawekwaga kauchawi,mtu anaweza kuna na akili zake timamu kwamba namchagua fulani wa upinzani lakini akifika pale anakuwa zombi mfawidhi anamdondoshea kura wa kijani
 
View attachment 1311600
View attachment 1311601
Chadema sasa inashambulia kama kansa ya damu inavyoshambulia wahanga
Mtamuua Magufuli wa watu unajua sometime nakuwa namwonea huruma nguvy anyotumia kufanya watu wampende na bado kuna harakati hizi za kumpinga na zinaungwa mkono kiasi hiki najikuta natafakari na kujiweka kwenye viatu vyake. I am human dont judge me for my emotions though!
 
siasa Ni hoja sio mapolis .mapolis walinde usalama Wa RAIA Na Mali zao
FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Chadema nao, haya mambo ni kizamani sana. Jiongezeni nyinyi! Subirini tamasha la Diamond huko Serengeti, akiwa jukwaani usiku, mpigieni simu live na muwaambie wananchi kuwa wana bahati,mnawapenda sana. Diamond atawahakikishia ushindi wa 100%. Acheni ushamba nyie.
 
Kalamu 1 namtuma Makene akuletee kadi ya Chadema unaonekana una madini fulani yanayoweza kusaidia
Nasubiri tu waTanzania wawakabidhi mikoba, halafu utaona moto nitakaowasha kuwachoma vidole vyenu kwa madudu mtakayokuwa mnawafanyia waTanzania.

Usisahau, wewe mwenyewe umewahi kunilalamikia humu humu JF na kunibandika kilemba cha kuwa 'agent' wa CCM. Umesahau?

Hapa ni 'equal opportunity' pande zote. Mstari ni mmoja tu ulionyooka - TANZANIA 'HURU'. KWA MAANA KAMILI YA NENO HILO.
 
Watanzania wanachokikosa zaidi ya kitu chochote, ni uhuru na demokrasia yao.
Na sina hakika kama CHADEMA na vyama vingine wamejipanga sawa sawa kulitimiza hili.

Huu ndio mtihani wao mkubwa kwa wananchi. Je, watafauru?
 
Back
Top Bottom