TARURA badilisheni mfumo huu wa maegesho ni wa ovyo sana

TARURA badilisheni mfumo huu wa maegesho ni wa ovyo sana

gango2

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2011
Posts
1,956
Reaction score
2,274
Habari,

Tarura hivi sasa mna mfumo wa ukusanyaji charges za maegesho kwa njia ya kielectronics. Huu mfumo kiukweli ni mfumo wa OVYO sana kwani unamuumiza sana mmiliki wa gari. Mfumo huu pia unatengeneza mwanya wa upotevu mapato sana kulinganisha na ule wa awali. Ninasema haya kwa sababu:

1. Sasa hivi hawa wanaoandika hizi charges hawaweki tena vile vikaratasi, yaani wao wanaandika charges bila kumjulisha mmiliki, kwa hiyo mmiliki anakuwa ana deni bila yeye kujua. (Na hivi mmeweka fine ya 10,000 hapa tatizo linakuwa kubwa sana)

2. Utaratibu unafahamika kuwa ukipaki gari zaidi ya dk 10 (kama sijakosea) ndio uchajiwe gharama za parking, lakini kwa sasa sio hivyo, Yaani hata ukipaki dk 2 na kuwasha hazard, unaandikiwa masikini bila hata kujua.

3. Sijui kama hamjui kuwa hawa wakusanyaji wenu wanakusanya sana fedha kwa kuwaambia wamiliki wa magari hawatawaandikia.

Hebu jaribuni basi kuwa wabunifu
1. Tengenezeni mfumo mtu akiandikiwa charges tu, apate notification kwenye simu yake, (hii ni very easy sana dereva ana leseni) ambayo imekuwa linked na NIDA, na makampuni ya simu

2. Wekani mfumo deni likiandikwa ili liwe validy lazima dereva afanye confirmation (either aweke namba yake ya leseni) kisha hizi fine zenu ndio zitokee hapo. Tena mki-link hizi fine mpya na leseni itakuwa very easy hata jeshi la polisi kuwasaidia katika ukusanyaji wa madeni yenu.
 
Sasa hivi wanapiga picha hata magari yanatembea barabarani. Juzi jumanne nimetoka posta nikalipia kwa simu baada ya kuuliza wapi risiti wakasema tumepiga tu picha. Nafika udsm naangalia nadaiwa mia tano tena na siku simama mahali.’
 
Kuwa na gari Tanzania hasa miji mikubwa ni anasa kweli...gari inakua kama kiwanda
 
Very well put. Message imewafikia wahusika bila shaka.
Habari,

Tarura hivi sasa mna mfumo wa ukusanyaji charges za maegesho kwa njia ya kielectronics. Huu mfumo kiukweli ni mfumo wa OVYO sana kwani unamuumiza sana mmiliki wa gari. Mfumo huu pia unatengeneza
 
Habari,

Tarura hivi sasa mna mfumo wa ukusanyaji charges za maegesho kwa njia ya kielectronics. Huu mfumo
Kuhusu notification TARURA wametangaza sana kuwa unaweza kusajili namba ya simu kwenye mifumo yao. Hapo unawaonea. Labda hayo mengine. Mimi hapa kila nikitoka parking baada ya masaa machache napewa notification.
 
Kwanza Kwa Nini ukipark gari ulipishwe tozo ? Je vyombo hivi vya usafiri havitakiwi kukanyaga ardhi ya mjini?
 
Si ueleze hapa namna ya kusajili hiyo namba
 
Msiwalaumu Tarura, Walaumuni e-GA maana akili zao ndio zimeishia hapo
 
CCM wametufanya watumwa katika nchi yetu. Walianza kukusanya mwanzoni kwa 2000's. Mpaka leo hawajajenga hata parking 1. Kuna sehemu nyingi sana tunapaki kwenye udongo wa Mungu halafu tunadaiwa pesa ya parking!
Kwanza Kwa Nini ukipark gari ulipishwe tozo ? Je vyombo hivi vya usafiri havitakiwi kukanyaga ardhi ya mjini?
 
Sasa hivi wanapiga picha hata magari yanatembea barabarani. Juzi jumanne nimetoka posta nikalipia kwa simu baada ya kuuliza wapi risiti wakasema tumepiga tu picha. Nafika udsm naangalia nadaiwa mia tano tena na siku simama mahali.’
Duh..
 
Habari,

Tarura hivi sasa mna mfumo wa ukusanyaji charges za maegesho kwa njia ya kielectronics. Huu mfumo kiukweli ni mfumo wa OVYO sana kwani unamuumiza sana mmiliki wa gari. Mfumo huu pia unatengeneza mwanya wa upotevu mapato sana kulinganisha na ule wa awali. Ninasema haya kwa sababu:

1. Sasa hivi hawa wanaoandika hizi charges hawaweki tena vile vikaratasi, yaani wao wanaandika charges bila kumjulisha mmiliki, kwa hiyo mmiliki anakuwa ana deni bila yeye kujua. (Na hivi mmeweka fine ya 10,000 hapa tatizo linakuwa kubwa sana)

2. utaratibu unafahamika kuwa ukipaki gari zaidi ya dk 10 (kama sijakosea) ndio uchajiwe gharama za parking, lakini kwa sasa sio hivyo, Yaani hata ukipaki dk 2 na kuwasha hazard, unaandikiwa masikini bila hata kujua

3. sijui kama hamjui kuwa hawa wakusanyaji wenu wana kusanya sana fedha kwa kuwaambia wamiliki wa magari hawatawaandikia.

Hebu jaribuni basi kuwa wabunifu
1. Tengenezeni mfumo mtu akiandikiwa charges tu, apate notification kwenye simu yake, (hii ni very easy sana dereva ana leseni) ambayo imekuwa linked na NIDA, na makampuni ya simu

2. wekani mfumo deni likiandikwa ili liwe validy lazima dereva afanye confirmation (either aweke namba yake ya leseni) kisha hizi fine zenu ndio zitokee hapo. Tena mki-link hizi fine mpya na leseni itakuwa very easy hata jeshi la polisi kuwasaidia katika ukusanyaji wa madeni yenu.
Wacha kelele kwenye 1, sajili namba yako ya gari kwenye namba yako ya simu kupitia *152*00# (4, 2, 3) utakuwa unapata meseji pindi ukiandikiwa gharama za parking.
 
Tarura parking fee ndio new baby in town kwa sasa ...hata bei ya mafuta tutasahau kuwq ilipanda
 
Back
Top Bottom