KERO TARURA irekebishe miundombinu ya Malolo - Tabora, Wananchi tunateseka kwa Mitaa kujaa maji

KERO TARURA irekebishe miundombinu ya Malolo - Tabora, Wananchi tunateseka kwa Mitaa kujaa maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
Ndugu zangu wana JF salaam, kuna jambo ambalo limekuwa kikwazo kwetu sisi wakazi wa Kata ya Malolo, Manispaa ya Tabora na Mkoa wa Tabora ambapo kama lisipofanyiwa kazi basi tutaendelea kuishi kwa kutaabika na wakati mwingine wenzetu kupoteza maisha kila kukicha.

Iko hivi, sisi wakazi wa Malolo, kwa mitaa tofauti tumekuwa tukisumbuliwa na changamoto ya makazi yetu kujaa maji mvua zinaponyesha, hii hali imesababishwa na Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) wanaojenga barabara mpya ya udhamini wa Benki ya Dunia yenye urefu wa zaidi ya Kilometa 10, kuamua kuelekeza maji kupitia makaravati kuja kwenye makazi ya watu pale mvua zinaponyesha hususani kipindi hiki cha Masika.
WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.01.43_1441ce39.jpg

WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.01.51_1f559753.jpg

WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.02.14_cf7c1f24.jpg
Ujenzi wa hiyo barabara inayoanzia Malolo Center kisha inakwenda kutokea Mwinyi Mwisho wa Lami (Sikanda) bado haujakamilika na kubwa ni kwamba Wananchi tunaokaa Maeneo hayo ndio tunaohangaika kila kukicha.

Maji yanaletwa na mitaro kwenye mazingira yetu yanazizunguka nyumba, inafikia wakati watoto wetu wanakuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha sababu ya maji kuzunguka makazi yetu hapa tunaweza kukaa hadi siku tatu maji bila kupungua.

Hapa Mtaa wa Msikitini, Kata ya Malolo kuna makazi ya watu zaidi ya nyumba 100 mpaka 200 (kwa makadirio ya chini) maji yanazingira maeneo yetu, mvua ikipiga sawasawa tunashindwa kwenda kwenye shughuli zetu za kuzalisha kipato sababu ya haya maji ambayo hayajatengenezewa utaratibu wa kusafiri hadi ambako yanatakiwa kwenda.

Kabla ya Manispaa ya Tabora kwa kushirikiana na TARURA kuanza ujenzi wa hii barabara, hali hapa kwetu ilikuwa afueni maana maji yalikuwa na njia yake lakini tangu waanze ile barabara kuchimba na kutengeneza makaravati, hali yetu ilianza kuwa mbaya kwa kuwa yale madaraja waliyojenga maji yalielekezwa kwenye makazi ya watu.

Hebu fikiria maji ya Tabora Mjini, Cheyo na mitaa mingine yanapokuja kwenye kata yetu tunakuwa kwenye hali gali? Kwa mantiki hiyo sisi tumetekezwa kwa kiwango kikubwa ndio maana tunaishi kama wakimbizi kwenye nchi yetu.
WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.02.53_d04f8594.jpg

WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.02.51_3d7de6c6.jpg
Mwaka 2024, Nchi ilikuwa inapata mvua kubwa hata sisi tulikuwa waathirika zaidi maana ilifikia wakati Jeshi la Zimamoto likawa linakuja kutuokoa baada ya maji kutokuwa na uelekeo sahihi na sisi tunachotaka ni kwamba, TARURA watengeneze njia ya haya maji ili yanapofurika na kufika kwenye makazi ya watu yapate pa kwenda na sio kutuama kwenye makazi ya watu.

Kutokana na maji haya kutuama kwenye kata yetu kwenye baadhi ya mitaa, tumeshapoteza watoto wanne ambao walikwenda kuogelelea walipodhani ni salama wakajikuta wamekwama kwenye udongo kwenye kina cha maji na kupoteza maisha yao, hii hali haikubaliki hata kidogo tunaziomba mamlaka kutuangalia wakazi wa Malolo ili tuepusha na hali hii.

Tumekuwa tukipata madhara makubwa hapa, watoto wetu wanaosoma Shule ya Msingi Milambo wamekuwa wakikaa hadi siku tano bila kwenda shule, hii imekuwa ikiathiri ukuaji wao kielimu kwa kiasi kikubwa sababu ya haya maji ambayo hayana uelekeo unaoeleweka hivyo mamlaka zifike kutunusuru na hii hali.

Mbali na elimu Miundombinu ya barabara na maji imekuwa ikiharibiwa mara kwa mara sababu ya maji kuwa mengi, wakati mwingine barabara imekuwa ikipasuka, sisi wenye magari tumekuwa tukishindwa hata kutumia barabara sababu ya kuharibika kutokana na hayo maji ambayo yanatoka Tabora mjini, yanatiririka kupitia mto Kenge na kuleta maji hadi kwenye makazi ya watu.

Ushauri wangu tusingojee madhara zaidi ya watu kuangukiwa na nyumba zao, watu kupoteza maisha sababu ya haya maji ndio hatua zichukuliwe badala yake hatua zichukuliwe sasa ambapo madhara machache yametokea katika maeneo yetu haya.

Kwako mwana JF.
WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.02.44_cccafb0c.jpg

WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.02.43_3ad8cee1.jpg

WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.02.49_4b637b65.jpg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.02.14_cf7c1f24.jpg
    WhatsApp Image 2024-12-30 at 16.02.14_cf7c1f24.jpg
    405.3 KB · Views: 4
Lakini mkuu, kuna mambo mengine wananchi hua tnakaza shingo na kuisingizia serikali bure.
Kwa wakazi wa Malolo, Ipuli na Malabi wengi mmejenga mabondeni na miaka michache nyuma maeneo hayo yalikua ni mashamba ya mipunga.
Binafsi sioni kama serikali inaweza ikawasaidia zaidi ya kuwataka muhame.
 
Back
Top Bottom