TARURA: Ni kweli Daraja la Mto Mngeta lilitumia Tsh. milion 31

TARURA: Ni kweli Daraja la Mto Mngeta lilitumia Tsh. milion 31

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
SIKU Moja baada ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi kutembelea Daraja la Mto Mngeta lililogharimu Sh Milioni 30 hatimaye Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Wilaya ya Kilombero ametolea ufafanuzi gharama za ujenzi huo.

Mhandisi Robert Magogo ambaye ni Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero ametolea ufafanuzi wa Ujenzi wa mradi huo akisema gharama zilizotajwa ni sahihi huku akieleza kuwa lina uwezo wa kudumu kwa miaka 10 hadi 15.

Akifafanua ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Magogo amesema Daraja hilo lina urefu wa Mita 40, kina cha Mto kikiwa ni Mita 4, upana wake Mita 5 na hivyo kufanya gharama za Daraja kuwa Milioni 27.

Mhandisi Magogo ameeleza kuwa gharama ya barabara kuingia na kutoka darajani ni Sh Milioni 4 na kufanya jumla yake iwe Sh Milioni 31.

" Urefu wa wa nguzo zilizotumika ni Mita 7 na unene wake ni Mita 0.5, Mbao ni Inchi 3 kwa 8 na Inchi 3 kwa 10 na aina ya Mti ambao Mbao zake zimetumika ni za Mti aina ya Mkarati, niwahakikishie kuwa daraja hili ni imara na litakua na uwezo wa kupitisha Tani 10 na litadumu kwa miaka 10 hadi 15," Amesema Magogo.

Kwa upande wake Mbunge Kunambi amesema Daraja hilo litaokoa uhai wa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekua wakipata changamoto ya kivuko kwani Mto huu una mamba ambao wamekua wakisababisha Vifo vya wananchi wetu," Amesema Kunambi.

WhatsApp%2BImage%2B2021-07-29%2Bat%2B9.44.28%2BPM.jpeg
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi (wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye Mtumbwi akivuka Mto Mngeta Februari mwaka huu ambapo aliitembelea Mto huo ukiwa hauna kivuko

WhatsApp%2BImage%2B2021-07-29%2Bat%2B9.46.38%2BPM.jpeg
Picha zikimuonesha Mbunge Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi akipita juu ya daraja la muda ambalo amefanikisha ujenzi wake. Daraja hili litakua na uwezo wa kupitisha Tani 10 na litadumu kwa muda wa miaka 10 hadi 15.

WhatsApp%2BImage%2B2021-07-29%2Bat%2B9.46.40%2BPM.jpeg
 
Mhandisi Robert Magogo ambaye ni Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero.
Mhandisi Magogo kaamua kuweka magogo ktk daraja ili kuenzi jina lake.

Picha zikimuonesha Mbunge Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi akipita juu ya daraja la muda ambalo amefanikisha ujenzi wake. Daraja hili litakua na uwezo wa kupitisha Tani 10 na litadumu kwa muda wa miaka 10 hadi 15.
"Daraja ni la muda", wakati huo huo linategemewa kudumu hadi miaka kumi na tano (15). Miaka 15 ni mda mfupi?
 
Na hapo ukute kuna kamsitu walienda kuzichinja
Tena wanaokata ni wafungwa.

Serikali kuna michezo ya kishenzi sana, vidaraja kama hivi ni vya kupigia hela. Miaka mitatu ijayo, watasema mbap zimeoza, na italetwa habari mwananchi mmoja kaliwa na mamba, basi madiwani watalambishwa laki laki, na kupitisha hoja, daraja jipya lijengwe. Procurement Officer na team yake wanalamba hata 15 Mil, maisha yanasonga.
 
Picha zikimuonesha Mbunge Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi akipita juu ya daraja la muda ambalo amefanikisha ujenzi wake. Daraja hili litakua na uwezo wa kupitisha Tani 10 na litadumu kwa muda wa miaka 10 hadi 15.
Ukihesabu idadi ya mbao, saruji, mawe, milingoti, misumari, kifusi, ufundi na 10% inazidi
 
Back
Top Bottom