Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Hivi huu Mkoa wa Tabora viongozi wa Wakala ya Barabara za Mjini na Vijijini TARURA wapo kweli?
Maana Barabara ya Madaraka iliyopo Mtaa wa Madaraka Manispaa ya Tabora imeharibika na inazidi kuharibika kila siku, kuna mashimo lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.
Nimeshuhudia zaidi ya mara nne watu wakinusurika kugongana wakati wakikwepa hayo mashimo kwenye ile barabara hivyo lazima hatua zichukuliwe.
Mvua kwa sasa ni kubwa na yale mashimo yaliyopo kwenye barabara hiyo yanaendelea kujaa maji na kuchimbika zaidi hawa TARURA watimize wajibu wao.