TASWA wampongeza Waziri Dkt. Pindi Chana kwa uteuzi, yatuma salamu kwa Simba, Yanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kinampongeza Dk. Pindi Hazara
Chana kwa kuteuliwa na Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Utamaduni,
Sanaa na Michezo mwanzoni mwa wiki hii.

Pia TASWA inampongeza Said Othman Yakub kwa kuteuliwa na Rais Samia kuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Uongozi mpya wa TASWA unawaahidi ushirikiano wa
kutosha viongozi hao kuhakikisha masuala ya utamaduni, sanaa na michezo yanapata mafanikio
makubwa nchini mwetu.

(B) Kila la heri Simba, Yanga na timu ya Taifa ya Riadha
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kinazitakia kila la heri timu za Simba na Yanga za Dar es Salaam, ambazo wikiendi hii zitakuwa na michezo ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). TASWA inaamini Simba na Yanga zitafanya kile ambacho Watanzania wengi tunakitaka wakifanye, nacho ni ushindi, hasa kwa vile watakuwa nyumbani Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

TASWA inaamini zimejiandaa vya kutosha, zina kila sababu ya kupeperusha vyema bendera ya nchi, tunawasihi mashabiki wote tuziombee timu zetu, kila mmoja kwa imani yake, bila shaka mambo
yatakuwa mazuri na hazitatuangusha.

Pia TASWA inaitakia mafanikio mazuri timu ya Taifa ya Riadha ambayo kesho Jumamosi Februari 18,
2023 itashiriki mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika "World Cross Country Championship' huko
nchini Australia.

Alfred Lucas
KatibuMkuu TASWA
Februari 17, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 002_page-0001 (1).jpg
 
Chawa kazini.
 
Back
Top Bottom