DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Jifunze kujua maaan ya lahaja kwanza inaonekana hata kiswahili na lahaja hujuiShida ilianzia hapa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jifunze kujua maaan ya lahaja kwanza inaonekana hata kiswahili na lahaja hujuiShida ilianzia hapa.
Sio kweli...Kuna Yesu wa akina Toni Kapora, wa akina Mwamposa, Makanisa ya kiroho na yale ya RC/KKKT hawa ni Yesu tofauti ujue
Dini zimejaa vitishoYaan ukianza kutumia COMMON SENSE kwenye mambo ya kiroho unapotoka....
Naona umeshiba + Kiburi Cha uzima unajikuta unaanza ku challenge dini (YESU KRISTO WA NAZARETH)
Acha kumtizama YESU KRISTO WA NAZARETH katika hiyo perception (Angle)uliyo mtizama Kuna mengi aliyo anayo yafanya mpaka muda huu ....
Wasalaam
Ficha umaamuma wako. Kwa nini unauonesha kwa watu kama vile ni kitu cha kujivunia?Jifunze kujua maaan ya lahaja kwanza inaonekana hata kiswahili na lahaja hujui
Sijajivuna ila nimejibu nilichoulizwa kawaida yangu sina hiyana kwenye kutoa majibu..Ficha umaamuma wako. Kwa nini unauonesha kwa watu kama vile ni kitu cha kujivunia?
Hujui kiswahili na unataka kuhalalisha kharamu. Hakuna tunaendaga, tunakulaga ni maneno wanayotumia wasiojua kiswahili. Unarekebishwa unashupaza shingo.Sijajivuna ila nimejibu nilichoulizwa kawaida yangu sina hiyana kwenye kutoa majibu..
Kuna kitu vijana mnashindwa kujua...Sijui walimu wenu w Kiswahili walikuwa 'akina nani?
Ngoja nikufundishe kidogo kwa elimu yangu ya Maamuma niliyopata miaka ya 80 na 90..
Kujivuna ni hali ya mtu kujiona kuwa bora kuliko wengine, au kujisifu kupita kiasi juu ya uwezo au mali zake.
Kwa Tafsiri hiyo hakuna sehemu nimejivuna labda huenda kutamka kwangu vile kumekufanya wewe ujihisi inferior (Io sio maana yangu) unisamehe sana nilichojibu ni swali nililo ulizwa na nimelijibu kwa makini bila kuongeza chumvi yoyote
Na ukiniuliza kuhusu Elimu hiyo Najihisi niko Proud na elimu yangu ntakujibu, Ndyo kwa sababu kuna wengine hawana na nashukuru kwa kidogo nilichonacho..
Ila bado sijajua mantiki ya kuni Attack au kufanya Character assasin ni nini?
Kama una hoja weka mezani Acha Kuumia..,Kuwa na Religious Torelance capability..
Hujui kiswahili na unataka kuhalalisha kharamu. Hakuna tunaendaga, tunakulaga ni maneno wanayotumia wasiojua kiswahili. Unarekebishwa unashupaza shingo.
Unakazana sana katika kukazania umaamuma.Haha Sawa 😅😅
Ngoja nikupe somo kidogo kijana pengine sio kosa lako...
Kiswahili hakikuwa sawa kama kilivyo sasa, Kiswahili kilichoongewa zamani kilikuwa kila sehemu na kiswahili chake....Na hizo ndo ziliitwa Lahaja..
Kulikuwa na lahaja nyingi sana..
(Yaani kulikuwa n Viswahili vingi sana hii ilitokana na kukua na kuimarika kwa kiswahili kwa kuchanganya Lugha ya kibantu,Kiarabu na baadhi ya lugha kama kongo)
Hizi lahaja ziligawanyika kwenye makundi mawili
- Lahaja za Pwani: Hizi ni lahaja zinazo/zilizozungumzwa katika maeneo ya pwani ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar, na Pwani. Lahaja hizi zina sifa ya kuwa na msamiati wa kipekee unaohusiana na maisha ya Pwani na Kidgo lugha ya kiarabu na huitwa lahaja sanifu
- Lahaja za Bara: Hizi ni lahaja zinazo/zilizozungumzwa katika maeneo ya bara ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Iringa, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Geita, Kagera, na Rukwa.
Mifano baadhi wa hizo lahaja ni
kutokana na kila lahaja zilijiona bora na kila moja iliona ni sahihi kuliko lahaja nyingine (Ina kiswahili sanifu kuliko nyingine)
- Kiunguja: Hii inazungumzwa katika kisiwa cha Unguja na sehemu za pwani ya Tanzania.
- Kimvita: Hii inazungumzwa katika mji wa Mombasa, Kenya, na katika baadhi ya maeneo ya pwani ya Tanzania. Sana sana Tanga..
- Kimrima: Hii ni lahaja inayozungumzwa katika mji wa Tanga, eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
- Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
- Kingwana: eneo la Kigoma na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Shikomor: Kiswahili cha Komoro
- Sheng: Kiswahili cha Nairobi (Kenya)
- Kinyamwezi ,
- Kihadimu (Kimakunduchi),
- Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
- Kipate: eneo la Pate, visiwa vya pate (Kenya)
- Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
- Kibajuni: magharibi mwa visiwa vya pate
- Kivumba: kisiwa cha Vumba na kaskazini kwa Tanga (Tanzania)
- Kimtang'ata: Mtang'ata, mkoa wa Tanga (Tanzania)
Mwaka 1924 lahaja ya Kiunguja (lahaja ya Zanzibar) iliteuliwa kuwa lahaja ya usanifishaji dhidi ya lahaja zingine.
Januari 1, 1930 iliundwa Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki iliyoitwa Inter Territorial Swahili Language Committee, ili kuvunja lahaja zingine zote Lakini haikuwa kama walivyopanga..hii ilikuwa inahusisha nxhi zote zilizokuwa zinaongea kiswahili kipindi hicho
mwaka 1954 Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa chini ya Mwalimu Julius Nyerere;
Kiliendeleza matakwa ya inter Territorial Swahili Language Committee ambacho chama hicho kilitumia Kiswahili chenye lahaja ya kiunguja katika harakati za kupigania uhuru.
sasa Elewa hiki kuwa..
Kimvita: Kwa miaka ya zamani ndo ilikuwa lahaja kubwa na ya kisomi ikitungiwa mashairi kuliko Kiunguja, Ambacho sasa hivi ndo unajitia kuwa ni ndo kiswahili...
SASA NIRUDI KWENYE HOJA YAKO
sasa baada ya Somo refu narudi kwenye Hoja yako ya mimi kuwa kichwa Ngumu kwa kusema maneno yafuatayo....
Tunakulaga ,Tunaendaga
Zote hizi ni lahaja za bara mikoa ya kusini na Hutumiwa na watu Watokao Mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini pia kama Mbeya Iringa,Na mikoa mingine...
Kiswahili hiki kwa mfano Tunaendaga kimetokana na neno "Twendaga" au "Tuendaga"
Ambalo lahaja hii imetoka katika lugha ya kibantu kutoka msumbuji mikoa ya Cabo Delgado, Nampula, na Zambezia. Katika mikoa hii, neno "Tuendaga" hutumika badala ya neno "Tunaenda"...
Yaani "Twe", " tue " inamaanisha na kubeba Nafsi yaani Tuna na "Endaga" linabeba tafsiri ya kisarufi inayomaanisha muda Enda maana yake Kitendo na Ga ni Hali iliyopo hali ya kuendelea...
Sasa Ninachokushauri usiwe unapinga au kukosoa kitu kama huna elimu nacho au huna ujuzi nacho au hujui chochote kukuhusu wapo watakaokusifia kufanya hivyo (Wanakupoteza) ila wapo sisi tusiopenda upotee
Unajua kubishana na wewe ni kuonekana mimi na wew tuna hali sawa..Unakazana sana katika kukazania umaamuma.
Hali zetu si sawa. Ndiyo maana unagoma kuelewa. Unalazimisha upotofu uwe sawa.Unajua kubishana na wewe ni kuonekana mimi na wew tuna hali sawa..
Unajua hata kuanzisha Conversation na wewe wakati nikijua wewe ni chizi ni kujirisk tu akili yangu..
Kina mwamposa wanaponya pia, kina nani yule wa kolomije anafufua waliokufa, fasyforwaf 500yrs to come watasikia stori kama za yesuYESU alikuwa anafanya ISHARA na MIUJIZA mbalimbali.
Kama: kuponya viwete, kuponya vipofu, kufufua wafu, kutoa Pepo wachafu, Kuamuru dhoruba, kuongeza vyakula, kutakasa wakoma, n.k.
Masuala ambayo yanafanywa na watu wa MUNGU PEKEE YAO. ISSUE ya mwanamke KAHABA ni issue ya kujinyenyekeza na kuomba msamaha kutokana na dhambi za huyo KAHABA.
LAKINI, lengo la YESU kuja ni kukomboa watu kutokana na utumwa wa dhambi, na watu hao ni lazima wajinyenyekeze na kujishusha.
KIFUPI: YESU angekuja TANZANIA watu wengi wangemwamini kutokana na ishara na MIUJIZA ambayo angeifanya.
FIKIRIA jinsi watu wanavyowafuata mitume na manabii ambao hawajafanya ishara yoyote zaidi ya kusababisha vifo vya watu na umasikini pamoja na kuwapiga fedha ndefu( halafu atokee mtu anayefufua wafu na kuponya viwete, vipofu, nk. Asifuatwe?, Nani kasema?)
Wakati wa Yesu dunia nzima haikuwa hata na watu mamilioni.Wee jamaa kama una sikio la kusikia nisikilize! Pamoja na ukweli ya kwamba uliyoyasema ni kweli, lakini Yesu alijitofautisha na kuwa mtu wa ajabu kuwahi kutokea kwa miujiza, busara, maarifa, unyenyekevu, huruma, n.k. kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuishi! Alithibitisha torati ya Musa ya kuwa yule aliyetabiriwa kwa torati na manabii ndiye na kitendo cha kutomwamini kinawatia hatiani ya kwanini hawakumwamini! Baadhi ya miujiza aliyoitenda kuthibitisha Ndiye ni pamoja na:
1. Kufufua mtu aliyekufa siku 3 kaburini (lazaro),
2. Kutembea juu ya maji,
3. Kulisha mamillioni ya watu kwa mkate mmoja na samaki wawili,
4. Kujua maandiko yote ya torati bila kufundishwa,
5. kuponya viwete, vipofu, ukoma, nk, n.k, n.k; kwa ushahidi huu pamoja na unyenyekevu wa kukaa na watu waliotengwa na jamii kwa kuonekana hawafai sijui wana dhambi; vilimtofautisha na binadamu yeyote na hawakuwa na udhuru kwanini hawakumwamini?
Sababu nyingine kubwa ni kufufuka katika wafu na kuwatokea watu wengi pia mwili wake kutoonekana kaburini licha ya kuweka walinzi kulilinda kaburi. Sababu nyingine ni hile hali ya kustahimili mateso kwa masaa zaidi ya tisa ya kupigwa mijeredi na kujeruhiwa kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuishi kwa kuchubuliwa na kubeba msalaba mzito! Hapakuwahi kutokea binadamu wa kuteswa kama Yesu alafu asife!
Binadamu wa kawaida ndani ya dakika au saa moja lazima ufe! Yesu alistahimili mateso ya kila namna ili binadamu tunapopitia magumu tusiwe na sababu ya kupinga wokovu! Naishia hapa kwa ujasiri mkubwa ya kwamba maisha ya Yesu hayakuwa maisha ya binadamu wa kawaida. By the way!
Akirudi atarudi kama mfalme na wala hatakanyaga ardhi na walokole atawanyakua juu na kukutana nao mawinguni! Hata hivyo nguvu za kuwezesha walokole kupaa na kunyakuliwa zitakuwa ndani yao kutokana na kazi za utumishi alizowapa wamtumikie!
Kuna walokole watashindwa kupaa na kubaki hapa duniani na kupitia mateso kama wale ambao hapo mwanzo walibeza maandiko!
Maisha ya sasa duniani walokole bado ni wachache! Wengi ni mapandikizi ya mpinga Kristo! Hata hivyo wanayohubiri ni kweli ya neno la Mungu! Mungu anaangalia Neno bila kujali linahubiriwa na nani?
[emoji1787]Alikwenda Kenya akawaambia wamchangie mabati ya kuezekea nyumba
Mkuu huamini!!?[emoji1787]