Taswira ya Yesu anayehubiriwa ni tofauti na Yesu halisi

Dini zimejaa vitisho
 
Ficha umaamuma wako. Kwa nini unauonesha kwa watu kama vile ni kitu cha kujivunia?
Sijajivuna ila nimejibu nilichoulizwa kawaida yangu sina hiyana kwenye kutoa majibu..

Kuna kitu vijana mnashindwa kujua...Sijui walimu wenu w Kiswahili walikuwa 'akina nani?

Ngoja nikufundishe kidogo kwa elimu yangu ya Maamuma niliyopata miaka ya 80 na 90..

Kujivuna ni hali ya mtu kujiona kuwa bora kuliko wengine, au kujisifu kupita kiasi juu ya uwezo au mali zake.

Kwa Tafsiri hiyo hakuna sehemu nimejivuna labda huenda kutamka kwangu vile kumekufanya wewe ujihisi inferior (Io sio maana yangu) unisamehe sana nilichojibu ni swali nililo ulizwa na nimelijibu kwa makini bila kuongeza chumvi yoyote

Na ukiniuliza kuhusu Elimu hiyo Najihisi niko Proud na elimu yangu ntakujibu, Ndyo kwa sababu kuna wengine hawana na nashukuru kwa kidogo nilichonacho..

Ila bado sijajua mantiki ya kuni Attack au kufanya Character assasin ni nini?

Kama una hoja weka mezani Acha Kuumia..,Kuwa na Religious Torelance capability..
 
Hujui kiswahili na unataka kuhalalisha kharamu. Hakuna tunaendaga, tunakulaga ni maneno wanayotumia wasiojua kiswahili. Unarekebishwa unashupaza shingo.
 
Hujui kiswahili na unataka kuhalalisha kharamu. Hakuna tunaendaga, tunakulaga ni maneno wanayotumia wasiojua kiswahili. Unarekebishwa unashupaza shingo.

Haha Sawa 😅😅
Ngoja nikupe somo kidogo kijana pengine sio kosa lako...

Kiswahili hakikuwa sawa kama kilivyo sasa, Kiswahili kilichoongewa zamani kilikuwa kila sehemu na kiswahili chake....Na hizo ndo ziliitwa Lahaja..

Kulikuwa na lahaja nyingi sana..

(Yaani kulikuwa n Viswahili vingi sana hii ilitokana na kukua na kuimarika kwa kiswahili kwa kuchanganya Lugha ya kibantu,Kiarabu na baadhi ya lugha kama kongo)

Hizi lahaja ziligawanyika kwenye makundi mawili
  • Lahaja za Pwani: Hizi ni lahaja zinazo/zilizozungumzwa katika maeneo ya pwani ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar, na Pwani. Lahaja hizi zina sifa ya kuwa na msamiati wa kipekee unaohusiana na maisha ya Pwani na Kidgo lugha ya kiarabu na huitwa lahaja sanifu
  • Lahaja za Bara: Hizi ni lahaja zinazo/zilizozungumzwa katika maeneo ya bara ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Iringa, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Geita, Kagera, na Rukwa.

Mifano baadhi wa hizo lahaja ni
  • Kiunguja: Hii inazungumzwa katika kisiwa cha Unguja na sehemu za pwani ya Tanzania.
  • Kimvita: Hii inazungumzwa katika mji wa Mombasa, Kenya, na katika baadhi ya maeneo ya pwani ya Tanzania. Sana sana Tanga..
  • Kimrima: Hii ni lahaja inayozungumzwa katika mji wa Tanga, eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
  • Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
  • Kingwana: eneo la Kigoma na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
  • Shikomor: Kiswahili cha Komoro
  • Sheng: Kiswahili cha Nairobi (Kenya)
  • Kinyamwezi ,
  • Kihadimu (Kimakunduchi),
  • Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
  • Kipate: eneo la Pate, visiwa vya pate (Kenya)
  • Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
  • Kibajuni: magharibi mwa visiwa vya pate
  • Kivumba: kisiwa cha Vumba na kaskazini kwa Tanga (Tanzania)
  • Kimtang'ata: Mtang'ata, mkoa wa Tanga (Tanzania)
kutokana na kila lahaja zilijiona bora na kila moja iliona ni sahihi kuliko lahaja nyingine (Ina kiswahili sanifu kuliko nyingine)

Mwaka 1924 lahaja ya Kiunguja (lahaja ya Zanzibar) iliteuliwa kuwa lahaja ya usanifishaji dhidi ya lahaja zingine.
Januari 1, 1930 iliundwa Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki iliyoitwa Inter Territorial Swahili Language Committee, ili kuvunja lahaja zingine zote Lakini haikuwa kama walivyopanga..hii ilikuwa inahusisha nxhi zote zilizokuwa zinaongea kiswahili kipindi hicho

mwaka 1954 Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa chini ya Mwalimu Julius Nyerere;
Kiliendeleza matakwa ya inter Territorial Swahili Language Committee ambacho chama hicho kilitumia Kiswahili chenye lahaja ya kiunguja katika harakati za kupigania uhuru.

sasa Elewa hiki kuwa..
Kimvita: Kwa miaka ya zamani ndo ilikuwa lahaja kubwa na ya kisomi ikitungiwa mashairi kuliko Kiunguja, Ambacho sasa hivi ndo unajitia kuwa ni ndo kiswahili...


SASA NIRUDI KWENYE HOJA YAKO

sasa baada ya Somo refu narudi kwenye Hoja yako ya mimi kuwa kichwa Ngumu kwa kusema maneno yafuatayo....
Tunakulaga ,Tunaendaga

Zote hizi ni lahaja za bara mikoa ya kusini na Hutumiwa na watu Watokao Mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini pia kama Mbeya Iringa,Na mikoa mingine...

Kiswahili hiki kwa mfano Tunaendaga kimetokana na neno "Twendaga" au "Tuendaga"
Ambalo lahaja hii imetoka katika lugha ya kibantu kutoka msumbuji mikoa ya Cabo Delgado, Nampula, na Zambezia. Katika mikoa hii, neno "Tuendaga" hutumika badala ya neno "Tunaenda"...
Yaani "Twe", " tue " inamaanisha na kubeba Nafsi yaani Tuna na "Endaga" linabeba tafsiri ya kisarufi inayomaanisha muda Enda maana yake Kitendo na Ga ni Hali iliyopo hali ya kuendelea...


Sasa Ninachokushauri usiwe unapinga au kukosoa kitu kama huna elimu nacho au huna ujuzi nacho au hujui chochote kukuhusu wapo watakaokusifia kufanya hivyo (Wanakupoteza) ila wapo sisi tusiopenda upotee
 
Reactions: Cyb
Unakazana sana katika kukazania umaamuma.
 
Unajua kubishana na wewe ni kuonekana mimi na wew tuna hali sawa..

Unajua hata kuanzisha Conversation na wewe wakati nikijua wewe ni chizi ni kujirisk tu akili yangu..
Hali zetu si sawa. Ndiyo maana unagoma kuelewa. Unalazimisha upotofu uwe sawa.
 
Na umesahau ni Yesu huyohuyo aliyemwambia mwanamke aliyefumaniwa akizini "wala mimi hata sikuhukumu, enenda zako, usitende dhambi tena", au huyohuyo aliyeponya wagonjwa, kufufua wafu, kulisha watu elfu 5. Huyohuyo aliyelazimika kuanza utume wake kwa kufuata ombi la mama yake Maria alipoomba afanye muujiza wa divai kwa kumwambia mwanaye "hawana divai", Yesu alimjibu, "...mama, muda wangu bado...." lakini alisimama na kufanya alichoambiwa na mama yake.

Yet ni Yesu huyohuyo, aliyekuwa msalabani akiwa amepigiliwa misumari mikononi na miguuni na shada la miiba limechomekwa kwa nguvu kichwani huku akiwa amechakazwa vibaya sana kwa vipigo tangu alfajiri ya siku hiyo, lakini bado akamwangalia mwanafunzi wake mmoja na kumkabidhi mama yake Maria, yaani katika hali ya maumivu yale bado alifikiria hatma ya mama yake na kufanya mpango wa kuhakikisha anabaki mikono salama.
Na katika hali hiyohiyo ya taabu aliweza kuwaambia wanawake waliokuwa wanamlilia kuwa "msinililie mimi, vililieni vizazi vyenu" na kuwakumbusha mambo magumu yajayo.

Wewe unataka kusema nini kwa mfano, maana hakuwa mtu wa kufake mambo, alikuwa straight kwa kila fact, hata hao makahaba na hao wengine umesoma response yake kwanini ali hang out nao? Na usisahau huyu alikuwa Mungu katika mwili, aliona hadi rohoni, hakuwa katika hali ya kujudge watu kama tunavyofanya sisi, wale wanaojifanya wasafi tunaamini ni wasafi kweli na kuwahukumu wengine kisa hawameet expectations zetu? There was nothing wrong with Him, alifanya kila kitu kwa usahihi. Msome vizuri huyo Yesu utaacha hayo mawazo potofu, na umkemee sana shetani anayekupa mawazo hayo!
 
Kina mwamposa wanaponya pia, kina nani yule wa kolomije anafufua waliokufa, fasyforwaf 500yrs to come watasikia stori kama za yesu
 
Umewaza sahihi kabisa, kipindi hicho Yesu alikuwa kama hawa wapinzani wa leo. Yaani kuna rais wa nchi halafu anatokea mtu anajiita raisi pia. Huo ni uhaini.

Then, amekua huku wanamuona na kumjua, ghafla anawaambia yeye mwana wa Mungu. Ngumu kuamini hata leo tusingemwamini.

So, waliomsulubisha hawakukosea.
 
Wakati wa Yesu dunia nzima haikuwa hata na watu mamilioni.
Wakati huo idadi ya nchi huenda ni kijiji kwa sasa
Utaacha huu ukweli naokupa utakimbilia jibu lenu "haya ni mambo ya kiroho"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…