Kwa ujumla mechi ilikuwa ya kiwango kizuri na cha kuridhisha kwa mtazamaji kwa vipindi vyote viwili.
1. Simba walitawala sn kipindi cha kwanza na km wangeacha kucheza show game na kucheza objective football wangeweza kupata magoli mengi zaidi.
2. Azam hawakuwa na mpango kazi sahihi wa kuwazuia viungo hatari wa Simba hasa Chama kwani alikua huru kufanya anachotaka. Km mnakumbuka mechi ya Simba vs Prison iliyoisha 0:0 mtaelewa ninachomaanisha.
3. Azam walitoa zawadi ya magoli yote ya Simba. Ukiangalia magoli waliyofunga Simba yalitokana na uzembe wa hali ya juu ambao usingetegemea ufanywe na wachezaji wa timu kubwa km Azam.
Goli la kwanza kona inapigwa wanakabia macho, halafu krosi inapigwa Yakubu akiwa amekabana na Nyoni haruki juu na kumwacha Nyoni apige kichwa. Lakini pia kipa naye hasaidii kufuta makosa ya beki wake anasita kudaivi akidhani mpira unatoka mwishowe goli linaingia.
Goli la pili ni uzembe usioelezeka wa Agrey Morisi. Goli la 3 la Kagere ni uzembe wa wazi wa kipa Lazaki Abalora. Mpira wa kudaka kabsa tena haukuwa na nguvu anafanya masihara mpira ukamponyoka na kuwa goli. Kwangu huwa sielewi ni kwanini Azam wanamng'ang'ania Lazaki ambaye ana utoto, masihara na uzembe mwingi sana unaigharimu timu mara kwa mara.
4. Refa aliwanyima penalti ya wazi Azam FC. Sjui warefa wetu wanatafsiri gani kuhusu penalti. Wao alifanya faulo 2 kwa mkupuo. Kwanza alimvuta Kipagwile na kisha akamkwatua. Pia tumeona mara kadhaa Morison akikwatuliwa kwa staili ile ile lakini Marefa hawatoi penalti.
Madhara ya makosa kama haya tutayaona pale timu zetu zitakapocheza na waarabu au timu za A. Magharibi.
Mwisho: Kilichowaponza Azam dhidi ya Simba ni uzembe wao wenyewe. Kwanza, uzembe wa kuwapa Simba wachezaji bora 4 ambao wote walianza mchezo wa jana, ambao wanaijua vizuri Azam ndani nje. Bila kumsahau pia babu Pascal Wawa ambae na walimuacha akiwa na ubora wake bila sababu za msingi.
Pili, ni uzembe na Lakia walioyafanya uwanjani yakawaghalimu moja kwa moja.
Sent using
Jamii Forums mobile app