Tathimini ya mechi ya Azam vs Simba

Tathimini ya mechi ya Azam vs Simba

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Kwa ujumla mechi ilikuwa ya kiwango kizuri na cha kuridhisha kwa mtazamaji kwa vipindi vyote viwili.

1. Simba walitawala sn kipindi cha kwanza na km wangeacha kucheza show game na kucheza objective football wangeweza kupata magoli mengi zaidi.

2. Azam hawakuwa na mpango kazi sahihi wa kuwazuia viungo hatari wa Simba hasa Chama kwani alikua huru kufanya anachotaka. Km mnakumbuka mechi ya Simba vs Prison iliyoisha 0:0 mtaelewa ninachomaanisha.

3. Azam walitoa zawadi ya magoli yote ya Simba. Ukiangalia magoli waliyofunga Simba yalitokana na uzembe wa hali ya juu ambao usingetegemea ufanywe na wachezaji wa timu kubwa km Azam.

Goli la kwanza kona inapigwa wanakabia macho, halafu krosi inapigwa Yakubu akiwa amekabana na Nyoni haruki juu na kumwacha Nyoni apige kichwa. Lakini pia kipa naye hasaidii kufuta makosa ya beki wake anasita kudaivi akidhani mpira unatoka mwishowe goli linaingia.

Goli la pili ni uzembe usioelezeka wa Agrey Morisi. Goli la 3 la Kagere ni uzembe wa wazi wa kipa Lazaki Abalora. Mpira wa kudaka kabsa tena haukuwa na nguvu anafanya masihara mpira ukamponyoka na kuwa goli. Kwangu huwa sielewi ni kwanini Azam wanamng'ang'ania Lazaki ambaye ana utoto, masihara na uzembe mwingi sana unaigharimu timu mara kwa mara.

4. Refa aliwanyima penalti ya wazi Azam FC. Sjui warefa wetu wanatafsiri gani kuhusu penalti. Wao alifanya faulo 2 kwa mkupuo. Kwanza alimvuta Kipagwile na kisha akamkwatua. Pia tumeona mara kadhaa Morison akikwatuliwa kwa staili ile ile lakini Marefa hawatoi penalti.

Madhara ya makosa kama haya tutayaona pale timu zetu zitakapocheza na waarabu au timu za A. Magharibi.

Mwisho: Kilichowaponza Azam dhidi ya Simba ni uzembe wao wenyewe. Kwanza, uzembe wa kuwapa Simba wachezaji bora 4 ambao wote walianza mchezo wa jana, ambao wanaijua vizuri Azam ndani nje. Bila kumsahau pia babu Pascal Wawa ambae na walimuacha akiwa na ubora wake bila sababu za msingi.
Pili, ni uzembe na Lakia walioyafanya uwanjani yakawaghalimu moja kwa moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulipomtaja yule Bw mpiga 'viwiko' wakati mpira umesimama ktk pointi yako namba 4 , umeshajisema we ni shabiki wa timu gani na hii sio tathmini bali ushabiki. Sasa tunasema subiri tar 8
 
Nyie mbutembute fc mnashida sana kwa hiyo jana makosa wamefanya Azam tu Simba hawajafanya makosa na hayo makosa ya waamuzi umeyaona waliyofanyiwa Azam tu.
Inavyoonekana wewe ni shabiki lialia wa yebo yebo na matokeo ya jana yamekuumiza sana.mkuu huu ni mwanzo tar 8/3 utateseka zaidi.
 
Simba na YANGA znajulikana kuwa ni timu bora na kubwa Tz. Nimeeleza mapungufu mengi ya upande wa Azam nikiamini si story au ajabu Azam kufungwa na Simba. Sote tulitegemea Azamu waje na suprise package ili kuizuia Simba. Ni km ambavyo isingekua story km Watford wangefungwa na Liverpool,lakn baada ya Liverpool kufungwa ikawa story dunia nzima. Makocha wengi watarudia kuitazama hiyo mechi mara nyingi ili kujua ni mbinu gani Watford walitumia kuizuia na kuifunga Liverpool. Uzuri na ubora wa Simba unajulikana ni kupoteza mda kuuelezea.
Tathimini yako imekaa kishabiki zaidi, nahisi unatathimini huku unaumia, kwanza tathimini gani ya upande mmoja tu, pili mpira ni mchezo wa makosa, ukifanya makosa ndio utakapo adhibiwa,

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwandiko wa Mwl. Kashasha kabisa huu. Safi sana kwa uchambuzi murua ama kwa hakika imependeza.
Siyo kweli! Mwalimu Kashasha hawezi kuandika pumba hizi! Huwezi paribu anakutanaribuukamkosoa rasmi refarii kuwa hakutoa penati. Ulaya ukifanya hivyo unaadhibiwa!! Ni ripoti ya kamisaa tu inayoweza kumkosoa rasmi refarii, wala kocha hana ubavu huo!!! akijaribu anakutana na rungu LA FA
 
Kwa ujumla mechi ilikuwa ya kiwango kizuri na cha kuridhisha kwa mtazamaji kwa vipindi vyote viwili.

1. Simba walitawala sn kipindi cha kwanza na km wangeacha kucheza show game na kucheza objective football wangeweza kupata magoli mengi zaidi.

2. Azam hawakuwa na mpango kazi sahihi wa kuwazuia viungo hatari wa Simba hasa Chama kwani alikua huru kufanya anachotaka. Km mnakumbuka mechi ya Simba vs Prison iliyoisha 0:0 mtaelewa ninachomaanisha.

3. Azam walitoa zawadi ya magoli yote ya Simba. Ukiangalia magoli waliyofunga Simba yalitokana na uzembe wa hali ya juu ambao usingetegemea ufanywe na wachezaji wa timu kubwa km Azam.

Goli la kwanza kona inapigwa wanakabia macho, halafu krosi inapigwa Yakubu akiwa amekabana na Nyoni haruki juu na kumwacha Nyoni apige kichwa. Lakini pia kipa naye hasaidii kufuta makosa ya beki wake anasita kudaivi akidhani mpira unatoka mwishowe goli linaingia.

Goli la pili ni uzembe usioelezeka wa Agrey Morisi. Goli la 3 la Kagere ni uzembe wa wazi wa kipa Lazaki Abalora. Mpira wa kudaka kabsa tena haukuwa na nguvu anafanya masihara mpira ukamponyoka na kuwa goli. Kwangu huwa sielewi ni kwanini Azam wanamng'ang'ania Lazaki ambaye ana utoto, masihara na uzembe mwingi sana unaigharimu timu mara kwa mara.

4. Refa aliwanyima penalti ya wazi Azam FC. Sjui warefa wetu wanatafsiri gani kuhusu penalti. Wao alifanya faulo 2 kwa mkupuo. Kwanza alimvuta Kipagwile na kisha akamkwatua. Pia tumeona mara kadhaa Morison akikwatuliwa kwa staili ile ile lakini Marefa hawatoi penalti.

Madhara ya makosa kama haya tutayaona pale timu zetu zitakapocheza na waarabu au timu za A. Magharibi.

Mwisho: Kilichowaponza Azam dhidi ya Simba ni uzembe wao wenyewe. Kwanza, uzembe wa kuwapa Simba wachezaji bora 4 ambao wote walianza mchezo wa jana, ambao wanaijua vizuri Azam ndani nje. Bila kumsahau pia babu Pascal Wawa ambae na walimuacha akiwa na ubora wake bila sababu za msingi.
Pili, ni uzembe na Lakia walioyafanya uwanjani yakawaghalimu moja kwa moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anzeni kulialia mapema na Morison wenu, tarehe 8 inakula kwenu. Yaani tarehe 4 unaanza kulalamikia waamuzi na makosa ya Azam. Ina maana Simba walikuwa hawachezi wanasubiri tu Azam akosee ili wafungee!!!

Sasa subiri jumapili utajua mpira unachezwa au Simba anasubiri makosa.

Halafu wachezaji waliotoka Vyura FC ...Benno, Gadiel, naAjibu hawatacheza ili msipate kisingizo kuwa mmeipatia Simba wachezaji
 
Hiyo itakua Ulaya ya Sumbawanga. Tunaangalia wachambukizi wa epl kila siku wanachambua makosa ya warefa wazi wazi.

Back
Top Bottom