Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Diamond anajua hivyo alikueleza?Uongo
Kila alie ingia pale Jangwani ukimuuliza wale watu hawakufika hiyo idadi uliyosema
Hata Diamond anajua hivo
Kumbe aliingiza mipesa yote hiyoo..vipi mbona huddah akashindwa kumlipa akashindwa kutokeaNajua wengi mlikuwa Mkisubiri hili jwa hamu kujua tadhimini nzima ya show mbili za Diamond na Team nzima ya Wasafi zilizo Fanyika Iringa na Dar! Sasa leo nimekuleteeni tathimini ya show zote mbili alizo Fanya Diamond!
Kabla sijatoa tathimini nzima naomba ifahamike hizi show zote mbili za Diamond zilikuwa na Mdhamini mkubwa ambaye ni VODACOM huyu amedhamini show zote mbili Dar na Iringa hadi kupelekea show Hiyo kuitwa VODACOM WASAFI BEACH FESTIVAL! Kama unajua kadhi ya mdhamini basi ujue hicho ndicho walicho Fanya Vodacom moja ya Kazi yao kubwa ni KUANDAA NA KUTEKELEZA MATAYATISHO YOTE YA SHOW ZOTE MBILI.....kuanzia stage na kuwalipa wote walio husika kwa namna moja au nyengine ikiwa ni pamoja na malipo ya wasanii wote walio toka nje ya Tanzania chini ya SALLAM,NA BABU Tale,Malipo ya matangazo yote ikiwa ni pamoja na kuwalipa Clouds Fm na Ebony Fm walio husika katika kutangaza hii show Dar na Iringa!,Kusafirisha na kulipia sehemu ambazo show itafika na wahusika kama vile kulipia Jangwani na Samora! .... Kwa kuwa Diamond ndie alie na Mkataba na Vodacom huenda pia vodacom ilihusika kuwalipa Harmonize,Rich Mavoko,Rayvanny na Queen Darling (JAPO KWA HILI SINA UHAKIKA SANAA ILA MSININUKUU VIBAYA)
Kifupi katika tathimini ninayo ileta Pesa Iliyo patikana ni itaingia moja kwa moja Katika Lebal ya WCB na Itafuata mkataba unavo sema kwa ma meneja!
Tukianzia na Dar Diamond aliingiza Mashabiki zaidi ya 3000 ikiwa sehemu waliyo iindaa ilikuwa na uwezo wa kuchukua watu 1500 hivyo waliingia Mara mbili ya Mategemeo Yao! Na kulikuwa na Tiketi za aina mbili kawaida na VIP.......Tukianza na Kawaida ambayo kiingilio kilikuwa 30,000 waliuza tiketi zaidi ya 2,800
Sasa chukua 2,800+×30,000= Millioni 84+
Kwa VIP waliuza Tiketi 200+ ambapo kila tiketi iliuzwa kwa shilingi 100,000
Sasa chukua 200+x100,000=Millioni 20+
Kwa Dar Jumla ni sh.Millioni 104+
Baada ya Hapo ni Alienda kufanya Show Iringa! Iringa alifanikiwa kuingiza watu 9,000+ kwa kiingilio cha sh 10,000
Sasa chukua 9,000+×10,000=Millioni 90+
Sasa chukua Millioni 104+ + Millioni 90+ =Millioni 194+
Hiyo hela ni kaingiza kwa Siku mbili Tuu!
Kifupi hiyo ndiyo tathimini ya haraka haraka sasa kaaa wewe na Nafsi yako jiulize Ni msanii gani mwingine Tanzania hii anaweza kufanya hivyo? Ifike muda anae Jua apewe heshima yake!
Wasanii wengine waangalie Mikataba ya kuingia..watu walimlaumu Diamond kwa kutokushiriki Fiesta kwa kuwa na Mkataba na Vodacom sasa nafikiri sasa mnaelewa maana ya mkataba alio ingia nao na manufaa anayo yapata! Imagine bila vodacom Diamond hizo millioni 104+ angezigawa vipi?
Sasa kupitia Vodacom wanataka kuzindua Wasafi Festival Ambayo watazunguka mikoa 10 Tanzania wakiaanza na Dar tarehe 14 Feb! Wakiwa na Vodacom means hiyo itakuwa ni zaidi ya Fiesta!
Hiyo Tathimini
DANYA nawasilisha!
Mkuu ndiye wewe ULIYE JIPATIA UMAARUFU kule Mbeya dayKumbe aliingiza mipesa yote hiyoo..vipi mbona huddah akashindwa kumlipa akashindwa kutokea
Voda chao n wateja wanaoingia kwenye showHivi kwenye hyo m 104 voda yao inakuwa ngapi? Au wanafaidika vipi na kuandaa show kwa ujumla?
Tumia akili tuu ya ziada mzizi wa show hizi mbili ni Vodacom wasafi beach part festival.....
MTU ALIE ELIMIKA hakai kuangalia makosa kama hayo
Huwezi ku argue wewe kaa Pembeni!Acha ukuda hakuna mzizi wala matawi. Nioneshe sehemu hata moja ambayo Diamond kaiita show ya Samora kuwa ni beach party. Ama umeamua kujitungia tu baada ya kuvimbiwa huko unakujs kupotosha
Huwezi ku argue wewe kaa Pembeni!
Tendea Haki Avarta Yako.sukari ya warembo huyo!! isije ikawa danya unawaza kutoka na diamond siku moja, kumpita zari kazi unayo
Kilichofanya huddah asije ni figisu za mama tee and nothing else.Kumbe aliingiza mipesa yote hiyoo..vipi mbona huddah akashindwa kumlipa akashindwa kutokea
Tendea Haki Avarta Yako.
Malcolm X ni mtu mkubwa sana, haipendezi kuwakilishwa kwa kauli zinazokutoka wewe.
kwa hiyo riwaya yako ndefuInauma ehhe...Diamond anasisitiza sana kuwa yeye ni sukari ya warembo, kwa maana kila mshabiki wa diamnd ni mrembo, hata wewe danya uliyekuja kwa jina la Pistmshai...ambaye ni mwanachama mzoefu ukajiunga tena dec mwaka huu, ona aibu
jiwe limerushwa kwa Danya wewe linakupataje?
watu wanaweka picha mpaka za Mungu na Yesu na Muhammad kwenye nyumba zao, mioyo yao na kila mahali na bado wanafanya mambo machafu tu
Nisiweze mimi kutokutoa kauli za kukufurahisha kwa sababu ya avatar ya malcom x? who is he by the way? ndiye aliyesema ukubali kuwa mshabiki wa diamond wakati yeye mond anasema ni sukari ya warembo? umejitukana au umejidhalilisha!!
ungetakiwa ku protest na kumwambia Diamond afute huo usemi, sasa aidha kwa sababu wewe ni mrembo kweli huwezi, au kwa sababu haujitambui unashindwa kuamua, au si riziki unashabikia tu
Be a man stay strong! mtu anaongea kauli za kudhalilisha unashabikia tu, akikuvua nguo je?? mwangalie
una lingine sema tu