View attachment 3099128
Rais Samia ktk Hafla Moshi
View attachment 3099159
Hoja ya Deusdedit Soka kuhusi intelijensia hafifu ya Jeshi la Polisi
1. Utangulizi
Akiwa katika Chuo cha Polisi Tanzania kilichooko mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, mnamo tarehe 17 Septemba 2024, Samia Suluhu Hassan, alivaa kofia zake zote kama Rais, Amiri Jeshi Mkuu, na Mkuu wa Nchi katika Jamhuri ya Muungano wa Kidemokrasia ya Tanzania.
Akiwa amevaa kofia hizo metoa hotuba ya dakika 57 ya kufunga Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa mwaka 2024 uliofanyika sambamba na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania.
Katika andiko hili nafanya tathmini ya uzuri, ubaya, na utata kabla ya kujadili hotuba hiyo, kuhitimisha na kutaja mapendekezo mahsusi
.
2. Matamko mazuri yenye sura ya kujenga
- Jeshi letu la polisi linapaswa Kwenda na wakati.
- Jeshi la polisi lilete bajeti kwa ajili ya kujiimarisha tekinolojia ya kufanya “saveilansi” kwa kutumia mbinu za kisasa na nitatekeleza mahitaji yao mara moja.
- Jeshi la polisi liboreshe mbinu zake za kuzuia vifo vinavyotokana na ajali za barabarani zinazoweza kuzuilika.
- Kwa mujibu wa majukumu yake ya kisheria Jeshi la polisi halipaswi kuwafumbia macho wale wote wenye nia ovu ya kuleta vurugu na uvunjifu wa amani.
- Jeshi la polisi lijitazame na kujisahihisha ili kurudisha Imani yake mbele ya jamii ili kuzuia aibu iliyotokea kule Mwanza jana ambapo ni wazi kuwa umma hauna imani tena na jeshi hili.
- Bado nina nia ya kuendeleza utekelezaji wa falsafa ya 4R, yaani, “Reforms, Resilience, Reconciliation, and Rebuilding.”
- Damu ya kila mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu maana uhai wa kila binadamu hauna bei.
- Hatutaruhusu kamwe mataifa ya nje kuingilia uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu ya ndani.
- Kwa kuwa uchaguzi ujao utapita lakini Tanzania itabaki, nalitaka jeshi la polisi linakuwa macho kabla, wakati na baada ya uchaguzi dhidi ya mtu yeyote mwenye nia ya kuhatarisha amani kwa kisingizio cha uchaguzi.
- Sikubaliani na matukio ya mauaji yanayohusisha wazazi, viongozi wa dini, wapenzi na waganga wa jadi.
- Jeshi la polisi liandae mpango kazi wenye kuonyesha vigezo vya kupima ufanisi ili tuweze kupima kasi ya utendaji wa kazi zenu.
View attachment 3099127
3. Matamko mabaya yenye sura ta vitisho
- Tarehe 11 Septemba 2024 Chadema walifanya mkutano huko Arusha, ambapo ajenda kuu ilikuwa ni jinsi ya kutumia maandamano kama mbinu ya kuvuruga amani na utulivu nchini.
- Wanataka kumwondoa Rais madarakani kwa njia ya maandamano lakini Rais hawezi kuondolewa kwa njia hiyo.
- Wamesahau misukosuko waliyopita hapo nyuma mpaka wakakimbia nchi nami kuwarejesha kwa kutumia falsafa ya 4R zangu wanayoikejeli
View attachment 3099129
4. Matamko tata yenye sura ya vijembe na mkanganyiko
- Ukimya wangu sio ujinga maana unanipa fursa ya kutafakari.
- Kauli za wakosoaji wangu wengi ni uropokaji bila werevu maana wao ni kama debe shinda lisiloacha kuvuma.
- Sio sawa kwa kifo kimoja tu cha Ally Mohamed Kibao wa Chadema kusababisha mtikisiko wa mwili na akili kiasi cha kuibua mihemuko ya kuhatarisha amani na utulivu wakati ni kifo kama vifo vya watu wengine waliouwawa siku za nyuma na wanaoendelea kuuawa kila siku kwa sababu mbalimbali, na katika matukio haya mengine hakukuwepo na mihemuko ya aina hiyo.
- Balozi za kigeni zilizokemea na kutaka uchunguzi wa kifo cha Mohamed KIbao ufanyike zilifanya hivyo bila baraka za Marais wa nchi wanazoziwakilisha na kinyume cha mwongozo wa kidiplomasia wa Viena.
View attachment 3099132
5
. Mjadala wa kutathmini kauli za Rais Ssmia
Tathmini yangu itajikita katika moja kuu: endapo Rais Samia anajua na kuelewa tofauti kati ya uhalifu na uadilifu au hapana?
Rais Samia amesema "kifo ni kifo" kwa maana kuwa kifo cha Ally Mohammed Kibao hakina tofauti na vifo vinavyotakana na sababu baki kama vile ajali za barabarani. Maswali sasa yanazuko:
Rais Samia h+anajua tofauti kati ya kifo kinachosababisha kwa makusudi na kifo kinachotokea kwa bahati mbaya?
Rais Samia anajua tofauti kati ya uovu wa kimaadili na uovu wa kifizikia, yaani moral evil versus physical evil?
Rais Samia anajua tofauti kati ya tendo la jinai lenye kiima cha dhamira na kiarifa cha utekelezaji, yaani mens rea versus mens reus?
Rais Samia anajua kuwa sayansi inayochunguza anatomia na fiziolojia ya matendo ya kihalifu (criminological praxiology) inasema kuwa kila kitendo kinachofanyika kwa makusudi ni kama mnyororo wenyw sehemu tatu, yaani LENGO, MBINU NA MAZINGIRA, na kwamba uadilifu wa kitendo hicho unapimwa kwa kuangalia pingili zote tatu kwa mpigo ili kujiridhisha kuwa hakuna pingili yoyote yenye doa la uovu?
Siku Rais Samia alipokuwa kiapo cha Urais kwa mara ya kwanza Rais alitwambia kuwa tumwamini kama Rais makini kwa kuwa yeye amelelewa katika familia yenye maadili yanayowezesha kuwa mkuu wa nchi bila kujali jinsia, dini wala hali yake baki. Katika mazingira ya hotuba ya sasa bado anataka tuamini maneno yake yale?
Na swali kubwa zIdi: wasaidizi wa Rais waliosaidia kuandaa na kuandika hotuba ya Rais wanao weledi kiasi gani hadi wampotoshe Rais kwa kiwango hiki?
Lakini pia, yeye Rais akipotishwa kwa nini akubali kulishwa matango pori bila kuyachukua kabisa?
Kuna jawabu moja tu kwa maswali haya: Kuna ombwe la kimaadili na kiweledi katika Ikulu ya Tanzania.
6. Hitimisho kuhusu aliyoyasema na aliyoyasahau
- Kauli ya Rais kuhusu “waropokaji” inaweza kuchochea ukamataji holela kama ule uliofanyika dhidi ya Deusdedith Soka kwa sababu tu ya kauli zake za kuvikosoa vyombo vya dola (tazama video hapo juu).
- Rais hajasema lolote kuhusu hadidu za rejea za Kamati ya Waziri Mkuu aliyosema ameiunda kwa ajili ya kuchungiza mauaji holela, na hivyo kuleta shaka katika uhalisia wa kazi ya kamati hiyo.
- Rais anasema kuwa kuna watu walifanya kikao kilichopanga kufanya uhalifu lakini hajaelekeza vyombo vya dola kuchukua hatua zozote dhidi yao, jambo linaloleta mashaka katika kile anachokisema.
- Rais ametoa kauli zenye kubatilishana katika suala la kukuza na kuhami uhai wa raia wasio na hatia, maana hakutofautisha vifo kwa kuzingatia sababu zake.
- Rais hakusema lolote kuhusu marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa yam waka 2023 inayoweza kuchochea machafuko nchini.
View attachment 3099134
7. Mapendekezo
- Rais aweke bayana hadidu za rejea kwa ajili ya Tume ya Waziri Mkuu.
- Rais atoe tamko la kuvitaka vyombo vya dola kuacha kuwakamata wakosoaji wa serikali kwa njia ya hoja. Kazi mojawapo ya rais ni kulinda uhuru wa raia katika suala la kufikiri na kueleza fikra zao bila hofu ya kutekwa, kuteswa na kuwekwa kuzuizini.
- Rais atoe agizo la kuachiwa kina Soka kwa sababu kosa lao ni kuikosoa serikali kwa njia ya hoja, na jambo hili sio kosa la jinai, sio uhaini na sio ugaidi.
- Rais aagize watu wote waliokaa kikao cha kuandaa vurugu wanafikishwa mbele ya sheria badala ya kuwa mlalamikaji na afisa propaganda. Kanuni ya kutofautisha kati ya taasisi na magenge ya wahuni ndani ya taasisi itumike hapa pia kama vilivyotumika kwa upande wa serikali.
- Rais amwagize mwanasheria mkuu wa serikali kusababisha marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa ya mwaka 2023 kwa kuondoa dosari zilizo katika vifungu vya 3, 5(2) na 19(1). Vifungu hivi vinaweza kusababisha machafuko nchini kupitia mikono ya maafisa usalama watakaoamua kuvitumia kufanya kazi za kipolisi.
Raia Mwema.