Tathmini hotuba ya Rais Samia miaka 60 ya Jeshi la Polisi: Uzuri, ubaya, utata na mapendekezo mahsusi

Madhara ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais ambaye hajawahi kupata mafunzo ya kijeshi, kama vile JKT au mafunzo ya mgambo, yanaweza kuwa makubwa na ya kutisha.

Kwanza, kiongozi ambaye hana ujuzi wa kijeshi anaweza kukosa maarifa muhimu yanayohitajika katika kupanga na kusimamia operesheni za kijeshi. Hii inaweza kupelekea maamuzi yasiyo sahihi katika nyakati za dharura, ambapo ufanisi wa maamuzi ni wa muhimu.

Pili, kuongoza wanajeshi bila mafunzo kunaweza kuathiri uwezo wa kiongozi wa kuhamasisha na kuimarisha morali ya askari. Wanajeshi wanahitaji kuwa na imani katika uwezo wa kiongozi wao, na ukosefu wa mafunzo unaweza kuleta shaka na ukosefu wa ushirikiano. Hali hii inaweza kusababisha migawanyiko ndani ya vikosi na kushindwa kwa operesheni muhimu.

Tatu, kiongozi ambaye hajawahi kupata mafunzo ya kijeshi anaweza kuwa na shida katika kutathmini hali ya kiusalama. Uelewa mdogo wa mazingira ya kivita na changamoto zinazoweza kutokea unaweza kupelekea mipango duni ya usalama, na hivyo hatari za kimataifa na za ndani zinaweza kushindwa kudhibitiwa.

Pia, athari za kisiasa si za kupuuzia. Umma unaweza kuwa na wasiwasi kuhusu uwezo wa kiongozi asiye na uzoefu wa kijeshi, na hii inaweza kuathiri uhalali wake. Upinzani kutoka kwa vyama vya siasa na jamii unaweza kuongezeka, huku wakihisi kuwa kuna hatari kwa usalama wa taifa.

Hatimaye, kukosekana kwa maarifa ya kijeshi kunaweza kuathiri mawasiliano kati ya serikali na vikosi vya usalama. Kiongozi ambaye hana ujuzi wa kijeshi anaweza kushindwa kuweka mikakati sahihi ya usalama na kushindwa kuendesha operesheni za pamoja kwa ufanisi. Kwa hivyo, ni muhimu kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais kuwa na uelewa mzuri wa masuala ya kijeshi ili kuhakikisha usalama na utulivu wa taifa.
 
Samia anataka kutuaminisha kuwa wale wakiomteka ally wakajitambulisha kuwa ni polisi walikua polisi kweli! Na kama walikua polisi kwahiyo wanashindana na wahalifu kuteka na kuua??
 
Avatar yako inaashiria kuwa wewe ni mwanamke (yaani: 'Mama' Amon ). Mwanamke mwenye Maono makubwa namna hii kwa nini 'usijitokeze hadharani' ili sisi wananchi tukukabidhi mikoba ya nchi ili kuokoa jahazi hizi linalizidi kwenda mrama na ambalo linataka kuzamishwa na Mwanamke mwenzako???
 
Ichafuke mara ngapi wakati watu wanatekwa na wanauawa hovyo na wauaji hawajulikani na hawajakamatwa?
 
Nataka nikitulia nishauri jeshi letu la Polisi ktk swala la mifumo mbalimbali.. kuna idea ninayo nitaileta hapa JF.
 
Ukiwa Rais lazima uwe veri tafu...Samia 2025💪
 
Nadhani Rais kapotoshwa.
Jana ametoa hotuba mbovu kupitiliza.
Naamini utekaji na mauaji yataongezeka kwa wale wakosoaji ambao Rais amesema ni waropokaji.
Tiss wamemuacha aendelee kulishwa matango pori na kina Makonda. Maana inaonekana wao ndo anawaona wa maana

Nafikiri Rais awe mwangalifu sana katika kuchagua maneno au lugha ya kuongea mbele za hadhara za Watu, asiwe anaamini kila kitu anachoambiwa na wale Watu wanaomzunguka. Sometimes anadanganywa au amekuwa akiambiwa Habari ambazo zimetiwa chumvi Sana. Awe anachuja maneno ya kuongea hadharani.
 
Albadir imeshaanza kuchanganya
 
KWA NCHI KAMA TANZANIA .. NI NCHI CHANGA SANA , HATUKAPASWA KUWA NA KIONGOZI MKUU WA NCHI. SISI KAMA NCHI TULIFANYA KOSA LA KIMFUMO. TULIIGA MAMBO YA WAZUNGU KUWA HAKI SAWA. TANZANIA NI NCHI CHANGA SANA,
1. KUANZIA MFUMO WA DEMOKRASIA, 2. 2.MFUMO WA KIUTAWALA, MFUMO WA 3.SIMAMIZI RASILIMALI NCHI.
4. MFUMO WA HAKI ZA KIBINADAM.
5. MFUMO WA SHERIA
6. MFUMO WA USALAMA.
KWA NCHI KAMA TANZANIA NA WINGI WA RASILIMALI HATUKAPASWA KURUHUSU MWANAMKE KUTAWALA.
Kutokana na Hali hii mambo ya aibu na ufujaji wa mali za taifa zimefanyika. Mfano Kwa kipindi kifupi deni la taifa limepanda,
Rushwa imekuwa, uwajibikaji umeshtuka,
Mikataba ya hovyo mingi imeingiwa mfano ni mktaba wa BANNDARI,
. MUUNDO MBINU IMEDUMAA.. KWA UFUPI hamna project mpya ambayo imekuja,
Uhuru wa mtanzania kuishi nchini na raia pia hawana amani kabisa katika nchi... Huyu mpaka kapuku anajikuta Hana aman kuishi nchini.. Masai ni mfano...
Rais kama Samia alitakiwa atawale kwenye ka nchi kama komoro au lethoto au ESWATINI...
WATANZANIA TUTAJUTA, NA ATAMWAGA DAMU MPAKA AKILI ITUKAE SAWA... TUSHAFIWA NA BABA , SISI NI YATIMA.. WAHUNI WATATUBAKA HUKU MAMA ANACHEKA.... MAMA ANALIWA NA MTOTO ANALIWA KIJANA WA KIUME NAO WANAVULIWA SURUALI...

HAHAHAHAHAJAHAJJAJA ... TUMERUKA MKOJO TUPO JUU YA KINYESI
 
Wewe Mama Amon ni mnafiki uliyekubuhu. Kwanini hukukemea CHADEMA na kauli yao ya kihaini ya Samia must go?
Kasema hivi......

Ni hivi: Kuna njia tatu za kuitafsiri.
Yaani, kauli hiyo inaweza kusomeka hivi:

  • "Samia must go by force"
  • "Samia must go willingly by resigning"
  • "Samia must go democratically through a ballot box"
 
Wewe Mama Amon ni mnafiki uliyekubuhu. Kwanini hukukemea CHADEMA na kauli yao ya kihaini ya Samia must go?
Wewe Matacore kweli,
Hivi shule ulienda somea ujinga CHADEMA walisema
Samia Must go!

1: By force and revolution?
3:Killing her?
4:Ballot Box?

Kati ya hapo wewe kiazi Umeelewa nini au ndio wazazi walipeleka ng'ombe shuleni huwezi changanua mambo,
Wewe hata ukiibiwa pusi wako nauhakika wezi watashinda kesi maana unaendeshwa na hisia kuliko uhalisia!
😁😁
 
Kasema hivi......

Ni hivi: Kuna njia tatu za kuitafsiri.
Yaani, kauli hiyo inaweza kusomeka hivi:

  • "Samia must go by force"
  • "Samia must go willingly by resigning"
  • "Samia must go democratically through a ballot box"
Najua kimoyomoyo mnakubali CHADEMA wamekosea kwenye hiyo kauli yao ndo maana utetezi wenu ni dhaifu mno. Haiingii akilini watu mna maandamano halafu mnatanguliza kauli yenye utata...
 
Wewe K hiyo tarehe 23 uwe mstari wa mbele kabisa kwenye maandamano ili uone kitakachokukuta..
 
Mimi ni mfuasi wa dhati wa mheshimiwa Rais Samia.
Nimesikiliza hotuba yake vizuri nikagundua kuna watu wa karibu na yeye wanampotosha.
Yeye mwenyewe aliwahi kusema "polisi hawawezi kujichunguza" ndipo akaagiza ziundwe kamati mbili za kuwachunguza.
Cha ajabu hotuba aliyoitoa hivi karibuni inapingana kabisa na uelewa wake.
Je, wanaompotosha wanalenga kupata faida gani?.
1.Hivi uhai wa mtu mnauchukuliaje yaani?.
2.Hivi hao maofisa wa Idara ya usalama wa Taifa wana weledi kweli au ndio wale waliopata D mbili?.
3.Hivi ni lini vyeo vikawa na thamani kuliko au sawa na UHAI wa binadamu wenzetu?.
NAWAKUMBUSHA TU:
VYAMA VYA SIASA VYOTE VITAPITA,ILA TANZANIA ITADUMU.
Tuilinde Tanzania, kuliko vitu vingine vyote.
 
1. Mama hana nia ya kuleta manadiliko kama watangulizi wenzake ana jali Uraisi wake, family yake na marafiki kuliko nchi kwa ujumla wake. Hivyo kwa maono yake katiba itampunguzia nguvu na maslahi ya family na ndugu
2. Mama ni mwoga sana hivyo hata pale kwenye hali ya uwazi kama kutekwa anaongopa maandamano hata kama hayana fujo. Akiona bango Mama must go anachanganyikiwa
3. Kwenye hii ya Rebuild anajenga nini hasa? Maana tunayo yaona hakuna analojenga zaidi ya chuki. Au anaongelea reli?!
4. Ubunifu hakuna lipwa watu wale wale wa Magu ndiyo watekaji na watu wanauliwa vilevile sasa ubunifu gani hasa Mama kaleta?

Yaani kwa yote Royal tour pekee ndiyo Mama kaweza kufanya na ni ubunifu lakini hizi 4R ni maneno matupu tu

Mama fuata sera zako mwenyewe 🤔
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…