Tathmini ya Chabruma Juu ya Upigaji Kura BMK, Chereko kwa CCM, Kilio kwa UKAWA,AKIDI KIULAINI


Wewe unawezaje kupinga utabiri huu kuwa hazitokuwa za ndio?
 
Last edited by a moderator:
Swali dogo tu...Hao UKAWA waliopiga ndio ni kina nani? isijekuwa mnadanganya kweupe...Hakuna UKAWA anaweza kupiga kura ...usijidanganye
 
Kujaza server tuu,,post hii iunganishwe na ya juzi. Cc: Mods
 
Kumbe Chaburuma ni mtu wa hovyo hovyo aisee !
 
LAANAA LA KUKU LEO LIMEMPATA MWEWE:angry:
 
"(9) Mjumbe yeyote aliye nje ya maeneo ya Bunge Maalum kwa ruhusa ya maandishi ya Mwenyekiti anaweza kupiga kura kwa njia ya nukushi, mtandao au njia nyingine yoyote itakayoelekezwa na Katibu baada ya kushauriana na Mwenyekiti na kura hizo zitajumuishwa pamoja na kura nyingine zilizopigwa chini ya Kanuni hizi.
(10) Kwa madhumuni ya fasili ya (9) ruhusa ya Mwenyekiti maana yake ni ruhusa ya maandishi kwa Mjumbe kutoka nje ya eneo la Bunge Maalum na ruhusa ya kupiga kura akiwa nje ya maeneo ya Bunge Maalum."

Hakuna mwanaukawa yeyote, narudia Hakuna mwanaukawa yeyote aliyeondoka BUNGENI kwa RUHUSA ya MAANDISHI. Kwahiyo HAKUNA mwanaukawa yeyote atakaeruhusiwa kupiga KURA akiwa nje ya BUNGE (au kwa mtandao !!!!!!).

Rudini mkachakachue tena hiyo IBARA ya KANUNI ZENU
 
Mkuu, bunge lina wajumbe wangapi?
 
We kahab.a nani kakwambia kura zote za siri ni ndiyo?halafu nani alikwambia safari ilikuwa ngumu?kuna mjumbe mmoja leo kasimama anasema hajawahi kuongea na apewe nafasi,alipopewa ilikuwa ni kumshambulia mwanasheria mkuu wa znz,Sitta akatulia tu wakati kumshambulia mjumbe bungeni moja kwa moja hairuhusiwi!huo ugumu wa safari unatoka wapi kama si ulegevu wa nyonga unaokusumbua!
Kulikuwa na haja gani kupiga kura ya wazi kwa siku karibu 3 wakati ingewezekana kumalizika sura zote kwa chini ya saa 2 kwa kura ya siri.kama si kupönda posho bila sababu ni nini?
Kwanini bmk liahirishwe saa 4 asubuhi,saa moja tokea lianze?kama si kuponda posho ni nin?
Wewe si mzalendo hata kidogo,umekaa kiushabiki kama wanamipasho wa taarabu,hata topic yako imekaa kiuchumia tumbo zaidi!
Wananchi ndio lungu la mwisho!
Nchi hii ina wapumb.vu wengi kweli,bora ungebadilishwa na ng'ombe ukaenda somalia!
 
Hongera chaburuma huo ndio ukweli na utabaki kuwa kweli.UKAWA imekula kwao
 
ndugu CHABRUMA umewafanya watu wote wakucheke sana ! Na wadharau thread zako zote za mwanzo , UMEJIAIBISHA SANA !
 
Kwa hiyo suala la katiba limekuwa ni CCM vs UKAWA & co...

Hivyo kwa mantiki hiyo kwa kuwa ni chereko kwa CCM unataka kutueleza hii ni rasimu ya katiba ya CCM inayopitishwa huko Dodoma...

Ni kweli Mkuu. UKAWA alijipambanua wenyewe kuwa walikuwa wanapambana na CCM


Chabruma...huajaelewa hoja ya Watu8. anaposema kwamba katiba hii imekuwa ya CCM, na wewe unakubali tu? hii ni katiba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. jitihada zote za UKAWA ni kui-lebo hii katiba kwa CCM. na wewe unakubali. hii inaonesha kwamba wengi katika CCM hilo hamjaliona bado. ni goli la kisigino la kujifunga hilo...
 
The game is over!
Kwa mujibu wa Samuel Sitta alivyotangaza jana, jumla ya Wabunge wote wa Bunge la Katiba = 629
Tanganyika = 419
Zanzibar = 210
2/3 ya 210 = 140
1/3 ya 210 = 70
Kwa hesabu ndogo tu hapo ni kwamba kuinyima Rasimu ya Vijisenti theluthi mbili (2/3) ya Zanzibar zilitakiwa zaidi ya kura 70 (kwa maana zikipatikana 71 itakuwa hapana 2/3 ya Zanzibar).
Sasa naomba tuhesabu pamoja. Miongoni mwa wajumbe 210 wa Bunge la Katiba wanaotoka upande wa Zanzibar:
Wawakilishi wa CUF = 33
Wabunge wa CUF ZNZ = 25
Wabunge wa Chadema ZNZ = 4
Wana UKAWA walotoka ZNZ miongoni mwa 67 = 5
Walopiga wazi HAPANA jana = 7
Wajumbe wawili (Mwanasheria Mkuu wa SMZ Othman Masoud na mjumbe Abdalla Abbas) hawakupiga kura = 2
Jumla = 76
Kuinyima two thirds ya Zanzibar ilitakiwa anything above 70 out of 210.
Hapa pana 76
Kwa lugha rahisi kufahamika ni kwamba Katiba inayopendekezwa haitopita maana haikupata theluthi mbili ya Zanzibar.
Hapa hatujui matokeo ya kura zilizopigwa SIRI. Pia wapo wale waliotajwa kwamba wameorodheshwa watapiga kura wakiwa nje ya Bunge Maalum. Lakini hata ukichukulia zote zitakuwa NDIO basi haziwezi kubadilisha uhalisi na ukweli wa kitakwimu uliopo hapo juu.
Kwa kifupi ni kwamba theluthi mbili ya kura za Wajumbe wote wa Bunge la Katiba wanaotoka Zanzibar HAIPO.
Sijui wale waliolazimisha kuendelea na Bunge Maalum la Katiba bila ya kupata maridhiano ya pamoja na wakapelekea kutumika mabilioni ya fedha za walipa kodi masikini wa Tanzania huku wakijua kwamba hawatopata theluthi mbili ya kura za Wabunge wote wa Zanzibar sasa watasemaje?
 
Km wanachakachua kura za wazi hizo za ndiyo zitasimamiwa na nani wasichakachue.
Haya ni maigizo haswaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…