Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wakuu wenzangu. Kuna huyu mpangaji ambae amekuwa tatizo kubwa kwa mwenye nyumba na wapangaji wenzake. Chanzo ni hivi... baada ya malalamiko mengi kuhusiana na nyumba aliyopanga Zuberi, ikabidi mwenye nyumba aitishe mkutano ili kujadili changamoto zinazoikabili nyumba yake. Katika mkutano huo wapangaji wote walihudhuria kasoro mmoja na familia yake ndo hawakufika kutokana na vigezo walivyompa mwenye nyumba kutokuvitimiza. Katika mkutano ule kila mpangaji aliongea matatizo na changamoto zake mbele ya mwenye nyumba na wageni mbali mbali walioalikwa kwenye mkutano huo. Cha kushangaza ilipofika zamu ya ndugu Zuberi (sio jina halisi) badala ya kuzungumzia matatizo na changamoto zake zinazomkabili kwenye ile nyumba, yeye akaanza kutiririka kuzungumzia matatizo na changamoto za yule mpangaji mwenzake ambae hakufika mkutanoni kwa sababu zake. Baada ya mkutano kuisha, yule mpangaji ambae hakufika mkutano pamoja na familia yake wakaanza kumshambulia ndugu Zuberi kwa kimbele mbele chake cha kukimbilia kuelezea matatizo ya mwenzake badala ya kueleza ya kwake, tena bila ruhusa ya muhusika mwenyewe. Ndugu Zuberi baada ya kuona mashambulizi yanazidi kutoka kila upande wa familia ya yule mpangaji mwenzake, akaona nitoke vipi kwenye hili janga nililo lichuma mwenyewe. Ndo ghafla amekuja na madai yasiokuwa na tija akidai kwamba aliekuwa mmiliki wa nyumba hiyo hayati Nondo aliwahi kumnyanyasa sana yeye na familia yake na kwamba ilifikia kipindi mpaka hayati yule alimtumia vijana wakaangamize na kulichoma shamba lake la mihogo. Sasa watu tunajiuliza wakati hayo yaliotokes yanatokea huyu ndugu Zuberi alikuwa wapi? Je aliwahi kutoa taarifa popote juu ya kile kilichotokea huku muhusika mwenyewe akiwa hai ili sheria iweze kutumika kumuwajibisha? Kama hakuwahi kutoa taarifa kipindi kile mwenye nyumba wa awali akiwa hai sasa hivi anatoa taarifa ili iweje? Kumuwajibisha marehemu kwa jambo ambalo hatuna uhakika nalo kama ni la kweli au la uongo? au ameamua kuripoti ili mwenye nyumba wa sasa amuonee huruma na kumnunulia shamba lingine? Au ameamua kufunika kombe mwanaharamu apite? Maana kuna mpambano mkali wa maneno kati yake na familia ya yule mpangaji mwenzake. Kwa kweli huyu mpangaji atakuwa ana tatizo sehemu. Nashauri waliopo karibu yake waangalie namna ya kumpeleka kwa wataalam wa seikolojia, huenda ndugu yako ameanza kuwa na mchwa kichwani kwake ambao kwa sasa wako busy kuitafuna akili yake. Asanteni wenye akili, kwa kunisoma.