Uchaguzi 2020 Tathmini ya Taarifa ya Habari ITV & TBC1

Uchaguzi 2020 Tathmini ya Taarifa ya Habari ITV & TBC1

Mwaka 2015 wanywa bia walikuwa walikuwa na hali bora zaidi. mwaka huu mnapitia kwanza kwenye mataputapu kisha mnaenda kusuuza na kabia kamoja hadi taarifa za habari zipite.
 
Mmekaa UVCCM mnakunywa bia baada ya kupewa pesa za Serikali mkiambiwa ni za chama mkaeneze uharo wa CCM wewe unaita watu. Watu gani hao wasio na akili wanamkubali Magufuli?
 
CCM Zanzibar inatia huruma .
Mgombea Urais Wanapewa
Wabunge wanapewa
Hata wawakilishi wanapewa kutoka Dodoma.

Tukumbuke ASP+TANU =CCM
Lakini Zanzibar hawezi kutoa M/Kiti wala SG

Kuna Makamu Wenyeviti 2

Akifa M/Kiti wao wa taifa anachukua nafasia Makamu wa Bara Ccm
Kwa ufupi Ccm Zanzibar Kama Tawi la Ccm Mtwara.

Wanzazibar hamkeni.
 
Sawa kada mwenzangu. CCM ndio nyumbani na ndio kula yangu ilipo. Kama ahadi namba nane ya TANU isemavyo, mwaka huu siwi mnafiki na sipepesi macho, naangalia sera. Hadi sasa ACT Wazalendo wamenivutia sana na ilani yao maana wameiandaa na ukiisoma unaifeel yaani, wamejitahidi hata kujaribu kutuma ujumbe kwa picha. Chama kipya lakini kina watu smart sana.

Lisu namkubali sana, ila CHADEMA mwaka huu coordination haiko vizuri, maandalizi ni hafifu sana. Sijui kwa nini.

Chama changu CCM kina resources kibao ila chacha my people my world....wao wanahubiri wanyonge ila hawajampa mnyonge kipaumbele cha kutosha
 
Huyo Msaliti Lissu anahangaika tu!
Mkombozi wa kweli wa Tanzania ni ELIMU kitu ambacho watawala hawataki kabisa kutupatia, wengi tunadhani DIV:1 zetu ktk NECTA exams ndio elimu bora.

Tumechelewa kujikomboa na tutachelewa sana kuelimishwa.

Mataifa yote yaliingia ktk ramani ya maendeleo walianza na mfumo wa elimu kwanza, rejea china rev ya 1979,Russia rev 1917, Cuba rev ya 1959 yote haya yalianza na social -cultural transformations.

Mfano, baada ya twenty years after Revolution Cuba iliweza kuzalisha madaktar wake wenyewe ambao waliisaidia cuba , Engineers , Teachers, etc.

Sisi tunamshangilia Lissu na magufuli tukidhani wao watafanya miujiza.

Tatizo la Tanzania siyo magufuli , wala Lissu hatakuwa tiba ya tatizo bali tatizo ni mifumo ambayo tiba yake ni kuifumua na kuifuma upya.

Kwa ufupi CCM imetuchosha wacha tubadilishe waje waongo wengine.
 
Uko sahihi sana mjumbe, elimu elimu elimu. Tunataka elimu hata ya ngazi ya cheti inayompa mtu ujasiri wa kujisimamia na kuleta matokeo chanya kwenye jamii
 
Malizia bia ukalale kabla ya wahuni wa kinondoni hawajaanza kufanya yao kwa walevi
Malizia kinywaji chako mapema kabla hujageuzwa asusa pindi utakapo poteza kumbukumbu zako kutokana ulevi wako. Kwa kutuambia hayo, ni lazima ukubali kuwa unaweka rehani heshima yako mbele ya jamii.
 
Uzuri umetujulisha kuwa hiyo ni tathmini ya mlevi, na bila shaka kwenye hiyo Meza unalewa na wanafisiemu wenzako
 
Leslie Mbena,
Mkuu umesahau Kitwanga(mawe3)alifukuzwa kazi kwa ulevi, angalia mkuu nawewe usje poteza ujira wako kwaulevi.....maana ata cc tusio naChama tumegundua izo niAkili za Mbope;kumbe viroba vlibakiziwa makada eeee
 
Ulishakunywa balimi ngapi kabla ya kupost. Lakini kwa kuchangia tu, nimetazama taarifa ya habari ITV sijapenda namna walivyomfanyia membe na tundu Lissu, yani kwa vipande walivyokua wanarusha katika mikutano yao wanaonyesha kimkusanyiko kidogo cha watu na si kuonyesha uwanja kwa upana wake, utakuta wanaonyesha watu wachache waliokaa pembeni kabisa ya uwanja lengo ni kutokuonyesha wingi wa wahuzuliaji.

kama mkutano wa membe ukiangalia utasema alikua anazungumza na familia yake.

Lakini linapokuja la upande wa pili wanatuonesha watu kama wamejaa sana adi wanakanyagana. "Tukitoa itikadi zetu za vyama kila mtu anaona Upinzani wanapitia wakati mgumu sana"
 
Back
Top Bottom