Sawa kada mwenzangu. CCM ndio nyumbani na ndio kula yangu ilipo. Kama ahadi namba nane ya TANU isemavyo, mwaka huu siwi mnafiki na sipepesi macho, naangalia sera. Hadi sasa ACT Wazalendo wamenivutia sana na ilani yao maana wameiandaa na ukiisoma unaifeel yaani, wamejitahidi hata kujaribu kutuma ujumbe kwa picha. Chama kipya lakini kina watu smart sana.
Lisu namkubali sana, ila CHADEMA mwaka huu coordination haiko vizuri, maandalizi ni hafifu sana. Sijui kwa nini.
Chama changu CCM kina resources kibao ila chacha my people my world....wao wanahubiri wanyonge ila hawajampa mnyonge kipaumbele cha kutosha