TAARIFA YA CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TATHMINI YA TAARIFA YA TUME YA JAJI CHANDE KUHUSU MATUKIO YA OKTOBA 29 MWAKA 2025, ILIYOTOLEWA TAREHE 23 APRIL 2026 PAMOJA NA KESI ZA JINAI ZINAZOMKABILI TUNDU ANTIPAS MUGHWAI LISSU.
11 Mei 2026, Dar es Salaam
1.0 Utangulizi
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ni taasisi ya kitaaluma iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Chama Cha Wanasheria Tanganyika, Sura ya 307 Kama ilivyorejewa Mwaka 2023, chama kimekuwepo kabla ya uhuru wa Tanganyika kuanzia mwaka 1954. TLS ni chama kinachowakutanisha mawakili wote waliosajiliwa na wanaofanya kazi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara. Kwa mujibu wa kifungu cha 4 Cha Sheria ya Chama cha sheria Tanganyika, TLS ilianzishwa kwa madhumuni ya kukuza na kulinda taaluma ya sheria, kuhakikisha maadili ya uwakili yanazingatiwa, kuimarisha utawala wa sheria nchini, kuulinda na kuutetea umma wa Watanzania kwenye mambo yote yanayohusu sheria pamoja na yote TLS inawajibu wa kuishauri Serikali, Mahakama na Bunge pamoja na kutetea haki za binadamu na upatikanaji wa haki kwa wananchi. TLS pia ina jukumu la kuimarisha utawala bora na kuhakikisha mfumo wa haki unafanya kazi kwa uwazi, ufanisi na haki kwa wote.
Ndugu waandishi wa habari
Mtakumbuka kwamba tarehe 14 Novemba 2025, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan aliunda Tume ya kuchunguza matukio ya ghasia na uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025. Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Tume hiyo iliongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu mhe. Mohamed Othman Chande ilipaswa kufanya kazi kwa muda wa siku tisini (90), yaani mpaka Februari 20, 2026. Hata hivyo, Tume iliongezewa siku 42 zaidi baada ya muda iliyokuwa imepewa kutamatika ikaongezwa tena siku 21 na tangazo la kuongezewa muda lilitolewa na Mwenyekiti wa Tume badala ya mamlaka ya uteuzi yenye uwezo wa kuongeza muda. Tarehe mpya ya kuwasilisha ripoti ikapangwa kuwa tarehe 23 Aprili 2026 na tarehe 28 April 2026 Tume ilikuja tena kufanya ufafanuzi kwa Umma.
Taarifa hii imeangalia mapungufu ya Taarifa ya Tume ya tarehe 23 April 2026 na ufafanuzi wa tume wa Tarehe 28 April 2026 ambao kisheria hauna nguvu za kisheria kwani tume
ilimaliza kazi zake kisheria baada ya kukabidhi ripoti yao. Tunawiwa kama washauri kuuujulisha umma kuhusu uhalali au vingivevyo wa kitendo cha tume kutoa ufafanuzi huo.
2.0 Hadidu za Rejea
Ndugu waandishi wa habari
Kwa mujibu wa taarifa ya Tume, zifuatazo zilikuwa hadidu za rejea na mawanda ya Tume:
Kuchunguza na kubaini chanzo halisi cha ghasia zilizotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 na siku chache zilizofuata,
ii. Kuchunguza lengo kuu lililokusudiwa na waliohusika katika kupanga na kutekeleza vitendo hivyo vya ghasia na uvunjifu wa amani,
Kuchunguza na kubaini madhara yaliyotokea kutokana na ghasia hizo, ikiwemo vifo, majeruhi, uharibifu wa mali na miundombinu pamoja na madhara ya kiuchumi na kijamii,
iv. Kuchunguza mazingira na hatua zilizochukuliwa katika kubaini na kukabiliana na ghasia zilizojitokeza,
V. Kupendekeza maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi ili kuongeza uwajibikaji wa viongozi na raia kwenye kulinda amani, utawala wa sheria, haki za binadamu, utawala bora na mfumo madhubuti wa majadiliano ya kisiasa, kijamii, kiuchumi hadi kufikia maridhiano ya kitaifa na kuhakikisha vurugu kama hizo hazitokei tena,
vi. Kuchunguza jambo lolote ambalo Tume itaona kuwa ni muhimu na linaendana na majukumu yake
3.0 Kuhusu chanzo cha Maandamano
Ndugu waandishi wa habari
Kwa muda mrefu wadau wa masuala ya demokrasia, uchaguzi, utawala wa sheria, utawala bora na haki za binadamu ikiwa ni pamoja na TLS tumeshauri ama kupitia maandiko ya kisomi, makongamano au mikutano na watendaji mbalimbali wa Serikali juu ya umuhimu na ulazima wa Serikali kutekeleza masuala ambayo Tume imeyaita kama vyanzo vikuu vya ghasia lakini isivyo bahati Serikali imekuwa ikipuuza maoni ya wadau kwa kutoyafanyia kazi inavyostahili.
Na hata baada ya kuyapuuza kwa kuzingatia wajibu wake chini ya kifungu cha 4 cha sheria ya Chama Cha Wanasheria Tanganyika pamoja na wadau wa utawala bora, haki za binadamu na utawala wa sheria wamefungua kesi kadhaa ili kupata nafuu kupitia mahakamani, lakini mahakama zimeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa kutotambua wajibu wake kama chombo cha kudhibiti na kuzuia matumizi mabaya ya madaraka ya mihimili mingine tatika matumizi mabaya ya madaraka na kuweka mkazo mkubwa katika masuala ya kiufundi.
Mtakumbuka hata kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika chama kilishauri ulazima wa kuifumua mifumo yetu ya kiuchaguzi ikiwemo uwezekano wa kupata Katiba mpya ambayo ingeweka misingi imara ya ukuu wa katiba, utawala wa sheria, mgawanyo wa madaraka na uhuru wa Mahakama ili kuliokoa Taifa na machafuko lakini Serikali haikuwa tayari ama kusikiliza, au kutekeleza maoni yetu, hata hivyo hatukukata tamaa tuliendelea kuishauri Serikali bila mafanikio.
Hata hivyo, kwa tathmini yetu, yote yaliyotokea, kwa sehemu kubwa yamechangiwa na Taasisi kama Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jeshi la Polisi, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Marekebisho ya sheria za uchaguzi yasiyozingatia maoni ya wadau na changamoto halisi zinazolalamikiwa na wadau wa uchaguzi pamoja na Mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake wa ulinganifu wa kimamlaka (checks and balance) na kuifanya Serikali kuwa na mamlaka zaidi ya mihimili mingine na hivyo kupuuzia na au kutokuchukua au kutokutekeleza maoni ya wadau kwani kama Tume ilivyotaarifu, madai hayo yamekuwepo kwa muda mrefu katika jamii yetu lakini yamekuwa yakipuuzwa.
Ndugu waandishi wa habari
Baada ya kupitia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume sisi kama Chama cha Wanasheria imetuwia vigumu kufanya uchambuzi wa kina wa ripoti kutokana na tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba ripoti ya uchunguzi haitatolewa kwa Umma Tuna sema wazi kuwa imekuwa vigumu kutoa tathmini ya ripoti ya Tume bila kuisoma taarifa kamili. Tuchukue fursa hii kueleza kuwa kitendo hicho ni kinyume na ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho. Tume iliundwa chini ya sheria husika kwa maslahi ya umma inakuwa haina mantiki kwa wanachi kutoiona na kutoijadili ripoti ya tume iliyoundwa kwa ajili yao. Kitendo cha kuwanyima raia maudhui ya ripoti hiyo ni ukikwaji wa Ibara za 18 na 21(2) za Katiba
Kwa sababu hizo Uchambuzi wetu umejikita kwenye hotuba iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume tarehe 23 April 2026 na 28 Aprili 2026. Katika uchambuzi wetu tumeona kuna mapungufu 30, ambayo yanatoa ukakasi kwa wananchi na ndio sababu ya wananchi kuendelea kulalamika na kufanya tusipige hatua katika kutatua changamoto zilizopo mbele yetu kama taifa na kuongeza mpasuko baina yetu.
4.0 Mapungufu
Ndugu waandishi wa habari
Mapungufu tuliyoyagundua yanayotiliwa shaka kutokana na taarifa ya Tume ni kama yafuatayo;
1. Kuna chanzo cha tatu kinatajwa kuwa ni masuala ya kijamii, ikiwa ni pamoja na madai ya utekaji na kupotea kwa watu, lakini maelezo ya kina yanaeleza kuwa watu kupotea ni tatizo. Lakini tatizo kubwa ni watu kutekwa, kuteswa na kuuawa wakiwa mikononi mwa dola, Mtu mzima hapotei labda anapotezwa na hilo ni chanzo kimoja wapo kikubwa.
2. Taarifa hiyo ya watu kupotea ni ile ambayo polisi walitoa kwa Tume, hakuna uchunguzi wowote ulifanywa na Tume kwenye chanzo hiki na hivyo kudogosha ukubwa wa chanzo, ndo maana sababu za watu kupotea zinasemwa kuwa mambo ya mapenzi, madeni na vitu vya namna hiyo, lakini Malalamiko kuhusu Kuchukuliwa na Kutekwa kwa Soka na wenzake, Mdude Mpaluka Nyagali, Humprey Polepole na wengine tunajua wamepotea kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa na ukosoaji katika sera mipango na masuala ya kiutendaji ya Serikali na sio hayo yanayosemwa na Tume ndio maana watu wanashindwa kuamini taarifa ya Tume. Na hii haijarejea hoja za kutekwa na kupotezwa kwa watu 94 kama zinazo oneshwa kwenye Orodha ya TLS iliyotolewa ambapo baadhi ya waliotekwa na kupotezwa walikuja kupatikana baadaye wakiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi.
3. Utendaji usioridhisha imetajwa kuwa ni chanzo cha ghasia hizo, lakini tunaambiwa kuwa ni kwa watendaji wa chini, ni kweli?, Kwa maoni yetu sio kweli kwamba Utendaji wa chini ni chanzo cha Mauwaji na uvunjaji wa haki za Binadamu Sheria na Katiba ya nchi iliyopelekea Mauwaji makubwa ya Raia na Waandamanaji na kwamba utendaji mbovu ni kuanzia kwa viongozi wajuu sio hawa wa chini. Hatukubaliana na kuona kisababishi ni watu wa ngazi za chini, hii taarifa haujazingatia ukweli kwamba Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi, Kuondolewa kwa ushindani wa kweli ikiwemo kuwekwa mahabusu kwa Kiongozi wa chama Kikuu cha Upinzani na Chama hicho kuzuia kushiriki Uchaguzi kwa maelezo ya kutosaini Kanuni za Maadili, Masuala ya Utekaji na Kupotezwa kwa watu hususana wakosoaji wa Serikali,Masuala ya malalamiko ya wananchi ikiwemo utwaaji holela wa Ardhi za wananchi na kuondolewa kwenye maeneo yao Kinyume cha sheria kwa kisingizio cha uhifadhi au uwekezaji na Matumizi ya nguvu kupita kiasi kwa jeshi la Polisi katika maswali ya kisiasa na Demokrasia ikiwemo kuzuia mfululizo wa haki mbalimbali za kujumuika na Kuandamana kwa Wananchi na Kuminywa kwa uhuru wa Kujieleza na kufungiwa kwa Makanisa, na malalamiko ya watu wengi kuendelea kushikiliwa mahabusu kwa muda mrefu kwenye kesi zinazo daiwa kuwa na Msingi ya kisiasa na zingine Ugaidi hakukuzingatiwa kabisa na Tume kama hali ambayo ilisababisha wananchi na jamii kuwa na hasira na Uchungu.
4. Taarifa hiyo inasema kuwa kichocheo kimojawapo ni kuwa kuna watu walipewa simu za mkononi ili waweze kurekodi matukio, lakini taarifa hiyo haisemi ni lini, ni wapi na ni nani aliwapa watu hawa hizo simu?, bila taarifa za kina hiyo inabaki kuwa tuhuma ambayo haijathibitishwa ni ngumu kwa umma kuamini.
5. Tumeambiwa kuna vichocheo kutokana na kauli mbalimbali lakini kauli hizo zimetolewa kwa ujumla na ubaguzi na kuacha kauli zilizochochea hasira zilizotoka wakati wa kampeni na viongozi wa dini, viongozi waliopo madarakani, na wanasiasa mbalimbali,
6. Pamoja na Tume kubainisha baadhi ya vichocheo vya vurugu hizo; hata hivyo, katika taarifa yake, Tume imeonekana kuwa na kigugumizi katika kuwataja waliohusika na kupendekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yao. Kwa mfano, Tume imekiri kuwepo kwa vitendo vya utekaji na kupotea kwa watu, na hata kutoa takwimu kuwa takribani watu 245 hawajulikani walipo hadi sasa.
7. Pamoja na uzito wa suala hili, Tume haijaweza kueleza kwa kina nani wanaohusika na vitendo hivyo, wala nani anayetoa amri ya utekelezaji wake.
8. Kwa tathmini yetu, taarifa hii haiwezi kuonekana kuwa kamili kwa mujibu wa hadidu za rejea zilizoiunda Tume, ambazo zilielekeza kuchunguza lengo kuu lililokusudiwa na wahusika katika kupanga na kutekeleza vitendo hivyo vya ghasia, pamoja na kubaini chanzo halisi cha ghasia hizo. Ni vigumu kufikia malengo haya bila kuwataja waliohusika na bila kupendekeza hatua mahususi za kuchukuliwa dhidi yao, ni ngumu ripoti hiyo kuaminika.
9. Taarifa ya Tume imeeleza kuwa baadhi ya waliohusika na vitendo vya ghasia walipata mafunzo maalum kwa muda wa takribani wiki mbili kabla ya uchaguzi.
Hata hivyo, pamoja na madai haya mazito, uchunguzi wa Tume umeshindwa kubainisha kwa kina mafunzo hayo yalitolewa na nani na yalifanyika katika eneo gani mahsusi, licha ya kutaja kuwepo kwa kituo cha mafunzo jijini Dar es Salaam ambacho kipo umbali mfupi kutoka kituo kimoja cha polisi. Hali hii inaacha maswali mengi bila majibu kuhusu uhalisia na uthibitisho wa madai hayo, hivyo ni ngumu kuaminika.
10. Aidha, Tume imeeleza kuwa baadhi ya waandamanaji walilipwa fedha na kudai kuwa ilipokea ushahidi wa kiapo kutoka kwa mmoja wa waandamanaji. Kwa mantiki ya kawaida, ushahidi wa kiapo unapaswa kubainisha wazi mhusika aliyetoa fedha hizo. Hata hivyo, katika hali isiyoeleweka, Tume haijaweka wazi ni nani aliyetoa fedha hizo, kwa watu wangapi?, wala malengo ya ufadhili huo, licha ya kudai kuwa na ushahidi huo wa kiapo hivyo ni ngumu kuaminika.
11. Pia kulikuwa na tuhuma za waandamanaji kubeba silaha lakini hakuna hata raia mmoja aliyeshitakiwa kwa kubeba au kukutwa na silaha kinyume na utaratibu hasa wakati wa mashauri mengi yaliyokuwa kwenye mahakama zetu maeneo mbalimbali nchini, hii inatoa mashaka juu ya ripoti hiyo. Kwa ujumla, hoja hizi zinaonesha kuwepo kwa mapungufu makubwa katika kutoa majibu ya kina na ya kweli kuhusu
madai mazito yahyowasilishwa, jambo linalotbua maswali juu ya ukamilifu na uwazi wa ripoti yenyewe,
Ndugu waandishi wa habari,
12. Eneo jingine ambalo Tume imeonyesha mashaka ni kuluen uaminifu wa talovima (data credibility). Tume imeelezea kuwepo kwa idadi inayolanana kati ya vitu vilivyotokana na risasi (197) na majeruhi waliopata majeraha ya risasi (197). Hata hivyo, kwa hali ya kawaida ni nadra sana katika mazingira halisi ya vurugu, kulanana kwa takwimu hizi lomaweza kuashiria tatizo katika ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu.
13. Jambo lingine la kushangaza katika taarifa ya Tume ni kukiri kwamba kulikuwa na miili takribani 39 iliyotambuliwa na ndugu katika vituo mbalimbali vya afya, lakini baadaye ndugu hao walishindwa kuipata, na hadi leo hawajafanikiwa kuichukua Hi ni suala zito linalogusa haki za msingi za kibinadamu na utu hasa kwa familia husika.
14. Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba Tume haijaeleza ni nani aliyewazuia ndugu kuchukua miili hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa vituo vya afya vilivyohusika ni vya umma. Hali hii inaibua maswali muhimu ni kwa mamlaka gani miili hiyo ilizuiwa, kwa malengo gani, na ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya waliohusika? Badala ya kutoa majibu ya kina, Tume inaonekana kuishia kueleza tatizo hili kana kwamba ni mlalamikaji, bila kuchukua msimamo wa wazi unaoendana na wajibu wake wa kubaini ukweli na kupendekeza hatua stahili.
Ndugu waandishi wa habari,
15. Enco jingine muhimu ambalo umma wa Watanzania ulitarajia kusikia msimamo wa Tume ni kuhusu uhalali wa tangazo la IGP Wambura lililowataka wakazi wa Dar es Salaam kutokutoka nje ya makazi yao, na ambalo baadaye lilionekana kutumika katika maeneo mbalimbali ya nchi. Kutokana na uzito wa suala hili katika muktadha wa sheria na Katiba, umma ulitarajia Tume kutoa ufafanuzi wa wazi kuhusu uhalali wake na athari zake. Hata hivyo, katika hali isiyoeleweka, Tume haikugusia kabisa jambo hili, jambo linaloacha pengo kubwa katika hoja za kisheria na kiutawala.
16. Vilevile, kulikuwa na matarajio makubwa kutoka kwa umma kuhusu madai kwamba kulikuwa na waandamanaji waliokodiwa kutoka nchi jirani kushiriki katika vurugu hizo. Maswali muhimu yalihusu waliingiaje nchini, ni nani aliyewafadhili, na kwa malengo gani na mamlaka za mipakani zilikuwa wapi. Hata hivyo, licha ya uzito wa tuhuma hizi katika mjadala wa kitaifa, Tume haikutoa maelezo yoyote wala kuchukua msimamo juu ya madai hayo, hali inayozidi kuongeza sintofahamu na kuacha maswali mengi ya msingi bila majibu.
Ndugu wandishi wa habari,
Wine waliingitmes kupewa tamita kuwa ni nani alitoa amri ya kuzimwa kwa
sme meshandwa kueleza kazimwa kwa mtandao kwa kiasi gani Awa watu na Mahan za kun humi kwa sababu walishindwa kupeana radhar walishindwa kuita usafiri mtandaoni ili waweze kupata usafiri Anda kwenda kupata matibabu, walishindwa kostanya miamala kwa kutumia mands na mambo mengine. Nume imekuwa na kigugumizi kwenye eneo hili.
Ndugu waandishi wa habart,
18 tambo ingine bumaletaka kuliangarsa ni kuhusu hatua ya Tume kuepuka kuwataja
wahusika wa mauan na majeruhi wa Oktoba 29, 2025 na kutopendekeza hatua mohsuse na kuwawanbisha badala yake, Tume imependekeza kuundwa kwa chombo kingine cha kinai kitakachopewa jukumu la kushughulikia masuala hayo, ikiwemo Kuwabalm na kuwachukulia hatua watuhumiwa wa mauaji hayo.
14 Nahi hainaibua swali la msingi kuhusu upeo na madhumuni ya Tume yenyewe, ikiwa Tome ya Mheshimiwa Jaji Chande haikuwa na mamlaka ya kushughulikia masuala ya kifinal jo dikuwa inachunguza nini hasa? Na ikiwa ilikuwa inapokea ushahidi wa mashahidi, hata kwa njia ya viapo, ushahidi huo ulikusudiwa kutumika wapi na kwa lenge gani? Nukosekana kwa majibu ya wazi katika masuala haya kunazua shaka juu ya ulanisi na mwelekeo wa kazi ya Tume, pamoja na uwezo wake wa kufikia mataralio ya umma katika kubaini ukweli na kuhakikisha uwajibikaji.
20. lambo jingine ni taarifa juu ya watoto, ni nani alihusika kuua watoto hao kwa malengo gani? je Watoto nao walilipwa au kupewa mafunzo?, hawakuwa na adhabu nyingine zaidi ya kifol.
Ndugu Waandishi wa habari,
21 jambo la mwisho ambalo wananchi na sisi kama chama cha sheria Tanganyika, tulitarajia kutoka kwa Tume na tumeshindwa kupata ni ukweli juu ya mambo mbalimbali, tulikuwa tunajua watu wameuwawa lakini ni nani kaua kwa amri gani ndo tulitaka kujua, tulikuwa tunajua watu wamejeruhiwa lakini ni nani kawajeruhi kwa amri ya nani?, Ni nani alizima mtandao ili iweje?, Taarifa hii ya Tume haionyeshi wkwell, uwazi wala haiwezi kusaidia uwajibikaji wa aina yoyote na wala haitupeleki kwenye maridhiano kama ambavyo baadhi ya watu wanajaribu kushawishi.
22. Tume kuna mambo mengine imehitimisha, wakati mambo mengine imekuwa na kigugumizi na kudai uchunguzi ufanyike, mfano kuhusu makaburi ya halaiki kwa Kondo imeenda na kufunga mjadala, huku waliopigwa risasi majumbani Tume inadai uchunguzi ufanyike. Hii taarifa inatia mashaka makubwa kuhusu nia ya Tume
23. Kuhusu makaburi ya halaiki, Tume imefanya uchunguzi makaburi ya Kondo tu, na imeshindwa kufanya uchunguzi maeneo mengine, imefanya kwa Kondo na kusafisha watuhumiwa bila uchunguzi wowote wa kitaalamu, Tume inadai ilimuuliza mtunza makaburi ambaye ni mwajiliwa wa serikali ambaye wakati wa ghasia na yeye hakuwepo maaana kulikuwa na zuio la kutoka nje, hakuna utafiti wowote wa kitaalamu umetolewa unaoweza kueleweka.
24. Tume imetoa taarifa kuwa majeruhi wote hawakuteswa lakini Tume haijasema kama iliwahi kuhoji watuhumiwa waliopelekwa mahakamani, sisi tulitoa msaada wa kisheria kwa watuhumiwa wote nchi nzima na wengi wao waliteswa vituo vya polisi ili wataje waliowatuma, walinyimwa chakula na huduma nyingine wakiwa vituo vya polisi, walikaa zaidi ya masaa 24 bila kupewa dhamana au kufikishwa mahakamani, na hawakupewa haki ya uwakilishi wa mawakili wakiwa vituoni maana kulikuwa na mazuio na wengi wao wamekaa zaidi ya wiki kwenye vituo vya polisi na hicho ni kinyume cha sheria na ni utesaji kwa raia.
25. Tume imedogosha dhana ya maandamano kwa kusimamia maelezo ya polisi, na kudai hayakuwa maandamano, hilo ni pungufu moja wapo, yale yalikuwa ni maandamano ya amani na hakuna Ushahidi wowote wa waandamanaji kubeba silaha.
26. Tume imeshindwa kutoa taarifa au kufanya uchunguzi kuwa katika yale maandamano ni watu wangapi wamepotea kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
27. Tume imchitimisha kwa kuonesha kuwa nguvu iliyotumika kudhibiti ghasia wakati na baada ya uchaguzi iliwiana na tukio husika, sisi tunasisitiza kuwa nguvu iliyotumika haikuwiana kwani kulikuwa na matumizi makuhwa ya nguvu.
28. Tume inabainisha matumizi ya nguvu kupita kiasi yaliyopelekea mauaji lakini bado wanapendekeza polisi hao hao wajichunguze hii sio sawa na haiwezi kututoa kwenye mkwamo huu.
29. Tume imeshindwa kutoa mapendekezo ya kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa nchi nzima, watu wanajiuliza hayo mariadhiano ambayo Tume inapendekeza yatafanyikaje bila Ukweli, uwazi na uwajibikaji wa wahusika?, lakini pia Tume imeshindwa kuelekeza ni hatua gani kwa utaratibu gani zinapaswa kufuata
katika hatua hizo za maridhiano
5.0 Ushauri na wito wetu
Ndugu waandishi wa habari,
Kufuatia uchambuzi wa taarifa ya Tume ya Jaji Chande, tunatoa msimamo na ushauri ufuatao kwa maslahi ya haki, uwazi na mustakabali wa taifa:
iv.Hatuungi mkono hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Chande na tulishatoa msimamo toka awali, na tunaamini taarifa/hotuba hiyo sio kipimo sahihi cha kututoa kwenye mkwamo huu, Kuna haja ya kuundwa chombo huru na shirikishi kitakachotoa majawabu kwa wananchi wa Tanzania.
Serikali inapaswa kukiri matumizi ya nguvu kupita kiasi na kupelekea vifo vya watu, kwani waandamanaji au raia wanahaki ya kulindwa sio kuuwawa bila hiyo hatua ya awali ya Ukweli, Haki na Uwajibikaji hakuna namna ambayo Taifa linaweza kutoka katika Mkwamo huu.
Hatuungi mkono pendekezo la kuundwa kwa chombo kingine cha kijinai kushughulikia masuala yaliyobainishwa na Tume. Tunaamini kuwa Tume ya Mheshimiwa Jaji Chande ilikuwa na uwezo na mamlaka ya kushughulikia masuala hayo, uwezo huo unatokana na hadidu ya mwisho ya rejea inayosema mambo yoyote yatokanayo kama kuna jinai ni mambo yatokanayo, ni dhahiri kwamba tume imeamua kwa makusudi kukwepa kufanya hivyo jambo linalo ashiria ukosefu wa utashi wa kisiasa wa kutaka kubaini chanzo halisi cha vurugu na mauaji hayo na asilani si ukosefu wa uwezo,
Kwakuwa vyombo vya dola na vya upelelezi ni wa tuhumiwa namba moja, na Tume ya Jaji Chande imeshindwa kufanya kazi hii, tunapendekeza ni muda muafaka sasa wa chombo huru kuundwa kufanya shughuli hii, ambao ni Jaji Mmoja atakayechaguliwa na chama cha majaji na mahakimu Tanzania, Mwakilishi wa Umoja wa Afrika wa haki za binadamu, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kitengo cha haki za binadamu, Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria, Mwakilishi wa Chama cha Madaktari, na Mwakilishi wa Jumuiya ya Madola, wahusika wote wachaguliwe na vyama au taasisi zao, kama ambavyo chama cha wanasheria Tanganyika kiliomba kupitia mahakama kuu katika shauri la Tanganyika law Society dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Police na Wenzake na Shauri la Rosemary Mwakitwange na wenzake 2 dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Tume na wajumbe wanzake, shauri Na. 32537 la mwaka 2025. Chombo hicho kingejumuisha watu wasiofungamana na upande wowote kutoka nje ya nchi kufanya kazi hii ya kubaini wahusika na hatua stahiki kuchukuliwa, kama ambavyo Jaji Chande alifanya kwenye nchi nyingine.
V. Wote waliohusika na mauaji na matumizi ya nguvu kupita kiasi, kama ilivyokaririwa katika taarifa ya Tume, wanapaswa kuwajibishwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria hila upendeleo wowote,
vi. Kabla ya mchakato wa maridhiano lazima kuwe na ukweli, uwazi, uwajibikaji( wa binafsi na wa kitaasisi) kwani taasisi nyingi zimehusika katika kutufikisha hapa kwa mfano Mahakama, TCRA, INEC, CHRAGG, POLISI, Msajili wa Vyama Vya Siasa, kukiri makosa na kuomba msamaha kwa Watanzania, kuwafidia waathirika wa vifo na majeruhi Kujua hatima ya Watanzania waliotekwa na kupotezwa na kuachiwa kwa watuhumiwa ikiwemo kusitishwa na kuondolewa kwa Mashtaka yote yenye Viashiria vya kisiasa na kukubali uchunguzi huru ndipo wazo la maridhiano shirikishi linaweza kuletwa mbele ya umma.
vil.Mchakato wa maridhiano bila kufuata Msingi tuliyo eleza hapo juu haupaswi kuanza kwani hauwezi kuliponya taifa, Maridhiano yanapaswa kuwa ya kweli na kuongozwa na vyombo huru kama SADC, AU au Umoja wa Jumuiya ya Madola ambao utahusisha watu huru na makundi ya watu walioteswa au wanaokandamizwa na watawala au wahusika wa hizi ghasia.
viii.Nia ya dhati ya kuwa na katiba mpya ipewe nguvu za kisheria na kikatiba ambayo itakuwa na utaratibu muda na commitment ya dhati ya serikali kwenye kupata katiba mpya
ix TLS, itachukua hatua stahiki Kushirikiana na wadau wengine kama ilivyo azimiwa katika mkutano wake mkuu wa Mwaka kuratibu hatua za Mabadiliko ya Katiba, sheria kwa kuona Umuhimu wa kushawishi Uwepo wa muongozo wa kisheria na Kikanuni wa utungwaji wa katiba mpya na kusimamia upigaji kura wa kura ya ndio au hapana, mehakato huu utafanyika kwa ushirikiano wa mawakili wote nchi nzima.
Mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya lazima uanze na suala la msingi la muundo wa muungano unaotakiwa. Kura ya maoni kuhusu hili lazima isimamiwe na tume huru ya uchaguzi na si tume iliyopo sasa hivi kwani uhuru wake unatiliwa mashaka na wananchi wengi. Hii itasaidia mchakato wa katiba mpya kutokwama kama ilivyokuwa mara ya mwisho, rasimu ya katiba itazingatia maoni ya wananchi juu ya muundo wa muungano.
xi.Wanasiasa wasishirikishwe kabisa katika bunge la katiba na rasimu ya katiba itayarishwe na timu ya wataalamu wachache sana wabobevu kwenye masuala ya katiba, bunge la katiba liwe na kazi moja tu ya kupitisha katiba kielelezo na sio kuijadili, kubadili na au kuongeza.
Bunge la sasa lisiwe bunge la katiba kwani bunge hili halina uhalali unaotakiwa na ibara za 8(1)(a) ya katiba na 5(1) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
N. TLS kama ilivyoelekezwa na Mkutano wake Mlaru wa Mwaka itachukua hatua kuanganisha wananchi na taasisi za kiraia katika kuratibu jitihada mahususi za wananchi kushiriki kikamilifu mchakato wa Katiba Mpya na ianze kuchukua hatua hizo mara moja bila kuchelewa kwa kuanza na makongamanno ya ndani na nje. kama sehemu ya kushughulikia chanzo kikuu cha malalamiko ya muda mrefu ya wananchi lakini haupaswi kusimamiwa na bunge la chama kimoja ni Lazima bunge la katiba liundwe na lipitishe katiba husika.
NIV. Kuendeleza mchakato wa nchi kupata katiba mpya kwa kuwa na sheria iliyotungwa na bunge ambayo itaweka utaratibu wa kufanyika kupitia katiba mpya. Kwa vile mara ya mwisho mchakato huu ulikwama kwenye muundo wa muungano sheria hii iweke bayana kuwa tutaanza na kura ya maoni ambayo itabidi isimamiwe na tume ya uchaguzi iliyo huru sio tume hii. Baada ya kupata muafaka wa muundo wa muungano timu ya wataalamu, itakayoundwa na wabobezi wachache wa masuala ya katiba wasiofungamana na upande wowote wasiozidi 10 ili ipitie maoni na rasimu/Katiba kielelezo ya katiba ya Jaji warioba ili kuandaa rasimu ya katiba ambayo itapelekwa kwenye bunge la katiba kwa ajili ya kupitishwa tu bila mabadiliko yoyote.
XV. Wafungwa wote wa kisiasa wanaoendelea kushikiliwa gerezani kuhusiana na matukio ya Oktoba 29, 2025 mashauri yao yaendeshwe kwa uharaka na wale watakaonekana hawana hatia waweze kuachiliwa mara moja.
xvi. Watu wote waliotekwa na kupotezwa, ambao kwa mujibu wa taarifa ya Tume ni zaidi ya watu 245 na bado hawajapatikana, wanapaswa kupatikana au kuachiwa mara moja bila masharti yoyote. Iwapo wapo waliofariki, basi ndugu zao wapatiwe miili ya wapendwa wao kwa wakati ili waweze kuwazika kwa heshima inayostahili.
xvii. Tunatoa wito na Kumshauri Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuitoa taarifa ya Jaji Chande hadharani kwa sababu taarifa hiyo sio yake binafsi ni ya umma na imeandaliwa kwa fedha za umma ni muhimu umma ukajua undani wa taarifa hiyo kwa kuwa Umma wa Watanzania unao waweka madarakani wale wote waliokatika mamlaka kwa mujibu wa lhara ya 8(1)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977
xviii. Wahusika wa mauaji, utekaji, utesaji na mateso kwa Watanzania, kabla, wakati na baada ya uchaguzi hawawezi kusikilizwa na mahakama zetu maana zinamgongano wa kimaslahi ni muhimu jumuiya ya kimataifa ikaingilia kati na kuunda Mahakama za kimataifa za muda (Ad hoc Court, kama ICTR, ICTY au Special Court for Sierra leone) au Suala hili kupelekwa ICC. Kwamba tutegemee huyu mwendesha mashitaka ambaye amehusika kuwabambia kesi za uhaini mamia ya Watanzania, anayeteuliwa na Rais na kupewa maelekezo ya nani wa kumkamata na nani wa kuamuachia anaweza kufanya kuendesha kesi dhidi ya viongozi wakubwa
waliohusika?, Hili linakinzana na busara ya kawaida ya kisheria kwamba Mtu asijihusishe na shauri ambalo maslahi yake yanaweza kuathiri maslahi ya uamuzi husika NEMO JUDES IN CAUSA SUE tunasisitiza kushauri na kuhimiza umuhimu kuwa na chombo huru kitakachoweza kuaminiwa kufanya kazi hii bila upendeleo wala kuonea watu.
xix.
Kuendelea kuunda Tume juu ya Tume, ni kujaribu kuahirisha tatizo na sio kulikabili, tukiendelea kutumia gharama za wanachi kukwepa uwajibikaji, tutajikuta 2030 hatujafanya lolote na linaweza kutokea tatizo kubwa zaidi ya hili.
Xx. Tanzania inapaswa kuridhia Mikataba ya kimataifa inayohusiana na ulinzi wa watu ili kuendana na kasi ya dunia, Mfano Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Watu Wote dhidi kupotezwa na kutekwa kwa watu (ICPPED) wa Mwaka 1994 Na Mkataba wa Kimataifa dhidi ya Utesaji (UNCAT) wa Mwaka 1984 na Mikataba mingine ya ulinzi wa watu.
xxi. Mahakama ya Rufaa inapaswa kupanga na kusikiliza kwa haraka Rufaa zote zinazohusu kesi za kikatiba ambazo zinalenga kurekebisha mfumo wa utawala wa sheria na utawala bora, TLS tuko tayari kuongoza kwenye hilo.
Katika kuhitimisha tunasema kwamba bila Ukweli, Haki na Uwajibikaji na kuchukuliwa kwa hatua za kweli za kurekebisha mapungufu yote yaliyojitokeza, kuna hatari kwamba katika Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa 2029 na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2030 hali itakuwa mbaya zaidi, tusirudie makosa
Na kwamba TLS tuko tayari kuongoza Jitihada stahiki za pamoja na Kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wadau wote wa ndani na nje ya nchi ikiwemo Mashirika ya kijamii ya ndani na nje ya nchi, Mashirika ya Kimataifa na Taasisi za Umma bila uwoga, hofu au upendeleo ili kupata namna bora na endelevu ya kuondoka mapungufu yote yaliyochangia kutufikisha katika hali hii.
KUHUSU KESI ZA JINAI ZINAZOMKABILI TUNDU ANTIPAS MUGHWAI LISSU
Ndugu waandishi wa habari,
Tundu Antipas Mughwai Lissu ni mwananchama wa Chama cha Sheria Tanganyika (TLS) na ni wakili mwenye namba ya Usajili 945. Tundu Antipas Mughwai Lissu aliwahi kuwa Rais wa Chama Cha Sheria Tanganyika kuanzia Mwezi wa Machi 2017 mpaka Mwezi Septemba 2017 aliposhambuliwa na Risasi na ikalazimu aende nje ya nchi kwa matibabu na hatua za kunusuru Uhai wake.
Ni katika Mutkathda huo Lissu kama mwanachama wetu na sisi katika kutimiza wajibu wetu kisheria kwa wanachama wetu tunaona inapaswa kusemewa kuhusu dhahma ambayo anakumbana nayo sasa hivi hususani kuhusiana na kesi mbili za jinai ambazo anakabiliana nazo.
Katika kutimiza haki yake ya kikatiba chini ya ibara 20(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 kama ambavyo imekuwa ikirekebishwa mara kwa mara Tundu Atipas Mughwai Lissu alijiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kupitia chama hicho alichaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Mwaka 2025 Januari Tundu Antipas Mughwai Lissu alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho cha siasa.
Katika kutekeleza haki yake ya kikatiba Tundu Antipas Mughwai Lissu akiwa kama Mwenyekiti wa chama hicho amekuwa akidai mabadiliko ya sheria za uchaguzi nchini Tanzania katika azma ya kuleta sheria ambazo zinahakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na wa haki kwa mujibu wa Ibara ya 5(1) ya Katiba.
Kauli zake hizo zikasababisha awe matatani na mnamo tarehe 9 April 2025 akiwa katika mkutano wa hadhara huko wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma alikamatwa na Polisi na kuletwa hapa Dar es salaam na kufunguliwa kesi mbili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kesi ya kwanza ni kesi ya uchochezi, kesi ambayo ina dhamana ni kesi namba 8606 ya mwaka 2025 ambayo bado iko Mahakamani na upande wa mashitaka bado haujaanza kuita mashahidi na haijulikani ni kwa nini kesi hiyo imesimama bila kuendela kusikilizwa. Kesi hii haina uhusiano wowote na kesi nyingine ya pili hapo chini
Kesi ya pili inahusu kosa la Uhaini, kosa lisilodhaminika, ni kesi namba 000019605 ya Mwaka 2025, ambapo anatuhumiwa kuwa mshitakiwa alitaka kupindua nchi kwa matamko yake aliyoyatoa wakati anahutubia mkutano wa ndani wa chama akihutubia wanachama waliokuwa wanatarajia kugombea nafasi mbali mbali katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Kesi hizo zote mbili zililetwa kwa mara ya kwanza tarehe 10 April 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam.
Kesi ya pili ambayo ina kosa la uhaini kwa mujibu wa sheria za Tanzania haiwezi kusikilizwa na Maahakama Kuu mpaka pale Mahakama ya hakimu Mkazi itakapofanya kabidhi mwenendo na mshitakiwa kuwa commited Mahakama Kuu ambayo ndiyo mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Kabidhi mwenendo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilifanywa kati ya tarehe 10 April 2025 mpaka tarehe 18 Agosti 2025 kipindi cha miezi 5 na siku 8.
Katika kabidhi mwenendo hizo upande wa mashtaka uliiarifu mahakama ya Kisutu kuwa itaita mashahidi 30 kuthibitisha kosa hilo.
Kesi hii ilikaa bila kusikilizwa kwa takribani mwezi mmoja na siku 4 na ikaletwa Mahakama Kuu kwa mara ya kwanza tarehe 22 Septemba 2025 na ikaendelea kusikilzwa mfululizo na baadae kuahirishwa tena.
Kuahirishwa kwa shauri hili siku chache kabla ya uchaguzi mkuu, kwa sababu ambazo mahakama inazifahamu iligongana na mapumziko ya mwaka ya mahakama za juu ambayo huanza tarehe 15 Disemba kila mwaka na kuisha tarehe ya kwanza ya kazi ya mwezi wa pili
Pamoja na tangazo la likizo la mahakama kutamka wazi kuwa kesi za jinai hazihusiki na likizo hiyo lakini mahakama bado haikusababisha kesi hii iendelee. Tulitegemea kuwa kwa sababu uhaini linatamkwa kuwa ni kosa la juu kabisa chini ya katiba ya Jamhuri ya Tanzania chini ya Ibara ya 28 (4) lisingeguswa na likizo ya mwaka ya Mahakama Kuu.
Shauri hili lilipangwa kuendelea kusikilizwa tarehe 16 Februari 2026, ambapo upande wa mashitaka uliendelea kuita mashahidi wake na ikafika mahali upande wa mashitaka wakaleta ombi la kuongeza mashahidi Zaidi ya wale waliotajwa katika kabidhi mwenendo, ombi ambalo lilikataliwa na Mahakama Kuu.
Upande wa waendesha mashitaka hawakuridhika na uamuzi huo mdogo na hivyo wakaamua kupeleka shauri hilo kwa mapitio kwenye Mahakama ya Rufaa Tanzania. Kwa utaratibu uliopo ni kuwa mara jalada la kesi linapopelekwa Mahakama ya Rufaa basi Mahakama ya chini inakuwa haina mamika ya kuendeea na shauri husika, vivyo hivyo ndivyo ambayo kesi ya Tundu Antias Mughwai Lissu ilisimama kwa mara nyingine tena kusikilizwa kwa maombi ya mapitio kama yalivyo wasilishwa na upande wa mashtaka.
Mpaka sasa ni takribani miezi mitatu toka upande wa mashitaka ulivyopeleka maombi yake ya mapitio Mahakama ya Rufaa na hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa kuna jopo la Mahakama ya Rufaa limepangwa kusikiliza maombi hayo ya mapitio.
Utaona kuwa mpaka sasa ni karibia mwaka mmoja na mwezi mmoja na siku kadhaa tokea mshitakiwa tundu Antipas Mughwai Lissu alipofikishwa Mahakamani kwa kosa la uhaini kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri na kosa ambalo halina dhamana.
Ndugu waandishi wa habari kutokana na historia fupi ya shauri hilo vitu vifuatavyo ni Dhahiri
1. Upande wa mashitaka hauna nia ya dhati ya kuendelea na shauri hili la uhaini dhidi ya Tundu Atipas Mghwai Lissu
2. Kesi mpaka leo imechukua mwaka mmoja mwezi mmoja na siku kadhaa toka siku ambayo kesi hii ililetwa Mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza.
3. Kuhairishwa na au kutoendelea na shauri hili mara zote hizo imetokana na upande wa mashitaka na mahakama mshitakiwa hajahusika hata kidogo na ucheleshaji wa kesi hil.
Tunapenda kukumbusha usemi usemao haki inayocheleweshwa ni sawa na haki inayonyimwa. Kushindwa kuendelea kwa kesi hii kumesababisha ukiukwaji wa haki ya kikatiba ya mwanachama wetu. Ikumbukwe kuwa kosa la uhaini halina dhamani hivyo
mwananchama wetu yupo korokoroni kwa kipindi chote hicho. Kitendo cha kuchelewesha kusikilizwa shauri ni ukiukwaji wa Dhahiri wa ibara ya 13(6)(a) ambayo inatamka kuwa:
Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba-
(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote inapohitajika kufanyiwa maamuzi na mahakama au chombo kingine chochote kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika:
kusikilizwa kwa ukamilifu ni pamoja na kumalizika kwa kesi haraka.
Ndugu waandishi tunakumbusha kuwa haki ya kumalizwa shauri kwa haraka inalenga
1. Kuhakikisha kuwa wenye makossa yasiyodhaminika yanamalizwa haraka ili kumuwezeshsa mshitakiwa aliye mahabusu kuweza kuwapata mashahidi wake kwa harahaka na pia kumuwezesha kuwa na kumbukumbu za kesi yake na hivyo kumfanya aweze kujenga utetezi wake madhubuti,
2. Haki ya jamii kuwa na Imani na Mahakama na kujua kwa haraka hatma ya kesi ambazo wananchi wanafuatilia.
3. Kupunguza msongo wa mawazo kwa mshitakiwa ambaye anakaa muda wote anafikiria majaliwa ya shauri lake na inakuwa halisia zaidi pale mshitakiwa anaposhitakiwa kwa kosa ambalo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa
Katika hili tunapenda kusisistiza kuwa haki ya shauri kusikilizwa haraka inahusu mashauri yote ya jinai makubwa na madogo na haki hii inahusika zaidi pale mshitakiwa anapokabiliwa na kosa ambalo halina dhamana ili kuwezesha kujua hatma ya shauri lake katika muda mfupi sana.
Tunapaswa kuangalia vigezo vifuatavyo ili kubaini kama shauri husika limecheleweshwa au la:
1. Muda ambao shauri limechukua, shauri linalochukua zaidi ya mwaka toka kukamatwa kwa mshitakiwa bila kumalizika inakuwa imekiuka haki ya usikilizwaji wa shauri kwa uharaka
2. Sababu za uchelewefu wa kesi; upande gani umesababisha kesi kutofikia tamati, katika shauri la Lisu upande wa mashitaka na mahakama ndio umesababisha
3. Je mshitakiwa amekuwa akisisistiza kesi yake kuisha haraka: katika shauri la Lisu mshitakiwa amekuwa, toka mahakama ya kisutu akisisitiza kuwa upande wa mashitaka unachelewesha kesi
4. Je Mshikakiwa ameathirika: ni Dhahiri kuwa mshitakiwa ameathirika na uchelewefa huo.
NINI KIFANYIKE
1. Shauri lililopelekwa Mahakama ya Rufaa lisikilizwe kwa uharaka iwezekanavyo ili haki ionekane kutendeka kwa wakati. Kama usikilizwaji wa Shauri hilo kwa uharaka inashindikana basi Mshitakiwa aachiwe huru kwani kwenye kesi ya uhaini inayomkabili uchelewefu huu ambao ni kinyume cha ibara ya 13(6)(a) ya katiba hautokani na mshitakiwa bali unatokana na upande wa mashitaka na mahakama kushindwa kuwa na usimamizi madhubuti na uendeshaji wa kesi
2. Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu kwa uharaka iendelee na usikilizwaji wa kesi ya uchochezi ambayo haiendelei na hakuna sababu zozote za kufanya kesi isiendelee na kama Mahakama inashindwa kuendelea na usikilizaji wa shauri hili basi mshtakiwa aachiwe huru
Imetolewa Na:
Tanganyika Law Society (TLS)