Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Naomba kuwakilisha hoja tuchemshe Bongo na kufanya tathmini ya Watanganyika na Tanganyika tangu mwaka 1400 hadi mwaka 1945.
Naomba radhi kwa Watanzania wenzangu wa Zanzibar, kwa kuwatenga katika hili, ila michango yeno katika kufanya tathminihii inapokelewa.
Je historia ya Watanganyika ni ipi? Asili yao ni wapi? Katika kufanya tathmini hii, naomba tuangalie Watanganyika kama watu kwa kutumia vigezo vya mfumo wa kijamii, kiuchumi na hata kisiasa.
Je historia tunayohadithiwa kila siku ina ukamili wa kweli? Ukiangalia hata miaka 120 ya mwisho, bado kuna utupu mkubwa wa kuwatambua Watanganyika na nchi yao. Tunajua baada ya mkutano wa Berlin, tuligeuzwa kuwa Koloni, kisha kuna kuja hadithi za kina Karl Peters, Abushiri, Kinjekitile, Mkwawa, Milambo, Mangi Meli halafu tunachipuka na TAA, TANU, Nyerere kisha Uhuru.
Lakini mnaomba turudi nyuma, je jamii za Watanganyika zilikuwa zinaishije miaka hiyo? zilikuwa na mifumo ya namna gani ya kimaisha hasa katika malezi na kujiongoza iwe ni kisiasa, kujizalishia na biashara katika uchumi na mahusiano mengine?
Siwafichi nawaonea gere wenzetu wa Zanzibar ambao wana historia iliyonona, ambayo inaonyesha wazi wao walikuwa na mfumo gani wa kiutawala, mfumo gani wa kiuchumi na mahusiano ya namna gani ya kijamii ambayo pamoja na matatizo na mizunguko yote iliyotokea Zanzibar, bado wana historia na wanaeleweka na wanajivunia asili yao.
Nikichukua mfano, je Wanyakyusa, Wamatengo, Wanyiramba, Wachaga, Waha, Wazigua, Wakurya, Wahaya, Wamakua, Wazaramo, Wafipa na kabila nyingin nyingi, je zilikuwa katika mfumo na muundo gani wa kimaisha kabla ya kuingiliana na mifumo ya kieni na hata baada ya kuingiliana na mifumo ya kigeni iwe ni Waarabu, Wagiriki, Waajemi, Wahindi, Wareno hata Waingereza?
Nasukumwa kujiuliza maswali haya ikia ni shauku yangu si kwa ajili ya historia pekee, bali kujijua kama Mtanganyika na sasa Mtanzania, nafasi yangu na muundo wa asili yangu, fikra , tabia na mapokeo mengine ni ya namna gani na hasa kwa kutathmini kuwa Watanganyika tupo tupo tuu kama vile ni watu wasio na dira au mwelekeo?
Iweje Wazanzibari wana hazina kubwa si ya kihistoria kwa maandishi tuu, bali hata vitendo vinavyoonekana ambavyo dhahiri kuna sehemu kubwa ni vyao vya asili na si maingiliano na Waarabu au Wazungu pekee?
Nikijiangalia kama Mtanzania na nafasi na asili yangu kama Mtanganyika, najiuliza, vizazi 10 kabla yangu vilikuwa ni vya watu wa namna gani? Wawindaji, Wahunzi, Wafanyabiashara, au Wahangaikaji wa mwituni? Je upeo wao wa kujituma kufanya kazi, kufikiri, kujiongoza, kuwajibika, malezi ya familia na mengine mengi yalikuwa yanafananaje kabla ya kukutna na tamaduni hizi ngeni ambazo leo ndio tunajivunia kuwa ndio asili yetu mpya?
Kama tuliamini kuwa kuna Miungu, ilikuwa ni kwa kazi gani na tulianzaje kuwa na imani ya Miungu moto, mlima, mti hata nyoka kabla hatujapewa hadithi za Mtume Muhamad na Yesu?
Tunapojiangalia leo kama Taifa, je tunarudi nyuma kihistoria kwa umbali gani kujipima tulikotoka na tunakokwenda? Je kama Watu na nchi yetu Tanganyika na hata sasa Tanzania, je tulifanya nini kabla ya Utumwa na Ukoloni ambacho kingetupa utambulisho rasmi?
Tunafahamu hata miaka 200 iliyopita Wazulu walikuwa na historia. Ukienda Congo ambako ndiko tunaambiwa chimbuko la Bantu Migration, kulikuwa na historia. Je historia na kuwepo kwetu ni kutokana na Shaka Zulu na vita vya Mfekane, au kutoka kwetu kama wahangaikaji kuanzia kule kwa Malkia Nzinga, tukatambaa mpaka Bunyoro na kwa kina Rumanyika na kuishia Idodomiya?
Changamoto kwenu ndugu zanguni!