Tathmini yakinifu uzinduzi wa mikutano ya siasa Mwanza

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Chadema kama chama tegemeo kwa ukombozi wa nchi hii ni tofauti sana na vyama vingine. Tofauti kubwa iliyopo ni kuwa chawa kama wale wa Mama huku si sifa bali ni machukizo.

Chadema iliyoko mioyoni mwa watu hutambua wakichemka wao na hata tunapochemka sisi. Hii ni bila kujali mpiga fyongo ni mkubwa au mdogo, ni Mbowe au Lema.

"Kama watoto mapacha hutokea wakati wakashindwa kuelewana sembuse miye na wewe Neema?"

Ipo kwenye rekodi kuwa Mbowe amewamwagia misifa Mama na polisi. Mbowe kaonyesha jinsi gani maridhiano hayakuwa rahisi. Yeye kama mtu mzima akiyafananisha na kumshawishi demu 😀😀."

FnDpVh9XoAAQkab.jpeg

"Mwenye macho haambiwi tazama wala mwenye masikio kwamba hakusikia."

Kwenye hotuba yake Mbowe kasisitiza umoja na vyama vingine dhidi ya mapande mapande ya uvyama kwenye ukombozi wa nchi hii. Ni wazi kuwa nchi hii haitakombolewa na Chadema peke yao.

Kwa upande mwingine ni wazi kuwa kiu ya watu haikutibiwa jana. Hii ikizingatiwa yapo mengi tuliyoyategemea pamoja na kuwa muda ulikuwa mchache:

https://www.jamiiforums.com/threads/chadema-jifunzeni-kwenye-ziara-ya-makamu-wa-rais-kahama.2057817/

-- hatukujifunza. Hii safisha njia kwa ajili ya viongozi kupita na kunakoitwa ulinzi kuimarishwa ni kero, na wananchi hawaipendi.

Ni muhimu Chadema kujitofautisha nao. Hata hii ya ma bodyguards mgongoni haina tija. Ya CCM yasiwe yetu.

https://www.jamiiforums.com/threads/mikutano-ya-siasa-wamebana-wameachia.2053571/

https://www.jamiiforums.com/threads...jibu-wa-kutengeneza-ajira-ni-ya-nini.2056617/

-- zipo kero nyingi kwa watu ambao hao ndiyo ulio mtaji wetu halisi. Kuruhusu mikutano au kukubali kuridhiana hakuwezi kutafsiriwa kama hisani. Labda tu ikiwa adui akisifiwa ni kwa kuwa kauvaa mkenge!

https://www.jamiiforums.com/threads...a-serikali-msitake-faida-tu-wekezeni.2052039/

https://www.jamiiforums.com/threads...-haramu-inaposhangilia-mapato-haramu.2053553/

Hata hivyo si mbaya wakatuita wanavyotaka, ila 25 Jan kitaeleweka tu.

Izingatiwe:

https://www.jamiiforums.com/threads...f-mtikila-julius-malema-au-kina-tutu.2013213/

Na pia:

https://www.jamiiforums.com/threads/chadema-bila-kuwapa-makavu-hakuna-katiba-mpya.1906749/

Mh. Tundu Lissu karibu nyumbani, ulipo tupo.

Aluta Continua.
 
Ipo kwenye rekodi kuwa Mbowe amewamwagia misifa Mama na polisi. Mbowe kaonyesha jinsi gani maridhiano hayakuwa rahisi. Yeye kama mtu mzima akiyafananisha na kumshawishi demu
Kweli haikuwa kazi rahisi. Pia Rais amekuwa jasiri kutetea maslahi ya Taifa badala ya kundi dogo la walanguzi
 
Kwa upande mwingine ni wazi kuwa kiu ya watu haikutibiwa Jana. Hii ikizingatiwa yapo mengi tuliyotategemea pamoja na kuwa muda ulikuwa mchache
Kwa matatizo yaliyoachwa na awamu ya Tano ni ngumu sana ku- address yote. Watu nado wana hamu yao.
 
Chadema kama chama tegemeo kwa ukombozi wa nchi hii ni tofauti sana na vyama vingine. Tofauti kubwa iliyopo ni kuwa chawa kama wale wa Mama huku si sifa bali ni machukizo.

Chadema iliyoko mioyoni mwa watu hutambua wakichemka wao na hata tunapochemka sisi. Hii ni bila kujali mpiga fyongo ni mkubwa au mdogo, ni Mbowe au Lema.

"Kama watoto mapacha hutokea wakati wakashindwa kuelewana sembuse miye na wewe Neema?"

Ipo kwenye rekodi kuwa Mbowe amewamwagia misifa Mama na polisi. Mbowe kaonyesha jinsi gani maridhiano hayakuwa rahisi. Yeye kama mtu mzima akiyafananisha na kumshawishi demu 😀😀."

"Mwenye macho haambiwi tazama Wala mwenye masikio kwamba hakusikia."

Kwenye hotuba yake Mbowe kasisitiza umoja na vyama vingine dhidi ya mapande mapande ya uvyama kwenye ukombozi wa nchi hii. Ni wazi kuwa nchi hii haitakombolewa na Chadema peke yao.

Kwa upande mwingine ni wazi kuwa kiu ya watu haikutibiwa Jana. Hii ikizingatiwa yapo mengi tuliyotategemea pamoja na kuwa muda ulikuwa mchache:

https://www.jamiiforums.com/threads/chadema-jifunzeni-kwenye-ziara-ya-makamu-wa-rais-kahama.2057817/

-- hatukujifunza. Hii safisha njia kwa ajili ya viongozi kupita na kunakoitwa ulinzi kuimarishwa ni kero, na wananchi hawaipendi.

Ni muhimu Chadema kujitofautisha nao. Hata hii ya ma bodyguards mgongoni haina tija. Ya CCM yasiwe yetu.

https://www.jamiiforums.com/threads/mikutano-ya-siasa-wamebana-wameachia.2053571/

https://www.jamiiforums.com/threads...jibu-wa-kutengeneza-ajira-ni-ya-nini.2056617/

-- zipo kero nyingi kwa watu ambao hao ndiyo ulio mtaji wetu halisi. Kuruhusu mikutano au kukubali kuridhiana hakuwezi kutafsiriwa kama hisani. Labda tu ikiwa adui akisifiwa ni kwa kuwa kauvaa mkenge!

https://www.jamiiforums.com/threads...a-serikali-msitake-faida-tu-wekezeni.2052039/

https://www.jamiiforums.com/threads...-haramu-inaposhangilia-mapato-haramu.2053553/

Hata hivyo si mbaya wakatuita wanavyotaka, ila 25 Jan kitaeleweka tu.

Izingatiwe:

https://www.jamiiforums.com/threads...f-mtikila-julius-malema-au-kina-tutu.2013213/

Na pia:

https://www.jamiiforums.com/threads/chadema-bila-kuwapa-makavu-hakuna-katiba-mpya.1906749/

Mh. Tundu Lissu karibu nyumbani, ulipo tupo.
Nifundishe jinsi ya Ku-attach link kama hizi
 
Kweli haikuwa kazi rahisi. Pia Rais amekuwa jasiri kutetea maslahi ya Taifa badala ya kundi dogo la walanguzi

"-- zipo kero nyingi kwa watu ambao hao ndiyo ulio mtaji wetu halisi. Kuruhusu mikutano au kukubali kuridhiana hakuwezi kutafsiriwa kama hisani." Labda tu ikiwa adui akisifiwa ni kwa kuwa kauvaa mkenge!
 
Nifundishe jinsi ya Ku-attach link kama hizi
Kuanzia leo kuna katatizo kwenye hiyo ku attach links. Itabidi kuwaambia Mod. Mapema ilikuwa ni bora zaidi. Angalia zilivyokuwa zinakuwa kwenye uzi huu;

https://www.jamiiforums.com/threads...epole-ndugai-na-wengine-tujitathmini.2042603/

Ila zipo njia mbili:

1. kwenye list ya nyuzi highlight Uzi unaotaka chagua "copy link address" Kisha njoo paste unapotaka.

2. Fungua Uzi au site unaotaka. Kisha copy address yake kwenye address bar uende ku paste unakotaka.

Kisha Post reply au save.

Kisha rejea kwenye edit futa maneno haya pekee:

unfurl="true"

Kisha save.
 
Thanks Mkuu
 
Makelele yote ya kumuona Mbowe mbaya kwa sababu ya maridhiano,, simply yanaonesha miongoni mwetu tulivyo wabinafsi , wenye chuki, tusivyo na mapenzi kwa maslahi ya taifa, na zaidi, yanaoonesha vile wengi bado hawajakomaa kwa ajili ya kuongoza nchi, wametawaliwa na mihemko.

Kama Mbowe anayepigania kuunganisha taifa leo anaonekana mlamba asali, maana yake watu hawa wanataka kuendeleza siasa za visasi, na kutoaminiana, matokeo yake kuzidi kuligawa taifa, bila kujua siasa ni sayansi, ni ngumu sana kuyafikia malengo mliyojiwekea.

Wafuasi wa Chadema mitandaoni wakati mwingine naona wanajiona kama malaika, sharti ufanye vile watakavyo, wao wanajua kinachozungumzwa hata kwenye mikutano wasiyohudhuria, wanahukumu kwa hisia, na hawataki ujitetee, hawa ni madikteta wasiotaka kumsikiliza mtu.

Endapo Chadema ikipata kiongozi atakayekuja kufanana nao akili, naona siasa za kiharakati zitarudi kwa nguvu na upesi sana, kukimbizana na polisi ndio itakuwa chai ya asubuhi, na sina kumbukumbu lini harakati za sampuli hiyo ziliwahi kufanikisha malengo yao.
 
Back
Top Bottom