Wizara aliyoongoza Ummy Mwalimu inaitwa afya, jinsia, wazee, walemavu na watoto.
Hiyo aspect ya ‘jinsia, wazee, walemavu na watoto’ ni sehemu ya social services inayodili na mambo ya safeguarding za hayo makundi na promotion za welfare zao.
Kila kukicha mtu kachinja mke, watoto wanalawitia, mama sijui kanyan’ganywa mtoto, mimba za utotoni bado tatizo, marginalised group mahitaji yao ya msingi kupata utata, standardisation ya huduma za afya zina variation kituo kwa kituo; kila kitu ovyo.
Wanachojivunia ni kuongeza miundombinu na budget ya dawa, but that has nothing to do with outcome ya wizara nor tackling social issues.
The woman is just incompetent kuongoza hiyo wizara. Alipewa hiyo nafasi kwa sababu ata hao mamlaka ya uteuzi sidhani kama wanaelewa competent skills za kupambana na hizo changamoto nilizo taja hapo juu.
Kumuweka Ummy Mwalimu kwenye hiyo wizara ata akirudishwa ni dharau kwa hayo makundi ni sawa na kusema serikali aioni umuhimu wa kupunguza hizo changamoto.
Basically baraza la mawaziri lililopita mawaziri waliojitahidi kwa upande wangu walikuwa Jaffo, Biteko na kwa mbali Bashe (Hila huyu ni tatizo anafahamu vitu juu juu tu hiko siku mapendekezo yake yatawatokea puani) tayari washaona kwenye pamba upuuzi wake wa price floor serikali ilibidi ifanye u turn wenyewe nakurudi kwenye bei za soko.