Hapana, ngoma asipewe thank you, ngoma bado ana vitu vingi kiukweli, ngoma na debora wakicheza double pivot ni hatari, lakini changamoto simba haina namba 10 mnyumbulifu, mwenye jicho la pass ya mwisho, mwenye kuchezesha watu wote pale juu, yule jean charles inabidi abadilike aboreshe mapungufu yake.. La sivyo ni mchezaji wa kawaida, itabidi simba icheze 4-4-2, simba wacheze na double strikers, mkicheza na mfumo wa striker mmoja maana yake namba 10 ana kazi ya kushuka chini, kuunganisha timu, kuivuta juu, na kuwa hatari zaidi kwenye robo ya mpinzani, jean kakosa sifa hizi.