Tatizo gani hili kwa mtoto wangu?

Tatizo gani hili kwa mtoto wangu?

Pelly

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
197
Reaction score
207
Habari zenu,

Nina mtoto wa kike ambaye kesho, tarehe 13/06/24, anafikisha miaka 11 kamili (Happy birthday in advance my daughter).

Mtoto alizaliwa vizuri ingawa alikunywa maji machafu baada ya kuchelewa kuzaliwa kwa masaa kadhaa. Hii inaweza kuwa ilitokana na mama yake kuwa na msongo wa mawazo (depression) au la, japo haikuonekana kwa wakati huo. Aliendelea vizuri tu, lakini alipofikisha miezi 6 au 9, mama yake alipoingia ndani alimkuta mtoto macho yakiwa kama makengeza. Mama jirani alimwambia macho yatakaa sawa, lakini baada ya wiki moja aliamua kumpeleka hospitali ambapo aliambiwa mtoto alitaka kupata degedege, ila macho yangekaa sawa.

Maisha yaliendelea, lakini mtoto alichelewa kuongea. Tulipata maoni mbalimbali kwamba tatizo lilikuwa ulimi kuwa umeungana kwa chini, hivyo tukampeleka akafanyiwa upasuaji mdogo na akaanza kuongea vizuri. Akiwa na miaka 3, alianza shule ya awali (baby class) na kisha darasa la 1 Montessori pale Msimbazi. Maendeleo hayakuwa mazuri, hivyo nikamuhamishia shule moja Kinondoni na akawa anafanya vizuri.

Hata hivyo, nilipata changamoto za kifedha na ikabidi nimhamishie shule ya English Medium Oysterbay. Alianza vizuri lakini darasa la 4 matokeo yakawa mabaya sana. Mungu mwema alifaulu na sasa yupo shule nyingine, lakini bado matokeo ni mabaya. Pia kuna tabia za ajabu alizonazo licha ya zingine alizokuwa nazo awali.

Anapenda kula maganda ya karanga, anapenda harufu mbaya kama ya kitu kilichooza, na chumvi. Anafanya mambo yasiyoendana na umri wake, na wakati mwingine analia bila sababu au anasema ameona kifo chake. Muhimbili kwenye afya ya akili, daktari wa watoto alisema ni suala la malezi, lakini daktari wa watu wazima alisema kuna shida kidogo pamoja na majibu ya vipimo. Kuna dawa alipewa lakini zilimchanganya kidogo tukaziacha.

Kuna mganga alisema wanamchukua msukule na nimuulize ndoto gani anaota usiku. Alisema anaota anaruka au anakula nyama. Mganga alisema nimpeleke amtibie, lakini sheikh mmoja alisema ana majini na inabidi yatolewe mapema, akanitajia pesa nyingi.

Basi hadi sasa nipo njia panda. Kwa anayejua njia za kumsaidia binti yangu naomba msaada.

Samahani kwa kuwachosha, kusummarize bado ni shida kwangu licha ya kufundishwa darasani. Ila hapa pia nimeandika vingine na kuacha vingine. Nitaviweka inapobidi.

Asanteni.
 
Hamna makosa kama dawa ulizotumia, Hizo za kumsizisha asilie wala kuota, dogo huyo ana illusions, Life will talk it all, usingempa dawa. Utampeleka sober, unakumbuka kipindi yuko vizuri, rudisha ile ratba, show her she is normal. Penda kumtoa out, asikae idle. Ila asome msisitize, ukimuweka kwa ugonjwa atabki hivo na utaishia sober boss.
 
Kwa maelezo hayo huyo mtoto ana biological neurological destruction/abnormalities. Waganga na mashehe hawez kupona. Na je anapitia vipindi mbalimbali vya kulegea mwili na kutoa mapovu mdomoni?

Familia mna mahusiano mazuri au ndo yale ya sogea uone?
 
Hamna makosa kama dawa ulizotumia, Hizo za kumsizisha asilie wala kuota, dogo huyo ana illusions, Life will talk it all, usingempa dawa. Utampeleka sober, unakumbuka kipindi yuko vizuri, rudisha ile ratba, show her she is normal. Penda kumtoa out, asikae idle. Ila asome msisitize, ukimuweka kwa ugonjwa atabki hivo na utaishia sober boss.
Asante, tunajitahidi sana kumjali hadi tukaambiwa tunamdekeza ndiyo sababu yupo hivyo,ila nashukuru kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
Pole kwa changamoto kiongozi.
KESHO kuna mti/ua nitakupigia picha ulitafute kisha utakua unamuogeshea kama sabuni yake ndani ya cku 7 tu. Ata kaa vzr TU.





KAZI ni kipimo cha UTU
Nashukuru sana I hope hapa Dar nitaupata huo mti
 
Pole sana, na hongera kwa kumjali binti yako kwa kupambana katika kuhakikisha anakuwa sawa, na happy birthday kwa binti yako Mungu ampe afya njema na maisha marefu yenye manufaa na baraka na yeye. Ikiwa mwanao amepigwa chanjo, mara nyingi matatizo kama hayo huwa yanawatokea baadhi ya watoto na kupelekea matatizo ya usonji. Jaribu kutafuta wataalamu wa magonjwa ya usonji wanaweza kukusaidia. Pole sana kwa mara nyingine tena najua jinsi gani tunavyoteseka katika kulea watoto wenye changamoto kama za mwanao.
Asante, wataalaam zaidi ya muhimbili ni wapi kama utanisaidia nitashukuru maana hata shuleni wamenipa Pole na wanasema nizunguke makanisani na endapo wataona hali inazidi kuwa mbaya watamfukuza shule tu
 
Kwa maelezo hayo huyo mtoto ana biological neurological destruction/abnormalities. Waganga na mashehe hawez kupona. Na je anapitia vipindi mbalimbali vya kulegea mwili na kutoa mapovu mdomoni?

Familia mna mahusiano mazuri au ndo yale ya sogea uone?
Asante, tupo vizuri japo uchumi sometimes unakuwa na shida vita vinatokea,sasa hapo sijui ni vizuri au vibaya? kwetu hakuna shida ila kwa mama sijui si unajua wanafichaga japo nimechunguza kama kuna bibi yao mzaa mama alikuwa na shida kama hiyo na alishapotea porini ninavyosikia
 
Back
Top Bottom