Tatizo hili ni la mke wangu tu au wanawake wote married?

Lakini kwa upande mwingine utakuta na yeye kuna madhaifu yako anayabeba! Hivyo jitahidini tu kuvumiliana!
 
Kaka wapo watu sampuli hii..nilikuwa na uncle wangu(sasa marehemu) askari magereza hapo wizarani(mambo ya ndani) alikuwa na utarati/masharti?/maagano?/ratiba? ni mwisho..na alikuwa hachagui mke,mtoto,mjomba,mfanyakazi,walinzi wote lazima kutii..ukimsalimia bila kukaa mguu sawa ni case,ukikaa kwenye kochi ukaegemea nyuma ni case,ndala za bafuni zikipishana ni case,kula wote ni saa moja jioni,kulala wote saa 3 ..ole ole wako uwashe taa usiku na usiwe na sababu za maana utamtambua..
Hii nadhani ni ndoa "bandia"!
<br />
<br />
 
katika kipindi cha miaka 12 ktk ndoa yangu nimegundua tatizo kubwa sana la mke wangu ambalo kwa ufupi ni chanzo kikubwa cha migogoro ktk ndoa yetu. Nimegundua kuwa wife wangu ni vigumu ku keep maagano au makubaliano consistently bila kuvunja. Kwa mfano mnakuta mmekubaliana kwamba tabia au mambo fulani ndani ya ndoa hupendi au yanaleta kero na ugomvi hivyo mke wangu anakubali kabisa kwamba nitaacha sitarudia tena kwani najua nakuudhi" vivyo hivyo na mimi mume nakubaliana na wife kwamba zile tabia zangu ambazo ni kero kwake nitaacha for good. Huwa nakuwa mwaminifu na nimeacha silika zinazomfanya mke wangu achukie na kukosa amani for her sake.

Mimi nilidhamiria na nimefanikiwa kuacha kabisa vitabia ambavyo ni kero na chanzo cha migogoro na wife kwani sipendi niwe chanzo cha kumfanya wife uncomfortable.

Cha ajabu ni kwamba yeye wife amekuwa na vicious cycle ya kuvunja maagano na maazimio kwa kurudia rudia mambo ambayo ni kero kwangu. Pamoja na kwamba sote ni wasomi kwa level ya masters inanipa shida kumwelewa ni kwa bahati mbaya au ni kwa makusudi anafanya anapoamua kurudia rudia tabia zinazo nikera. Ukimwuliza kwa nini umevunja makubaliano huwa mbishi na no apology na kuna uwezekano wa escalation ya ugomvi. Hii inanipa shida sana kwani huwa nataka tukikubaliana basi i keep promise kama ninavyomfanyia lakini never.
Uwezo wake wa ku maintain ahadi hauzidi miezi miwili hata kama last time ugomvi ulikuwa mkubwa kiasi gani.

Kinachonishangaza zaidi ni kwamba huyu wife kazini kwake kote alikiofanya kazi anasifiwa kwa kufanya vizuri iwe yuko na bosi mwanamke au mwanaume. Najiuliza kichwa hichohicho kinashindwaje kufanya hivyo hivyo nyumbani kisifiwe na husband?
Huyu wife ni mwepesi wa kukiri kosa na kuomba msamaha ila ndo hivyo anarudia tena.
Naomba kuwauliza mlioko kwenye ndoa je tatizo hili ni la wanawake wote au ni mke wangu tu analo? Na je solution yake nini kwani nimetumia uwezo wangu wote kumwelewesha anavyosababisha ugomvi kwenye marriage bado anaonekana kusahau wiki chache baada ya ugomvi? .

tafuta maana ya logname yangu, utapata jibu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
We unataka muishi bila kukwaruzana? kukwaruzana ni sehemu ya ndoa na saa zingine mikwaruzano huwa chachu ya kuzidisha mapenzi yenu
 
kuwa mwanume wa vitendo sometimes inasaidia though si simamii violence kama diplomacy inashindwa use other methods of negotiation kama kumpeleka mbele ya wazee, kwasababu ninaimani amefunzwa kwao
 
Katika kipindi cha miaka 12 ktk ndoa yangu nimegundua tatizo kubwa sana la mke wangu ambalo kwa ufupi ni chanzo kikubwa cha migogoro ktk ndoa yetu. Nimegundua kuwa wife wangu ni vigumu ku keep maagano au makubaliano consistently bila kuvunja. Kwa mfano mnakuta mmekubaliana kwamba tabia au mambo fulani ndani ya ndoa hupendi au yanaleta kero na ugomvi hivyo mke wangu anakubali kabisa kwamba nitaacha sitarudia tena kwani najua nakuudhi" Vivyo hivyo na mimi mume nakubaliana na wife kwamba zile tabia zangu ambazo ni kero kwake nitaacha for good. Huwa nakuwa mwaminifu na nimeacha silika zinazomfanya mke wangu achukie na kukosa amani for her sake.

Mimi nilidhamiria na nimefanikiwa kuacha kabisa vitabia ambavyo ni kero na chanzo cha migogoro na wife kwani sipendi niwe chanzo cha kumfanya wife uncomfortable.

Cha ajabu ni kwamba yeye wife amekuwa na vicious cycle ya kuvunja maagano na maazimio kwa kurudia rudia mambo ambayo ni kero kwangu. Pamoja na kwamba sote ni wasomi kwa level ya Masters inanipa shida kumwelewa ni kwa bahati mbaya au ni kwa makusudi anafanya anapoamua kurudia rudia tabia zinazo nikera. Ukimwuliza kwa nini umevunja makubaliano huwa mbishi na no apology na kuna uwezekano wa escalation ya ugomvi. Hii inanipa shida sana kwani huwa nataka tukikubaliana basi I keep promise kama ninavyomfanyia lakini never.
Uwezo wake wa ku maintain ahadi hauzidi miezi miwili hata kama last time ugomvi ulikuwa mkubwa kiasi gani.

Kinachonishangaza zaidi ni kwamba huyu wife kazini kwake kote alikiofanya kazi anasifiwa kwa kufanya vizuri iwe yuko na bosi mwanamke au mwanaume. Najiuliza kichwa hichohicho kinashindwaje kufanya hivyo hivyo nyumbani kisifiwe na husband?
Huyu wife ni mwepesi wa kukiri kosa na kuomba msamaha ila ndo hivyo anarudia tena.
Naomba kuwauliza mlioko kwenye ndoa je tatizo hili ni la wanawake wote au ni mke wangu tu analo? Na je solution yake nini kwani nimetumia uwezo wangu wote kumwelewesha anavyosababisha ugomvi kwenye marriage bado anaonekana kusahau wiki chache baada ya ugomvi? .

Nimeshukuru kwa sababu umenisaidia kujua kuwa kumbe tuko wengi. Mimi nina zaidi ya miaka kumi kwenye ndoa na mke wangu hana cha masters wala mtoto wa masters. Afadhali wako anaahidi kubadilika na anajitahidi kubadilika kwa muda mfupi (miezi miwili) kisha anarudi kwenye ile vicious cyle. Lakini kizuri nilichokiona kwenye maelezo yako ni kuwa anaomba msamaha kila mara anapojua kuwa amekukosea. Hili ni jambo zuri kwani inaonesha huwa anakumbuka makubaliano yenu na anajua kuwa amekuudhi.

Kuna wengine huwa hata hilo wazo la kubadilika hawataki kukubali na wanachukulia kuwa unadhani kuwa wanaupungufu. Wengine wanafikia kudhani kuwa umepata mwingine huko nje na unataka kumbadili yeye tabia afanane na yule uliyempata huko nje. Na ukianza huo mjadala wa kubadilika ndio unakuwa chanzo cha ugomvi. Nilichogundua baada ya kuwa "philosopher" kwenye ndoa ni kuwa mwanamke huwa yupo kwenye mission ya kumbadilisha mwanaume afanane na tabia anazopenda yeye na wakati huohuo huwa anajitahidi kubakia na tabia zake zilezile. Ukihitaji mifano zaidi nitakumwagia kwani iko mingi tu.

Siamini kama huyo wako huwa anasahau makubaliano mnayofikia ya kubadilika ila nadhani bado yuko kwenye mission. Solution: keep on reminding her every time she breaks your agreements. Usiwe unalundika matukio ya violations halafu baada ya muda unakuja na orodha ya incidences ambazo amevunja makubaliano yenu.
 
Mwana Kwetu, umeandika mengi na umepata michango mingi kutoka kwa wanaJF. Umeona wengi wamekwambia mkeo ni mke mzuri wanatamani wangekuwa naye japo kuwa kwako unaona ana vijitabia vinavyokukela. Cha msingi wewe usilazimishe abadilike gafla kama upendavyo, na wewe pia yawezekana una vitabia vinavyomuuzi lakini havisemi, hivyo kubalance na yeye anapuuziaa yale unayomwambia.Nenda naye taratibu mkuu atabadilika kuwa +ve na endelea kumshirikisha Mungu pia.

Unalalamika kwa hivyo vitabia vidogo na unasema ulishamfukuza kwa tabia ambazo hajaziacha, Mwana kwetu hujapata wanawake pasua kichwa ungemuona huyo wako ni lulu. Nakushauri na wewe uanze kumkubali mkeo kwa mafanikio yake ya kiofisi na hayo mengine anayofanya vizuri hata hapo nyumbani. Anapata credits nyingi kutoka kwa watu wengine (maofisini) lakini kwa mumewe hajakubalika vyema, hiyo siyo sawa. Hebu mkubali na wewe umwonyeshe mkeo kuwa anaweza huone kama hivyo vitabia havitaisha. Ongea naye kwa utaratibu huyo ni mtu mzima mwenzako na mkeo. Mkiwa mmetulia muonyeshe hizo appreciations kwa yale aliyoyafanya vyema. Atajisikia Vizuru na ni rahisi sana yeye kujirekebisha na kuacha hivyo vitabia vinavyo kuudhi. Nakwambia haya kama mwanandoa pia, wake zetu wanapenda na wanafurahi kama tukiwapa compliments pale zinapostahili, ninaitumia hii technique kwa shemeji yako na mambo ni yanaenda vizuri.

Kama kakosea usiwe unawaka sana, upende kumsikiliza na mkiwa kwenye furaha muulize kwa nini kafanya hilo kosa na umwambie ni jinsi gani unavyohuzunishwa na makosa kama hayo aliyofanya. Anapokusimulia mambo ya ofisi kwake uwe unamsilikiliza na hata kama ulikuwa hutaki kusikiliza hizo story. Anakwambia hayo mambo kwa sababu wewe ndiye mume wake na kama anahitaji msaada mpe, kwa kufanya hivyo utashangaa mambo yanavyokwenda vema.

Usipende pia kukumbushia makosa ya nyuma, kama ulimsamehe basi yapite anza chapter mpya na msonge mbele. Ndoa ina changamoto zake kaka hilo halihepukiki na zinatofautiana uzito/ukubwa. Nyie ni watu wawili tofauti japo Mmeunganishwa kuwa mwili mmoja, hivyo kubali kuwa kufikiri kwako na kwake ni tofauti. Hata mapacha wanaofanan pia hutofautiana kitabia sembuse nyie ambao si wa baba/mma mmoja? Vumilia mwana kwetu, hivyo ni vijimambo vidogo tu, mkeo ni mwili wako mkubali alivyo.
 
Mwana kwetu

Huyu mwanamke kwanza umeshamshtaki kwa wazee wake (wazazi) na hata kwa ndugu zako (mama yako) so umeonyesha yeye ni mtu asiyefaa hana uwezo au ni dhaifu... Mtu ukisham-devalue kiasi hicho kw watu wake wote anakosa raha ya maisha

Ushauri:
1. Usipeleke shauri lolote linalohusu ndoa yenu kwa mtu yoyote zaidi ya nyinyi wawili
2. Lower your expectation usitegemee kwamba atafanya mambo makubwa kama unavyotaka
3. Akifanya chochote dogo appreciate sana..na uonyesha kuwa that is more than enough...
4. mwisho: men angalia je wewe unahusika vipi?
 
Mwana Kwetu, umeandika mengi na umepata michango mingi kutoka kwa wanaJF. Umeona wengi wamekwambia mkeo ni mke mzuri wanatamani wangekuwa naye japo kuwa kwako unaona ana vijitabia vinavyokukela. Cha msingi wewe usilazimishe abadilike gafla kama upendavyo, na wewe pia yawezekana una vitabia vinavyomuuzi lakini havisemi, hivyo kubalance na yeye anapuuziaa yale unayomwambia.Nenda naye taratibu mkuu atabadilika kuwa +ve na endelea kumshirikisha Mungu pia.

Unalalamika kwa hivyo vitabia vidogo na unasema ulishamfukuza kwa tabia ambazo hajaziacha, Mwana kwetu hujapata wanawake pasua kichwa ungemuona huyo wako ni lulu. Nakushauri na wewe uanze kumkubali mkeo kwa mafanikio yake ya kiofisi na hayo mengine anayofanya vizuri hata hapo nyumbani. Anapata credits nyingi kutoka kwa watu wengine (maofisini) lakini kwa mumewe hajakubalika vyema, hiyo siyo sawa. Hebu mkubali na wewe umwonyeshe mkeo kuwa anaweza huone kama hivyo vitabia havitaisha. Ongea naye kwa utaratibu huyo ni mtu mzima mwenzako na mkeo. Mkiwa mmetulia muonyeshe hizo appreciations kwa yale aliyoyafanya vyema. Atajisikia Vizuru na ni rahisi sana yeye kujirekebisha na kuacha hivyo vitabia vinavyo kuudhi. Nakwambia haya kama mwanandoa pia, wake zetu wanapenda na wanafurahi kama tukiwapa compliments pale zinapostahili, ninaitumia hii technique kwa shemeji yako na mambo ni yanaenda vizuri.

Kama kakosea usiwe unawaka sana, upende kumsikiliza na mkiwa kwenye furaha muulize kwa nini kafanya hilo kosa na umwambie ni jinsi gani unavyohuzunishwa na makosa kama hayo aliyofanya. Anapokusimulia mambo ya ofisi kwake uwe unamsilikiliza na hata kama ulikuwa hutaki kusikiliza hizo story. Anakwambia hayo mambo kwa sababu wewe ndiye mume wake na kama anahitaji msaada mpe, kwa kufanya hivyo utashangaa mambo yanavyokwenda vema.

Usipende pia kukumbushia makosa ya nyuma, kama ulimsamehe basi yapite anza chapter mpya na msonge mbele. Ndoa ina changamoto zake kaka hilo halihepukiki na zinatofautiana uzito/ukubwa. Nyie ni watu wawili tofauti japo Mmeunganishwa kuwa mwili mmoja, hivyo kubali kuwa kufikiri kwako na kwake ni tofauti. Hata mapacha wanaofanan pia hutofautiana kitabia sembuse nyie ambao si wa baba/mma mmoja? Vumilia mwana kwetu, hivyo ni vijimambo vidogo tu, mkeo ni mwili wako mkubali alivyo.

Ushauri huu ni wa kiutu uzima na unaonyesha ukomavu wa hali ya juu ;mkuu nakushukuru na mawaidha yako na mengine mengi nitayafanyia kazi kwa kina kwani mimi ni msikivu na pia napenda wazo la upande wa pili ndo maana nimelileta hili hapa jamvini nashukuru sana
 
MWANAKWETUUU..."NYOKA HAFUNDISHWI KONAAAA"

Au mara hii umesahau hiyo signature yako uloweka hapo chiniii..umesahau kunako biblia mwanamke alidanganywa na nyoka??...umesahau kuwa nyoka na akili zake bado alimzidi ujanja mwanamke na kumdanganya kitu alichokatazwa na mungu...kula tunda la mti wa katiii???...NAAMINI NIMEKUKUMBUSHA

UMESEMA KUWA MKEO NA WEWE WOTE NI WASOMI WA AT LEAST MASTERS????...

...ILA HAMJASOMEA MASTERS YA KUKUMBUKA NA KUTEKELEZA MAJUKUMU MADOGO MADOGO YANAYOHATARISHA UWEPO WA NDOA YENU NA KUEPUSHA MIKWARUZANOOOO...

OKKK...NIMEKUMBUKAAA...HIYO MASTERZ HAIPO DUNIANI....SOO MNATAKIWA MURUDI SHULE.."UNIVERSITY OF HARDKNOCKS WANAITOA HIYO MASTERS....HATA HAPA TANZANIA IPO"ELIMU MTAANI DOT COM"...HAPO UTAPATA ELIMU ZOOOTE ZISIZOTOLEWA CHUO CHOCHOTE RASMI DUNIANILASTLY...MAHUSIANO NI ZAIDI YA ELIMU ZA CHUO KIKUU..NDIO MAANA MAMA PROF. TIBAIJUKA KUNAKO MAHUSIANO ANACHEMKA MBAYA KULIKO DADA FATMA YULE BINTI WA MZEE KONDO ALIYEACHISHWA SHULE DARSA LA 3 NA KUOLEWA NA MZEE BASHIR KULE PANGANI TANGA....

TAFAKARI....ISHI NA MKEO/WANAWAKE KWA AKILI.
 
google translate imegoma banaa,sikui kama bakita wataweza. dokeza hata mkoa basi yakhe!
<b><span style="font-family: comic sans ms"><font size="4"><font color="#800080">tafuta maana ya logname yangu, utapata jibu</font></font></span></b>
<br />
<br />
 
Nimeshukuru kwa sababu umenisaidia kujua kuwa kumbe tuko wengi. Mimi nina zaidi ya miaka kumi kwenye ndoa na mke wangu hana cha masters wala mtoto wa masters. Afadhali wako anaahidi kubadilika na anajitahidi kubadilika kwa muda mfupi (miezi miwili) kisha anarudi kwenye ile vicious cyle. Lakini kizuri nilichokiona kwenye maelezo yako ni kuwa anaomba msamaha kila mara anapojua kuwa amekukosea. Hili ni jambo zuri kwani inaonesha huwa anakumbuka makubaliano yenu na anajua kuwa amekuudhi.

Kuna wengine huwa hata hilo wazo la kubadilika hawataki kukubali na wanachukulia kuwa unadhani kuwa wanaupungufu. Wengine wanafikia kudhani kuwa umepata mwingine huko nje na unataka kumbadili yeye tabia afanane na yule uliyempata huko nje. Na ukianza huo mjadala wa kubadilika ndio unakuwa chanzo cha ugomvi. Nilichogundua baada ya kuwa "philosopher" kwenye ndoa ni kuwa mwanamke huwa yupo kwenye mission ya kumbadilisha mwanaume afanane na tabia anazopenda yeye na wakati huohuo huwa anajitahidi kubakia na tabia zake zilezile. Ukihitaji mifano zaidi nitakumwagia kwani iko mingi tu.

Siamini kama huyo wako huwa anasahau makubaliano mnayofikia ya kubadilika ila nadhani bado yuko kwenye mission. Solution: keep on reminding her every time she breaks your agreements. Usiwe unalundika matukio ya violations halafu baada ya muda unakuja na orodha ya incidences ambazo amevunja makubaliano yenu.

Mkuu Tata nashukuru umeniongezea experience na pia kunipa strategy ya nini cha kufanya ili nisikwazike. Kusema kwamba wako kwenye mission ni kweli kwani hata rafiki yangu jirani huwa ana experience ya namna hiyo kwenye marriage yake na tunatofautiana handling procedures kwani haziwezi ku work kwa kila ndoa. Mimi kwenye hii thread kutokana na michango yenu najaribu ku derive formula ili nichukulie hizi tabia positive na nijue kutumia udhaifu wa wife kwa manufaa kuliki violence.
 
Mtoa mada kwanza kabisa nashukuru na kukupongeza kwa mada yako ambayo kusema ukweli kwa wengi wetu imetufungua akili kwa kiasi kikubwa. Nafikiri tatizo unalolirefer kwa mkeo au wanawake liko pia kwa wanaume. Kuna wanaume ambao wana tabia kama uliyoisimulia hapo kuwa mkeo anayo. So kwanza nikuweke sawa tu kuwa si wanawake pekee wanaoweza kuwa na tabia kama hiyo bali pia wapo wanaume.

Pili hapo kwenye rangi kidogo sijakuelewa vizuri, umesema ukimwuliza anakuwa mbishi and no apology but at the same time ni mwepesi sana wa kukiri kossa na kuomba msamaha....kidogo inanichanganya.
But all in all kumbuka kuwa kwenye ndoa kuna sacrifaces, kuchukuliana na kuvumiliana. Umeshaujua udhaifu wa mwenzi wako kwa muda mrefu sasa ilikupasa uwe umeshajiadjust katika kuyakubali mapungufu yake na kujitengenezea kaji"bullet proof" kako ili kuepusha migongano ya mara kwa mara na si kumlazimisha au kung'ang'ania mkeo abadilike. Ilimradi hayo mapungufu yake haya'hatarishi' usalama wa afya ya ndoa yenu mfano kama anacheat, unamfumania unamkanya na kisha anarudia, hilo ni kosa nitakuelewa but kama anachelewesha chakula; anachelewa akienda kwa mashoga zake au anapenda sana kwenda saluni- hivyo ni vitu vidogo ambavyo ni kujipanga tu namna ya kumuaccomodate kwani ndo kilema chake but not kumlazimisha abadilike kwa kuwa hutokuwa unamtendea haki kumfanya aishi vile unavyotaka wewe kwa kusacrifice hata vitu ambavyo kwake vinampa furaha and yet they are not that harmful to your marriage.

But kumbuka pia kuwa ukiona kwako kunaungua, basi jua kwa mwingine kunawezakuwa kunateketea kabisa. kila mtu akiweka hapa mapungufu ya spouse wake hapa nadhani tunawezajikuta wanaJF wote tunakutana makanisani kutoa sadaka za kushukuru kwa kuwapata wenzi tulio nao.

AMEN

Babu DC
 
MWANAKWETUUU..."NYOKA HAFUNDISHWI KONAAAA"

Au mara hii umesahau hiyo signature yako uloweka hapo chiniii..umesahau kunako biblia mwanamke alidanganywa na nyoka??...umesahau kuwa nyoka na akili zake bado alimzidi ujanja mwanamke na kumdanganya kitu alichokatazwa na mungu...kula tunda la mti wa katiii???...NAAMINI NIMEKUKUMBUSHA

UMESEMA KUWA MKEO NA WEWE WOTE NI WASOMI WA AT LEAST MASTERS????...

...ILA HAMJASOMEA MASTERS YA KUKUMBUKA NA KUTEKELEZA MAJUKUMU MADOGO MADOGO YANAYOHATARISHA UWEPO WA NDOA YENU NA KUEPUSHA MIKWARUZANOOOO...

OKKK...NIMEKUMBUKAAA...HIYO MASTERZ HAIPO DUNIANI....SOO MNATAKIWA MURUDI SHULE.."UNIVERSITY OF HARDKNOCKS WANAITOA HIYO MASTERS....HATA HAPA TANZANIA IPO"ELIMU MTAANI DOT COM"...HAPO UTAPATA ELIMU ZOOOTE ZISIZOTOLEWA CHUO CHOCHOTE RASMI DUNIANILASTLY...MAHUSIANO NI ZAIDI YA ELIMU ZA CHUO KIKUU..NDIO MAANA MAMA PROF. TIBAIJUKA KUNAKO MAHUSIANO ANACHEMKA MBAYA KULIKO DADA FATMA YULE BINTI WA MZEE KONDO ALIYEACHISHWA SHULE DARSA LA 3 NA KUOLEWA NA MZEE BASHIR KULE PANGANI TANGA....

TAFAKARI....ISHI NA MKEO/WANAWAKE KWA AKILI.

Nakubaliana na wewe 100%
 
Mwongezee asilimia 2 binti wa kazi utaona mabadiliko mara moja.

Inabidi nijipange kwani kumfukuza nitakuwa pia nimetesa watoto wangu ambao obvious hiyo adhabu haiwahusu. Ila pia nitakuwa nafanya tu basi na yeye atakuwa na kazi gani kwani asilimia 98 ya kazi zote anafanya binti wa kazi.
 
Back
Top Bottom