ivonne heslone
New Member
- Aug 5, 2022
- 1
- 0
Matatizo ya afya ya akili ni nini?
Ni matatizo ya ubongo ambayo humfanya mtu kuwa na hisia, fikra, na matendo tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii na kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha. Afya ya akili inaweza kuathiri namna ya kufikiri,na pia inaathiri mfumo mzima wa namna ya kufanya maamuzi. Kila mtu yupo kwenye hatari ya kupata tatizo la afya ya akili kulingana na changamoto mbalimbali za maisha ikiwemo uchumi, kumbukumbu mbaya kutoka utotoni kama unyanyasaji wa kijinsia, wazazi kutengana, kufiwa na wazazi n.k, sababu za kiafya, na matukio mabaya yaliyofuatana katika maisha ya mtu husika. Mara nyingi ni ngumu sana kumtambua mtu mwenye matatizo haya kwa sababu anapokuwa kwenye mkusanyiko wa watu huigiza kuwa sawa,ni mtaalamu au mtu mwenye uelewa juu ya matatizo ya afya ya akili anayeweza kumtambua mtu mwenye tatizo hilo.
Vitendo tishio ni vipi?
Tukizungumzia vitendo tishio ni vitendo ambavyo vinaleta madhara ya moja kwa moja katika taifa ikiwemo uchumi, mazingira ya kijamii kuwa hatarishi nk, vitendo hivyo ni kama ongezeko la matumizi ya madawa ya kulevya, kesi za ubakaji na ulawiti, kesi za mauaji na kesi za kujinyonga. Kati ya mwaka 2021-2022 kumekuwa na ongezeko la watu wanaojitoa uhai (kujinyonga) na kati ya sababu zinazoongoza kutoka kwenye makadirio ya WHO vifo hivyo vinasababishwa na matatizo ya afya ya akili.
Vyanzo vya matatizo ya afya ya akili na madhara yake kwenye jamii,
Hitimisho.
Nini kifanyike?

- Matatizo ya kiuchumi; umaskini na hali ngumu ya maisha ni kati ya vyanzo mbalimbali ambavyo vimekua vikitajwa kama sababu ya watu kujitoa uhai, kama nilivyoelezea awali kwamba matatizo ya afya ya akili yanaathiri mfumo mzima wa kufanya maamuzi hivyo watu wengi hufikia hatua ya kutoa uhai wao wenyewe kwasababu wanakosa msaada,katika kesi iliyotokea mkoani Tabora mnamo tarehe 24.10.2021 kijana wa miaka 18 aliyejinyonga na kutokana na uchunguzi alijitoa uhai kwasababu ya msongo wa mawazo uliosababishwa na hali ngumu ya kimaisha. Lakini pia tatizo la kiuchumi ambalo limekua chanzo kikubwa cha matatizo ya afya ya akili, kwa vijana imeleta madhara makubwa zaidi kwani vijana wamejikuta wakijuhusisha kwenye vitendo hatarishi kama uuzaji wa madawa ya kulevya, wizi ili waweze kupata kipato na kusaidia familia zao na wakati huohuo serikali inawahimiza vijana kujiajiri ikiwa wametoka kwenye familia ambazo hata kupata mtaji ni changamoto na familia hizo hizo waliuza kila kitu kuhakikisha kijana wao anasoma kwa matarajio ya kupata ajira na kuja kuwasaidia baadae, hivyo hali hii ya mategemeo kwa vijana na wazazi inasababisha wote kupata tatizo la afya ya akili na matendo hatarishi kutokea.
- Kumbukumbu za matukio mabaya yaliyotokea utotoni; mnamo tarehe 27.8.2020 Said Juma mwenye umri wa miaka 36 alihukumiwa kutumikia kifungo cha maisha baada ya kumbaka mtoto wa miaka minne “ofisi ya taifa ya mashitaka”. Kwa adhabu kali iliyotolewa kulingana na sheria namba 130(1),(2)(e) na 131(1),(3) na kanuni ya adhabu sura namba 16 ni wazi kwamba mtuhumiwa alipata adhabu stahiki lakini je vipi kuhusu huyu mtoto wa miaka minne aliyebakwa, ni hatua gani zilichukuliwa kumrejesha katika hali yake ya kawaida?, je huyu mtoto atakuwa na akili na mtazamo sawa na yule ambaye hakupitia changamoto hiyo wakati wa utoto wake?. Katika kesi za watoto wanaolawitiwa kama wasipopatiwa tiba sahihi hata katika ukuaji wao kuendelea kukubali kufanyiwa vitendo hivyo na mpaka kufikia hatua ya kuzoea na kuona ni jambo la kawaida na pia ni rahisi kuwafanyia wengine wanapokua watu wazima kwa sababu hukua na mtazamo hasi juu ya binadamu wenzao na kukosa hisia ya huruma ndani yao. Hivyo serikali inashughulika zaidi na matokeo ya matatizo ya afya ya akili na kuacha shina ambalo baada ya muda huchipua na kesi za ubakaji na ulawiti kuongezeka.
- Changamoto za mahusiano; mahusiano yamekua chanzo cha maumivu kwa baadhi ya watu na kupelekea kushindwa kuzuia hisia za mihemko na kujikuta wakihatarisha maisha yao wenyewe au ya watu wanaowapenda, mfululizo wa matukio ya usaliti kwa mtu yanaweza kupelekea kesi kama kuwatoa uhai watu ambao wapo nao kwenye mahusiano kwa muda huo pale hali ya usaliti inapojirudia mfano katika kesi iliyotokea jijini Mwanza mnamo mwaka 2022 mme kumpiga risasi mke wake. Haya ni baadhi ya matokeo ya matatizo ya afya ya akili yatokanayo na changamoto za mahusiano kwasababu watu hawa wanapopata mfululizo wa matukio mabaya katika mahusiano hawapati msaada na mara nyingi hujiona wako sawa kwasababu jamii haina elimu juu ya dalili za matatizo ya afya ya akili.
Hitimisho.
Nini kifanyike?
- Katika vituo vya afya mjini na vijijini kuwepo kitengo cha afya ya akili (urahisi katika upatikanaji wa huduma), kuanzisha programu mbalimbali za kufundisha na kuelimisha kuhusu afya ya akili (uelewa kwa jamii kuhusu tatizo),kufanya uchunguzi wa mbinu mpya zitakazo saidia kupambana na tatizo hilo (kutibu tatizo), kozi ya saikolojia kupewa kipaumbele na kuongeza nafasi za ajira (ongezeko la watoa huduma), kutoa ushirikiano wa kutosha kwa taasisi binafsi zinazojishughulisha na utoaji elimu wa afya ya akili (ushirikishaji kwa taasisi zenye ujuzi).
- Pia kwa vyombo vya habari ni muhimu kutengeneza matangazo mbalimbali kwa ajili ya kuelimisha watu ili huduma za afya ya akili zitakapoanzishwa watu wawe na uelewa na utayari wa kwenda.
Upvote
0