Ibun Mallik
Member
- Dec 18, 2017
- 41
- 11
SABABU ZA TATIZO LA AJIRA KWA WASOMI, MADHARA NA UFUMBUZI WAKE TANZANIA.
Utangulizi
Tatizo la ajira kwa wasomi ni janga la dunia mzima lakini limeathiri zaidi katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Tatizo hili linahusisha kuwa na idadi kubwa ya watu wenye ujuzi, maarifa na uwezi mzuri waliohitimu kutoka vyuo mbalimbali kubaki au kukaa bila ajira. Japo kuwa serikali na jamii ikiwemo wazazi wa meekeza kwa kiasi kikubwa cha fedha kwa wasomi hao.
SABABU ZA TATIZO LA AJIRA KWA WASOMI.
ASILI YA MTAALA WA ELIMU ULIOPO.
Kuwepo kwa changamoto za malalamiko mengi juu ya mtaala wa elimu unaofuatwa katika mfumo wa elimu wa Tanzania. Wadau mbalimbali na waajiri wa wasomi hao walikilalamika kuwa wataalamu wanaozalishwa hawakidhi mahitaji ya sekta husika. Mtaala wa elimu ulipo unawanyima wanafunzi kupata ujuzi wa kile anachokisomea na badala yake kukalili maandiko mbalimbali yasiompa ujuzi. Hivyo kupekekea wasomi hao kutoka vyuo mbalimbali kukosa sifa za kuajiriwa.
KUWEPO KWA IDADI KUBWA YA WASOMI KULINGANISHA NA MAHITAJI YALIYOPO.
Kutokana na maendeleo makubwa yaliyopatikana katika sekta ya elimu Tanzania kuanzia mwaka 2005, yamepelekea kuzalisha idadi kubwa ya wasomi kulinganisha na mahitaji yaliyopo. Mfano mzuri ililipotiwa na waziri wa TAMISEMI mwezi wa 5 tarehe 25 mwaka 2021 kuwa kalibia wahitimu wa ualimu laki moja wameomba nafasi elfu sita za walimu zilizotangazwa tarehe 9 mwezi wa 5 mwaka 2021. Kutokana na hilo hupelekea wahitimu wengi kukosa nafasi za ajira kutokana kuzidi mahitaji ya nafasi zilizopo kwa zaidi ya mara mbili.
KUTOWEPO KWA MAZINGIRA RAFIKI KWA UANZISHAJI WA BIASHARA BINAFSI.
Wahitimu kutoka vyuo mbalimbali wamekuwa wakijalibu kuanzisha biashara ndogo ndogo mbalimbali maarafu hujilikana kama machinga lakini kumewepo na mazingira yasio rafiki kwa wajasiliamali hao na kukata tamaa ya kuendelea. Mfano mzuri viongozi wakuu wa nchi mara kwa mara hulalamikia suala hili kwa watendaji wa mamlaka husika kwa kutotendewa sawa kwa wajasiriamali hao, ikiwemo kauli ya Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassani wakati wa mazungumzo na vijana mkoani mwanza, juu ya kuondolewa kwa machinga mkoani morogoro.
KUKOSEKANA KWA USHAURI MZURI KWA WANAFUNZI WAKATI WA MACHAGUZI YA KOZI ZA KUSOMEA.
Idadi kubwa ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kujiunga na vyuo vikuu ama kidato cha nne na kujiunga na vyuo vya kati wanakosa ushauri juu ya kozi za kusomea katika ngazi hizo za elimu ya juu. Idadi kubwa ya wanafunzi hufanya maamuzi wakati wapo katika vituo vya kufanya maombi na kushauri na wahudumu wa vituo hivyo. Kwa mfano kumewepo na tabia ya kuchagua kozi ambazo zimepewa kipaumbele katika mkopo maarufu kama "BOOM" badala ya kuangalia soko na mahitaji.
MTAZAMO MBAYA KWA WAHITIMU JUU YA NAFASI NYINGINE ZA AJIRA.
Wahitimu wana mtazamo mbaya juu ya nafasi zengine za ajira mbali na kile alichokisomea. Hili limekuwa janga kubwa kwa wahitimu wa Sasa Tanzania, mara nyingi wazazi wa wahitimu hawa wamekuwa wakisikika kuwa wasomi wao hawataki kujishirikisha katika fursa na nafasi mbalimbali zinazojitokeza na kutafutiwa na walezi ama wazazi wao. Hivyo basi kufanya wahitimu wao kubaki bila ajira.
MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA NA MASHARTI YA WAAJIRI.
Kwa kiasi kikubwa kumekuwa na changamoto ya aina ya wataalamu wanaozalishwa na hitaji la soko la ajira, hili huchangiwa na mtaala wa elimu ulipo na masharti ya waajiri wenyewe. Waajiri wengi wamekuwa na masharti magumu wanayowafanya wahitimu wengi kukosa nafasi zinazotangazwa. Kwa mfano asilimia kubwa ya matangazo ya ajira yanayotoka yanahitaji wataalamu wenye uzoefu wa muda mrefu, na kwa uhalisia wahitimu wao wanatoka mashuleni moja kwa moja kwenda vyuoni hukosa sifa hizo.
MADHARA TATIZO HILI LISIPO TATULIWA.
Tatizo lolote huja na madhara yake, tatizo la ajira kwa wasomi pia lina madhara mengi sana ikiwemo:-
SERIKALI HUPOTEZA RASILIMALI NYINGI.
Serikali ya Tanzania inaghalamikia elimu pasipo na malipo ya ada tangu mwaka 2015 kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari kama elimu ya lazima kwa kila mtoto wa kitanzania. Pia hutoa mikopo kwa elimu wa ngazi ya juu ili kusaidia watoto wa kimasikini wasio na uwezo wa kijisomesha. Wanafunzi hao ndio wanakuwa wahitimu ama wasomi ambao hawana ajira. Hii hupelekea hasara kwa taifa.
KUONGEZEKA KWA UHALIFU.
Kutoka na watu kuwa na uwezo na maarifa mbalimbali wanaweza kuyatumia maarifa na uwezo wao kwenye masuala mbalimbali ya kihuni na uhalifu. Kwa mfano serikali siku za kalibu kupitia wizara ya mawasiliano imekuwa ikidai kuwa kuna wizi wa mtandao uliokidhili na wajaasiliamali wengi kwenye sekta husika wanaibiwa na waalifu hao.
WASOMI WENGI KWENDA NJE YA NCHI (BRAIN DRAIN).
Hili pia huweza kutokea, endapo wasomi wengi kutoka vyuo vikuu na vyuo vya kati kukosa nafasi za ajira wanaweza kutanua mawazo yao hata kutafuta nafasi hizo nje ya nchi ili kuweza kunufaika na elimu yao. Kufanyika kwa hilo litadhoofisha uchumi wa nchi kwa kunufaisha mataifa ya nchi kwa wataalamu waliosomeshwa kwa pesa na rasilimali mengine za Tanzania.
KUONGEZEKA KWA UMASIKINI KATIKA JAMII.
Mbali na serikali kihudumia elimu pia jamii ikiwemo wazazi hutoa kiasi kikubwa cha pesa na Mali zao zengine ili kuwezesha watoto wao kusoma. Endapo wahitimu wao hukaa bila ya kurudisha kile kilichotalajiwa na jamii hupelekea umasiki kwa familia wa wahitimu wao. Kwa mfano asilimia 80 ya watanzania ni watoto wa wakulima na wafugaji, hivyo rasilimali nyingi hupotea.
UFUMBUZI WA TATIZO LA AJIRA KWA WAHITIMU TANZANIA.
Zipo njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika na kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la kutokuwa na ajira kwa wasomi. Njia hizo ni pamoja na:-
KUTOLEWA KWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAFUNZI.
Kutokana na kuwepo kwa janga la ajira kwa wasomi, serekali kupitia wizara husika wanaweza kuboresha mtaala wa elimu kwa kufundisha kwa somo la ujasiriamali kuanzia ngazi ya sekondari hadi vyuoni kama somo la lazima. Kufanya hivyo kutawezesha wahitimu kuwa na ujuzi wa namna ya pekee juu ya utafutaji wa fursa katika mazingira mbalimbali kabla au baada ya kumaliza masomo yao.
KUPEWA USHAURI MZURI KWA WANAFUNZI JUU YA KOZI ZA KUSOMEA KABLA YA KUJIUNGA NA VYUO.
Ushauri ni jambo linalo hitajika kila sehemu na hatua ya maisha, kupewa ushauri wa wanafunzi juu ya kozi za kujisomea kulinganisha na mahitaji ya soko la ajira ni jambo zuri na lisaidia kupunguza janga hili. Ushauri huo ikiwemo aina ya wataalamu wanaohitajika zaidi katika sekta mbalimbali. Kwa mfano wataalamu wa teknolojia ya habari sasa wanaohitajika zaidi kutokana na dunia kuhamia katika ulimwengu wa kidigitali.
KUWEPO KWA MAZUNGUMZO YA PAMOJA KATI YA VYUO NA WAAJIRI.
Ili kuzalisha wataalamu wenye sifa na ujuzi wenye kuhiitajika na waajiri, watumishi na viongozi wa vyuo wanapaswa kuzungumza na waajiri kupata maoni yao juu ya aina gani ya wahitimu ama wataalamu wanaohitajika ili kwenda kuboresha mitaala ya kusomesha wanafunzi wao. Kwa mfano wapo baadhi ya waajiri wanaodai kuwa wahitimu wengi wa ngazi za juu za elimu wamekuwa na mchango mdogo katika maendeleo ukilinganisha na wale waliochini kielimu.
KUBORESHWA KWA MTAALA WA ELIMU NA UENDESHAJI WAKE.
Serekali kupitia mamlaka na wizara husika inapaswa kuboresha mtaala wa elimu na ufundishaji. Malalamiko mengi wa wadau mbalimbali wa elimu na wasio wa elimu yaonesha mbali na kuwa na mtaala wa zamani wa elimu lakini pia ufundishaji mbovu unaogemea zaidi kwenye ufanyaji wa mitihani katika kalatasi badala ya kuhusisha vitendo kwa wingi katika mazingira halisi mbali na darasani.

Upvote
3