Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema tumshukuru sana Rais Samia Suluhu kwasababu alipoingia madarakani aliamua kwanza kufungua fursa za ajira nchi nzima alitoa vibali vya ajira zaidi ya elfu 55 nchi nzima.
Lakini pia aliongezea kuwa “Mwezi wa pili mwaka huu tunatarajia kuchukua watu 1,769 kutoka kwenye database [kanzidata] na kuondoa ile ya kuwarudisha rudisha kuja kufanya interview [usaili] wakati wameshafaulu. Kazi yetu itakuwa kuwachukua na kuwapangia majukumu mbalimbali.”
Tatizo la ajira linaendelea kutatuliwa vijana tusiwe na wasiwasi Rais Samia Suluhu anahakikisha tatizo hili linaisha kabisa kama usipoajiriwa na serikali anaweka mazingira wezeshi ya kujiajiri.
Huyu huyu mama enzi za Jiwe ndio alikuwa anasifu sera za kutoajiri na kusema wafanyakazi wameongezewa mshahara kwa kujengewa miundo mbinu na kwa kununuliwa ndege 11 kwa mpigo!
Leo tena ana msifu mama Samia kwa kufungua nchi na kukuza ajira za kuajiriwa na kuboresha mishahara
Anyway ngoja niende zangu kijiweni nikajichezee draft tu mimi