Tatizo la ajira lingetangazwa kama janga tu , inawezekanaje ajira 14648 za walimu ziombwe na watu zaidi ya laki mbili

Tatizo la ajira lingetangazwa kama janga tu , inawezekanaje ajira 14648 za walimu ziombwe na watu zaidi ya laki mbili

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Nimeshituka sana tangu Jana kuaona ajira za walimu na idadi ya walioomba , kumbuka anayesoma ualimu ni either 1. Mtoto wa maskini 2. Uwezo mdogo shuleni 3. Kama hayo mawili hayapo Basi alikumbwa na matatizo flani kwenye maisha, mimi ni mwalimu ualimu hauwezi kuwa kimbilio , hii idadi ya waliojitokeza inashitua sana na inatosha kuwa salamu kuwa maskini wameongeza kasi ya kuzaa sana hivo serikali ijipange kudhibiti huu mfumuko wa watu wasiokuwa na ajira hivyo ili kudhibiti haya itangaze tu kama ajira ni janga ili mbinu muafaka za kupambana na tatizo zianze kuchukuliwa
 
Enzi za mkapa na kikwete ajira ya ualimu ilikuwa njenje, div 4 point 27 unakwenda kusomea ualimu miezi nane tu unapangiwa shule matokeo ya mtihani yatakukuta huko umeshazoea kazi. Iliitwa jina la utani voda fasta, yaani walimu wa voda fasta. Shule nyingi hususani za vijijini hazikuwa na walimu wengi, nafasi zilikuwa nyingi mpaka za kujitolea, ukijitolea unapata ajira humohumo halmashauri, tena ajira ya kudumu. Lakini siku hizi wahitimu wa ualimu ni wengi na nafasi ni chache, wengine hukaa mitaani muda mrefu mpaka wanajianzishia shughuli zingine, wanachoka kusubiri ajira na umri unasonga
 
Back
Top Bottom