Enzi za mkapa na kikwete ajira ya ualimu ilikuwa njenje, div 4 point 27 unakwenda kusomea ualimu miezi nane tu unapangiwa shule matokeo ya mtihani yatakukuta huko umeshazoea kazi. Iliitwa jina la utani voda fasta, yaani walimu wa voda fasta. Shule nyingi hususani za vijijini hazikuwa na walimu wengi, nafasi zilikuwa nyingi mpaka za kujitolea, ukijitolea unapata ajira humohumo halmashauri, tena ajira ya kudumu. Lakini siku hizi wahitimu wa ualimu ni wengi na nafasi ni chache, wengine hukaa mitaani muda mrefu mpaka wanajianzishia shughuli zingine, wanachoka kusubiri ajira na umri unasonga