Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Fikra ni namna mtu anavyochukulia jambo fulani, fikra ni mawazo ya mtu juu ya kitu fulani katika maisha kwa ujumla wake, mara nyingi kabla ya kumshauri mtu, tunaanza na fikra, start with mindset, fikra ni dhana, fikra, umasikini na utajiri vinaenda sambamba,lakini tujiulize nini chanzo cha fikra,kwa tuliopita seminary za Cuba, tumesoma tabia nne za watu,sanguine, melancholic, choleric na phlegmatic,kama haitoshi tulisoma vitu vingine vitatu hulka, saikolojia na mazingira, hivi vyote vinaweza kukusaidia kuishi kokote na kuweza kuchunga kondoo wa Bwana, lakini pia vitu hivyo ndio chanzo cha fikra kwa binadamu yeyote zitakazokupeleka kwenye ubunifu na kuwa tajiri au masikini.
Hivi leo kila kijana ni chawa kwa bosi wake,maana hakuna namna nyingine zaidi ya kuwa chawa ili usile nyasi,wakati wewe unaangaika kukusanya mchele mikoa yote ya Tanzania ili uuze Umoja wa mataifa upate angalau dollar laki mbili,kuna chawa mmoja yeye yupo kwenye bus anasema dhambi zote za bosi wake apewe yeye,na digrii yake akili yake ndio imeishia hapo,hili ni tokeo la elimu iliyokosa fikra bunifu,Leo kila kijana ni mwanasiasa maana ndio fursa pekee ilipo,kila kijana kachukua form kugombea ujumbe wa halmashauri kuu,wengine uenyekiti wa vijana taifa,tena wanajitanabaisha mimi injinia nichagueni nimetoka kijijini, mwingine anasema tumchague sababu yeye yatima,awa wote wana machawa kwenye mtandao wanawapigia kampeni,jana kuna chawa kanipa cv yake nimsaidie kutafuta kazi, nikamwambia andika proposal hii kuomba dollar 50,000 kwa ajili ya kilimo,akanijibu yupo busy sana na Uchaguzi anagombea uenyekiti wa vijana,uvinini sijui,
Vijana awa hata ufanyaje hawana mpango wala mkakati wa ubunifu,wameridhika kuwa machawa kwenye siasa na kuwa machawa makazini,wale machawa wakazini wao ni sawa na wale "house nigger" awa ma house nigger kule Marekani ukimwambia bosi wako anakutesa anaenda kusema kwa bosi wake,mali ya bosi ikipotea yeye analia zaidi ya bosi,huyu ana digrii mbili lakini bosi wake akimwambia nenda kapigane anaenda kupigana,hili ni tokeo la elimu iliyokosa fikra bunifu,injini ya utajiri na mafanikio ni ubunifu,ubunifu ndio ujasiriamali wenyewe, ubunifu unaunda na kuzalisha mawazo ambayo ndio njia ya kutatua matatizo, ubunifu ndio huduma mpya zinazoweza kuingiza kipato,China walipata bahati ya kuwa na Marais wenye akili za ubunifu Mao Zedong,Deng Xiaoping Marais awa walikuwa na fikra bunifu za asili,
China tuionayo leo mambo yote mazuri yalianzia kwenye mifumo yao ya elimu yenye fikra za ubunifu,ni kama ilivyo Veta lakini elimu hiyo ilihusisha kila mchina kupata elimu ya ubunifu baada ya kufanikiwa kwenye hili la ubunifu,Rais Deng Xiaoping alikuja na mfumo wa wazawa kupata mitaji kupitia mabenki china,walianza na mikopo midogo midogo na baadae mikopo mikubwa na sekta ya ubunifu ikakua, Ubunifu wa Wachina ulisababisha China kuanza kutengeneza vitu vya teknolojia ya juu sana na bora watakupa ubora sawa na mahitaji yako,kwa sasa China imechukua teknolojia zote bora duniani kwa asilimia mia na inaweza kuzichezea kwa ubunifu na zikatoa kitu kingine kipya duniani,Huawei moja ya kampuni bora za mitambo ya simu na vifaa vyake, ukiacha huawei anafatia kwa mbalii na akina Siemens na Nokia,
Hisense ni moja ya kampuni zinazotengeneza electronics ikiwepo tv tena kwa kutumia cheap za kichina na inamilikiwa na Serikali ya China,Fikra za ubunifu zimepelekea China kuwa na licence ya kutengeneza Samsung,iphone na brand nyingine nyingi ndio maana hata kutengeneza Hisense,Mchina hajapata shida sababu technology ya tv ameipata kupitia Samsung, sony nk.kuna kipindi ubunifu wa Mchina ulimpa fikra ya kuwekeza sana kwenye soka,China ilitaka kutengeneza league ya kuvutia kama ilivyo ya Uingereza,fikra hii inaonyesha Mchina halali wala hapoi,wakati sisi tukibuni namna ya kuwa chawa wa kiwango cha juu,Mchina anawaza suala la brands zake kuteka soko la dunia, Mchina anaweka low cost of production ikilinganishwa na nchi nyingine ukiacha india,dunia iliyobaki yote imeamua kwenda China kuoutsource manufacturing kutokana na fikra za kibunifu zenye Automation.
Tanzania inahitaji kuwa na mfumo wa elimu wenye fikra za ubunifu kujikita kwenye kubuni bidhaa mpya kisha bidhaa iliyobuniwa inaenda kutatua tatizo moja kwa moja mfano simu janja nafuu mfano ya laki moja au elfu hamsini itatatua mawasiliano,mashine za kutengeneza juice hili litatatua suala lishe duni kwa maana njaa na lishe duni nazo zinaathiri mfumo wa fikra bunifu,ubunifu wa nguo,vyombo,sabuni na viatu,Ubunifu unarahisisha kazi kupitia uundwaji wa njia mbadala za utekelezaji wa majukumu ya kila siku mfano teknolojia ya mawasiliano, utunzaji taarifa, mtiririko wa majukumu,mifumo ya afya,na mifumo ya elimu,
Kwa taifa ubunifu ndio unaopelekea uwepo wa biashara na biashara italeta kodi na ushuru kwa Serikali na upatikanaji wa ajira ni matunda ya moja kwa moja ya elimu yenye fikra ya ubunifu kwa taifa la Tanzania,lipo pia suala la kisaikolojia kwa maana ya utimamu wa akili,hapa kuna kitu kinaitwa vicious cycle of poverty,mtu toka azaliwe hajawahi kua na nafuu ya maisha; hii inamfanya aathirike kifikra inampotezea kujiamini katika kufikiri,na kuwasilisha mawazo yake,matokeo ya mwisho ya hili ni kuharibika kwa uwezo wa kujifunza na mwishowe ufikiri wa mtanzania unakuwa umeharibika hawezi kufanya chochote cha tofauti katika kufikiri na kubuni,hawezi kufikiri kuwa ubunifu utampa ajira bila mtaji,ubunifu utampa pesa ya matumizi kisha utajiri wa hali ya juu mfano utajiri wa Mark na Facebook na wengine wengi.
Nimalizie na yafuatayo kwa manufaa ya Mtanzania,Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka,mazingira ndio chakula,elimu na vitendea kazi,vijana wengi wa Tanzania wamezungukwa na mazingira mengi magumu yakiwemo miundombinu mibovu,ambayo huathiri harakati za kujikwamua katika nyanja za usafirishaji,mawasiliano, na technolojia,ubovu wa miundombinu inaathiri moja kwa moja fikra za ubunifu kupitia kuongezeka kwa gharama za usafirishaji,familia nayo inahusika hasa wazazi ambao ni waalimu wa kwanza kwa mtoto au kijana yeyote,malezi ya mzazi yana nafasi ya kumjenga au kumbomoa,wazazi ndio wanaomfanya kijana awe na uwezo wa kujiamini,kwa kumfundindisha maadili,bidii na uwezo wa kufanya yanayofaa katika kujihudumia na kuihudumia jamii,
Mwisho kabisa ni elimu; hili ndilo eneo muhimu katika malezi na makuzi ya kijana au mtoto, hapa kijana anajifunza mahusiano na watu, kile anachotarajia kufanyia kazi na maarifa mapya kupitia historia au mifano iliyo hai,na mwisho kabisa ni utawala,hili ndilo eneo linalobeba familia na jamii,serikali ndio kichocheo cha kukuza au kudumaza vijana na watu wake kupitia sera na miongozo yake katika jamii,PLO Lumumba akasema
"Tatizo letu waafrika ni kwamba, wenye maono na mawazo hawana madaraka,wakati wenye madaraka hawana maono wala mawazo" nami naongezea mwenye pesa hana mawazo na mwenye wazo hana pesa,je tuuze wazo kwa mwenye pesa au tumpe pesa mwenye wazo? hapana,mwenye wazo bila pesa,ana uwezekano mkubwa wa kupata pesa kwa mawazo yake,kizungumkuti ni kwa mwenye pesa bila wazo,pesa zake lazima zimuishie hewani.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;-
-Assessment on the effects of Micro-Financing on poverty Reduction.