Ngoja niichaji simu yangu nitarudi hapa.. Lakini mpaka Kiba kuja kufika level za Naseeb basi mwanangu christine atakuwa ndio anamaliza A level. Ukweli usemwe hata kama unaumiza, hata Tuzo anazowaniaga huwa anabebwa tu lakini hakuna hata wimbo wake wowote wenye uwezo wa kuchezwa Africa mashariki na kati. Huwezi Kuulinganisha my no moja na kimasomaso au nagharamia na Utanipenda. Kiba bado ni Kichuguu na Diamond ni mlima kilimanjaro
Kuna shehe mmoja wa Morogoro anaitwa Mohamed Idd (Abuu Idd) huwa anaandika makala katika gazeti la Mwananchi. Aliwahi kuandika hivi:
"Kuna namna mbili za kuonekana mzuri kwa bosi wako ili akupende wewe kuliko wengine, ya kwanza ni kufanya kazi kwa bidii na weledi wako wote automatically bosi atakupenda tu. Ya pili ni kujipendekeza sana kwa bosi na kupeleka peleka umbeya umbeya ili wengine waonekane wahovyo na wewe upendwe."
Anachokifanya Kiba ni kutumia hiyo njia ya pili, kumponda Diamond ili yeye aonekane ni bora zaidi badala ya kufanya kazi nzuri watu wakampenda. Kama kweli yeye ni bora apige kazi watu aone.
Kuna mtu anaitwa nifah yeye anadai kuna tofauti kati ya kuimba mziki mzuri na kuwa maarufu. Kama alikuwa hajui, ni kwamba hivyo vinaenda sambamba. Kuna wanamuziki wengi Nigeria kuliko Tanzani kwa mfano, lakini hatuwajui kutokana na kigezo hicho cha kazi zao ni very local. Ukiimba vizuri utatoboa tu, we mwenyewe si unamuona Vee Money, Navy Kenzo (Nah reel na shem wetu).
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.