Tatizo la baadhi ya Wahadhiri kuomba rushwa ya ngono. Je, suluhisho ni nini?

Tatizo la baadhi ya Wahadhiri kuomba rushwa ya ngono. Je, suluhisho ni nini?

Joe Miles

New Member
Joined
May 8, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Habari zenu wana JamiiForums

Naomba kuuliza ama kutoa dukuduku; hivi kwanini baadhi ya Wahadhiri wa vyuo haswa Wahadhiri wa kiume wanakuwaga na tabia ya kuwadhalilisha wanachuo wa kike kingono sana, tena haswa linapokuja suala la mitihani na kutafuta courseworks

Unakuta msichana/mwanamke amefanya kazi vizuri ila tu anafelishwa kimakusudi na ili apite/kufaulu anaombwa atoe rushwa ya ngono kwa mwalimu na akikataa ndo anakomolewa kwa kufelishwa au kupewa kazi ngumu sana na kufanyiwa visa ili tu aone chuo kichungu

Akubali kutoa rushwa ya ngono ama akate tamaa aache chuo kama bado anakuwa na msimamo wake wa kujiheshimu?
 
Back
Top Bottom