Tatizo la CHADEMA ni kukosa wazee wa ushauri ndiyo matokeo ya kinachoendelea sasa

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
TATIZO LA CHADEMA NI KUKOSA WAZEE WA USHAURI NDIO MATOKEO YA KINACHOENDELEA.

Utakubaliana na mimi kwamba chama kikubwa cha siasa aina ya Chadema ambacho uhai wake ni zaidi ya miaka 30 kukosa wazee wa Ushauri ni aibu na ndio matokeo ya minyukano inayoendelea kipindi hiki cha Uchaguzi wa wao wa ndani ya chama.

๐๐ข ๐ข๐ฆ๐š๐ง๐ข ๐ฒ๐š๐ง๐ ๐ฎ ๐ค๐š๐›๐ข๐ฌ๐š ๐ค๐ฎ๐ง๐ ๐ž๐ค๐ฎ๐š ๐ง๐š ๐ฐ๐š๐ณ๐ž๐ž ๐ฐ๐š ๐๐ฎ๐ฌ๐š๐ซ๐š ๐ง๐๐š๐ง๐ข ๐ฒ๐š ๐‚๐ก๐š๐ฆ๐š ๐ฐ๐š๐ง๐ ๐ž๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐ฐ๐š๐ข๐ญ๐š ๐Œ๐›๐จ๐ฐ๐ž ๐ง๐š ๐‹๐ข๐ฌ๐ฌ๐ฎ ๐ฆ๐จ๐ฃ๐š ๐š๐ค๐ฎ๐›๐š๐ฅ๐ข ๐ค๐ฎ๐ญ๐จ๐ ๐จ๐ฆ๐›๐ž๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐ฆ๐š๐ฌ๐ฅ๐š๐ก๐ข ๐ฆ๐š๐ฉ๐š๐ง๐š ๐ฒ๐š ๐‚๐ก๐š๐ฆ๐š. ๐๐ฎ๐ฌ๐š๐ซ๐š ๐ณ๐š๐ข๐๐ข ๐Œ๐›๐จ๐ฐ๐ž ๐ค๐ฐ๐š ๐”๐ฆ๐ซ๐ข ๐ฐ๐š๐ค๐ž ๐ง๐š ๐ฆ๐ฎ๐๐š ๐ฐ๐š ๐ฆ๐ข๐š๐ค๐š 22 ๐š๐ฅ๐ข๐จ๐ค๐ข๐จ๐ง๐ ๐จ๐ณ๐š ๐‚๐ก๐š๐ฆ๐š ๐š๐ง๐ ๐จ๐ฆ๐›๐ฐ๐š ๐š๐ค๐ฎ๐›๐š๐ฅ๐ข ๐ค๐ฎ๐ค๐š๐š ๐ฉ๐ž๐ฆ๐›๐ž๐ง๐ข ๐ข๐ฅ๐ข ๐š๐ฆ๐ฐ๐š๐œ๐ก๐ข๐ž ๐‹๐ข๐ฌ๐ฌ๐ฎ. ๐๐ข ๐๐ก๐š๐ก๐ข๐ซ๐ข ๐ก๐š๐ฒ๐š ๐ฒ๐š๐ง๐š๐ฒ๐จ๐ž๐ง๐๐ž๐ฅ๐ž๐š ๐ง๐ข ๐ค๐ฐ๐š ๐ฌ๐š๐›๐š๐›๐ฎ ๐ฒ๐š ๐ค๐ฎ๐ค๐จ๐ฌ๐š ๐ฐ๐š๐ญ๐ฎ ๐ฐ๐š ๐ค๐ฎ๐ฐ๐š๐ฐ๐ž๐ค๐š ๐ฉ๐š๐ฆ๐จ๐ฃ๐š ๐ก๐š๐ฐ๐š ๐ฆ๐š๐ก๐š๐ฌ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐ฐ๐š๐ฐ๐ข๐ฅ๐ข. ๐Œ๐ข๐ง๐ฒ๐ฎ๐ค๐š๐ง๐จ ๐ก๐ข๐ข ๐ก๐š๐ข๐ง๐š ๐š๐Ÿ๐ฒ๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐‚๐ก๐š๐ฆ๐š ๐ง๐š ๐ง๐ข ๐ค๐ฎ๐ฆ๐ฌ๐š๐Ÿ๐ข๐ฌ๐ก๐ข๐š ๐ง๐ฃ๐ข๐š ๐Œ๐š๐ฆ๐š ๐’๐š๐ฆ๐ข๐š 2025 ๐ง๐๐ข๐จ ๐ฆ๐š๐š๐ง๐š ๐ค๐ฎ๐ง๐š ๐ฎ๐ฐ๐ž๐ณ๐ž๐ค๐š๐ง๐จ ๐ƒ๐จ๐ฅ๐ฅ๐š ๐ค๐ฎ๐ฉ๐ข๐ญ๐ข๐š "๐€๐›๐๐ฎ๐ฅ" ๐ง๐๐ข๐จ ๐ค๐š๐ณ๐ข ๐ฐ๐š๐ง๐š๐ฒ๐จ๐ข๐Ÿ๐š๐ง๐ฒ๐š ๐ง๐š ๐ฐ๐š๐ง๐š๐ž๐ฅ๐ž๐ค๐ž๐š ๐ค๐ฎ๐Ÿ๐š๐ง๐ข๐ค๐ข๐ฐ๐š. ๐Š๐ฎ๐ญ๐จ๐ค๐ฎ๐ฐ๐ž๐ฉ๐จ ๐ค๐ฐ๐š ๐–๐š๐ณ๐ž๐ž ๐ฐ๐š ๐”๐ฌ๐ก๐š๐ฎ๐ซ๐ข ๐ง๐ข ๐”๐๐ก๐š๐ข๐Ÿ๐ฎ ๐ฐ๐š ๐Œ๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž๐ค๐ข๐ญ๐ข ๐š๐ฆ๐›๐š๐ฒ๐ž ๐ง๐๐ข๐ฒ๐ž ๐ค๐ข๐จ๐ง๐ ๐จ๐ณ๐ข ๐ฆ๐ค๐ฎ๐ฎ ๐ฐ๐š ๐‚๐ก๐š๐ฆ๐š.

Amesikika Mhe Lissu akisema kwamba Uchaguzi mkuu wa chama taifa husimamiwa na wazee wa chama. Amesema hajui hata wazee wa Chama ni kina nani maana huko nyuma wazee wa Chama walikua kina Mzee Mtei, Mzee Bob Makani, Ndesamburo, Mzee Arcado Ntagazwa,Profesa Baregu, Profesa Safari nk. Lakini gawa Wazee hawa hawapo kwenye Chama kwa sasa. Kama Makamu Mwenyekiti wa Chama anasema hawajui wazee wa Cham, hivi hali ikoje? Bado tunaona tu Mbowe anastahili kuendelea kukiongoza CHADEMA kwa madhaifu kama haya kweli?

Mbowe alikua na uwezo wa kutafuta hata wazee wa chama kutoka wastaafu wa Chama katika ngazi za kanda na mikoa. Siyo lazima wawe wa ngazi ya taifa. Pia hii ya kukosa wazee wa chama ngazi ya taifa ni kwa sababu ya kukaa madarakani kwa muda mrefu, miaka 20 kungekua hata na wazee 2 wa nyadhifa za uenyekiti. Makatibu wakuu na manaibu wastaafu.

Hata BAZECHA pia inaweza kutoa wazee wa ushauri wangewakalisha hawa watu kukinusuru chama.

Honestly, tukienda kwenye uhalisia wa upepo wa ndani na nje ya Chama, Lissu ndiye mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Chama kuliko mbowe, hii ilikua ni turufu pekee ya chama. Lakini Mbowe ameamua Chama kimfie mikononi anaangalia. Ni dhahiri kabisa kwamba Mbowe hajashauriwa.
 
Mbowe anatumika na waleeee.....anapiga deal....
 
Mbowe mwenyewe ni mzee...hahitaji ushauri ๐Ÿ˜
 
Mbowe anatumika na waleeee.....anapiga deal....
Mbowe anatumika, anajua kabisa hana Public Legitimacy ya kua Chadema na ameishiwa nguvu. Anamuona Lissu kama adui, mambo ya kijinga sana.
 
Mbowe mwenyewe ni mzee...hahitaji ushauri ๐Ÿ˜
Angewatafuta wazee wenzake washauriane watafute njia nzuri ya kukinusuru Chama. Sasa jamaa limejawa tamaa halifikirii mbele zaidi.
 
Mkuu, tatizo la CHADEMA siyo kukosa wazee. Laiti ungejua zimeshafanyika juhudi nyingi za kuwakalisha Lissu na Mbowe tena kwa kutumia watu maarufu kweli kweli. Je, unajua kuwa hata nyumbani kwa dr Slaa kumeshafanyika kikao cha kuwakutanisha? Je, unajua kuwa kuna vikao vya viongozi wa dini na wazee wengine wenye ushawishi ambavyo vimefanyika? Tatizo la CHADEMA ni fedha na ahadi za Samia kwa Mbowe plus Mbowe kukaa kwenye madaraka kwa muda mrefu mpaka akazoea na kujiona kuwa chama ni mali yake.
 
No! Ni zama mpya za transparency, haya mambo ya kufanya vitu gizani ndio yakome, mto mada unamaanisha uhalufu wa kitaasisi ufichwe kwa maelekezo ya wazee? Tungejuaje uchafu wa chadema chama kilichokua kimebeba matumaini ya watanzania kumbe ni uozo tu! Watu wanajitolea na kumwaga damu kumbe ni liscam tu linatumika na watawala!
 
ACT naimani itakua inafurahia sana hii mbungi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ