Uzi unalenga lenga hasa wazungu wa West (Marekani na Ulaya/EU) hao wengi wa mashariki kama Serbia, Russia, Belarus wako mbali sana kiutamaduni na West.
Wewe unaona mashiko yoyote Rais aliyeopo madarakani analalamika kuibiwa kura katika majimbo yanayoongozwa na chama chake?
Mambo ya Trump kusema ameibiwa kura ni ujinga na ujuha mtupu. Waliosimamia uchaguzi anakosema aliibiwa ni Republicans wenzake, bunge la seneti lililothibitisha matokeo ya urais lilikuwa linaoongozwa na Republicans wenzake, makamu wa Rais ambaye ni mtu wa mwisho kuthibitisha matokeo alikwa makamu wake, mwanasheria wake mkuu aliyemteua mwenyewe alisema Trump ameshindwa kihalali, mahakama zote za chini mpaka mahakama kuu iliyojaa Republicans wote walisema uchaguzi haukuwa na shida yoyote na listi bado inaendelea. ., sasa wewe utapata wapi mfumo wa haki na wa huru zaidi ya huo hapa duniani??!