Pre GE2025 Tatizo la chaguzi za Afrika ni nini hasa? Kwa nini wazungu wanaheshimiana sana kwenye chaguzi zao?

Pre GE2025 Tatizo la chaguzi za Afrika ni nini hasa? Kwa nini wazungu wanaheshimiana sana kwenye chaguzi zao?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ha ha

Kwanza kabisa ukome kunichagulia mambo am bayo naweza na ambayo siwezi kubishana. That aside.

Hunijui, so huwezi kusema kwamba sielewi au sijaona au kushiriki kwenye Chaguzi!

Hizo nchi ambazo mnadai hakuna uchafu huko nao walitoa ripoti za Uchaguzi, na hakuna hata mmoja aliyesema Uchaguzi Tz ni Upuuzi. Ieleweke Hayo ni maoni yako tu Non else.

Sasa, Kilicho wazi ni kwamba hata Ulaya na Marekani kuna Uchaguzi tata.

Na wewe acha Ukasuku. Uwe unavaa na akili zako mchana. Umekula?
Kuitwq mpuuzi sio tusi Basi naomba nikuite wewe ni "mpuuzi". Nimekwambia nitajie Nchi ambayo kiongozi wake ametajirika kupitia uongozi wa kisiasa unaleta ngonjera..
 
Honestly hata sijui huwa unaongeaga utoto gani?! Na si ajabu ukakomaa hapa kwenye huu uzi na utoto huo huo!
Kavae akili wewe gaidi. kawadanganye wajinga wenzako huko Ugaidini. Kama huna akili siwezi kukusaidia. Kanuni ni kwamba huelewi unauliza ueleweshwe.
Zaidi ya hapo ulegee tu
 
Msingi wa chaguzi yoyote unaanza kwa kuaminiana. Kama hakuna kuaminiana lazima kelele ziwe nyingi.

Tena ikiletwa na teknolojia ya kupiga kura kupitia mitandao kama wazungu, ndio kabisa lazima kuna hati hati ya kuchinjana kisa fulani analaumu mwenzake kamchezea faulo kwa kuhack system ya kielektroniki🥱 na kuiba kura.
 
Tukizungumzia demokrasia za huko Duniani tunazungumzia Amerka ya kaskazini na Ulaya ya magharibi !

Sio Amerika ya kusini na wala sio Ulaya ya mashariki !
Kwa mara ya kwanza katika historia yao ya demokrasia ni Trump pekee ndiye aliyeleta ule utata katika Uchaguzi , Na mpaka leo bado wanamshangaa !!
Kwanza nashangaa mnapozungumzia Afrika mnaweka Bara lote kwenye kikapu kimoja.Hamzitenganishi kama ulivyo fanya kwa Amerika Kaskazini na Ulaya Magharibi.
Pili Trump hakuwa wa kwanza kupinga na kuelezea wasiwasi wake juu ya chaguzi.
Nitakupa mifano miwili 1960 Richard Nixon alipinga ushindi wa JF Kennedy .Alidai kuwekuwa na wizi kwenye states 9.Illinois,Texas,Delaware Michigan Minnesota,Missouri,New Jersey New Mexico,Nevada,Pennsylvania na South Carolina.
Mwaka 2000 Al Gore alipinga ushindi wa George Bush Senior na ikabidi ushindi uamuliwe na Mahakama.
 
Honestly hata sijui huwa unaongeaga utoto gani?! Na si ajabu ukakomaa hapa kwenye huu uzi na utoto huo huo!
Mbowe, Zitto, Lema na wengine wengi tu walikuwa masikini.
Kuitwq mpuuzi sio tusi Basi naomba nikuite wewe ni "mpuuzi". Nimekwambia nitajie Nchi ambayo kiongozi wake ametajirika kupitia uongozi wa kisiasa unaleta ngonjera..
Sasa kama unaniambia nikujibu vipi tena? Uliuliza?

Usijiondoe Ufahamu.
 
Yoda Tafadhali.

Usipotoshe.

John Quincy Adams kwenye uchaguzi wa Rais ma Andrew Jackson alisema uchaguzi umeibiwa! hiyo ilikuwa mwaka 1824.

Samuel Tiden 1876 alidai lulikuwa na vitisho na wizi wa kura.

Richard Nixon alishindwa kwa J.F Kenedy nao alidai wameongeza kura kwenye masanduku! hiyo ni 1960!

Al Gore mwaka 2000!

au?

Utakataa hayo?

Hizo taarifa Wikipedia zipo, wewe unatudanganya hapa kama sio ktukana na kupotosha
Ingawa yote uliyoandika ni uongo, upotoshaji na yako mbali kabisa na muktadha wa uzi lakin hata kama ingekuwa ni kweli huoni kwa kipindi karibia cha miaka 250 ya uhai wa Marekani kama una matatizo ya uchaguzi mkuu yasiyofika hata 10 kumi huo mfumo uko vizuri sana na uchaguzi ni jambo la kuheshimika?!
 
Tatizo lako ni sweeping statements. Serbia ni Nchi ya wazungu kumetokea maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi,wapinzani wakidai wameibiwa.Marekani uchaguzi uliopita mgogoro bado unaendelea.Uwewahi kusikia mgogoro wa uchaguzi Botswana,Namibia au hata Zambia.Je hizo sio Nchi za kiafrika?
Migogoro mingi inaletwa pia na upande mmoja kutoheshimu sanduku la kura. Wakishinda wao all is all right wakishindwa wameibiwa.
Uzi unalenga lenga hasa wazungu wa West (Marekani na Ulaya/EU) hao wengi wa mashariki kama Serbia, Russia, Belarus wako mbali sana kiutamaduni na West.

Wewe unaona mashiko yoyote Rais aliyeopo madarakani analalamika kuibiwa kura katika majimbo yanayoongozwa na chama chake?

Mambo ya Trump kusema ameibiwa kura ni ujinga na ujuha mtupu. Waliosimamia uchaguzi anakosema aliibiwa ni Republicans wenzake, bunge la seneti lililothibitisha matokeo ya urais lilikuwa linaoongozwa na Republicans wenzake, makamu wa Rais ambaye ni mtu wa mwisho kuthibitisha matokeo alikwa makamu wake, mwanasheria wake mkuu aliyemteua mwenyewe alisema Trump ameshindwa kihalali, mahakama zote za chini mpaka mahakama kuu iliyojaa Republicans wote walisema uchaguzi haukuwa na shida yoyote na listi bado inaendelea. ., sasa wewe utapata wapi mfumo wa haki na wa huru zaidi ya huo hapa duniani??!
 
Tatizo elimu iliyopandikizwa kwetu ndio kikwazo chenyewe. Wakati huo UK iko chini ya utawala wa Kifalme. Sisi tunaona ujinga. Na huo ndio ujinga wenyewe.
African tuna tradition zetu ambazo hazifanani na watu weupe. Huwezi kama Mwafrika kuletewa eti Haki ya mwanaume kuinamishwa halafu ukikataa uonekane haufai kuwa kiongozi.

Huwezi kulazimisha 50/50 ngazi za utawala wakati tunajua mwanamke wa kiafrika ni nani na mwanaume ni nani?
Huwezi kulazimisha mwanaume wa Kafrika aende kliniki na mke wake wakati tunajua hata nature zao za kazi . Ni upuuzi tupu.

Afrika i solve matatizo yake katika mtindo wa Kafrika sio observers to nje ya Afrika.
Never ever. Tutabaki katka vicious cycle hii forever
Mimi ninazungumzia uchaguzi, mbona hata huko nchi za Africa ambako wagombea wote wanapinga ushoga bado matatizo ya uchaguzi ni makubwa mno kupeleka migogoro mikubwa ya kisiasa na hata vita vya wenyewe??
 
Umasikini, njaa na kutokuthaminiana!, Mkurugenzi wa uchaguzi anatoa tamko kwa wakurugenzi wa wilaya chama kipi kishinde, mkurugenzi wa wilaya anatoa maelekezo kwa wasimamizi wa kata mgombea yupi ashinde na kura zipigwe ziongezwe baada ya raia kupiga kura halali!.
Mfumo mbovu wa tume ya uchaguzi, tume imejaa makada wa chama!, Hizo 4R zinazopigiwa debe zianze kwenye Reformation ya tume ya uchaguzi pale ni uozo... 2015 nimekuwa sehemu ya huu huu mchakato nilichokiona hakika ni upuuzi mtupu.
Mbona nchi za magharibi hakuna hata tume za uchaguzi na watu hawaibiani kura na pia kama kuna matatizo yoyote yanamalizwa kwa ustaarabu mkubwa na amani tele kupitia vyombo mbalimbali na mahakama??
 
sasa mbona kama mifumo yao imekufa, mbona hawafikii hatua ya kuuana, vita na vurugu kama kwetu afrika ambako uchaguzi ukiisha tu ni taharuki!yaani hata kabla ya uchaguzi nchi zinakua ktk taharuki ambayo ni ya kijinga hvi!
Swali la msingi, yani uchaguzi Africa hadi mawasiliano yatakatwa mpaka uchaguzi uishe na hadi vifaru vya kijeshi vitazagaa mitaani, taharuki tupu!
 
Msingi wa chaguzi yoyote unaanza kwa kuaminiana. Kama hakuna kuaminiana lazima kelele ziwe nyingi.

Tena ikiletwa na teknolojia ya kupiga kura kupitia mitandao kama wazungu, ndio kabisa lazima kuna hati hati ya kuchinjana kisa fulani analaumu mwenzake kamchezea faulo kwa kuhack system ya kielektroniki🥱 na kuiba kura.
Kwa nini Waafrika hawaaminiani katika uchaguzi? Tatizo hasa ni nini??
 
Kwanza nashangaa mnapozungumzia Afrika mnaweka Bara lote kwenye kikapu kimoja.Hamzitenganishi kama ulivyo fanya kwa Amerika Kaskazini na Ulaya Magharibi.
Pili Trump hakuwa wa kwanza kupinga na kuelezea wasiwasi wake juu ya chaguzi.
Nitakupa mifano miwili 1960 Richard Nixon alipinga ushindi wa JF Kennedy .Alidai kuwekuwa na wizi kwenye states 9.Illinois,Texas,Delaware Michigan Minnesota,Missouri,New Jersey New Mexico,Nevada,Pennsylvania na South Carolina.
Mwaka 2000 Al Gore alipinga ushindi wa George Bush Senior na ikabidi ushindi uamuliwe na Mahakama.
Katika nchi 54 za Africa Unafikiri nchi zipi za zina afadhali na za mfano linapokuja swala la uchaguzi ??
 
Mbona nchi za magharibi hakuna hata tume za uchaguzi na watu hawaibiani kura na pia kama kuna matatizo yoyote yanamalizwa kwa ustaarabu mkubwa na amani tele kupitia vyombo mbalimbali na mahakama??
Sababu ya kuwepo kwa Strong institutions kikatiba !!
 
Fikra hasi kama hizi kwa Mwaafrika ndizo zinazozo wachanganya watu kufikiria hatushehimiani...

Afrika hakuna shida za kuheshimiana, shida ipo kwa wazungu kutokuheshimu mifumo na michakato ya Uchaguzi za Waafrika.

Waafrika kwa sasa hawadanganyiki sana kivile.

Waambie waache kutuingilia katika chaguzi zetu.
Lini waliingilia chaguzi zetu ? Hizi ndio shida ambazo mtoa mada anazisema kuwa Waafrica tuna tatizo sehemu
 
Botswana,Namibia,Seychellerna,Mauritius,Ghana Liberia(hivi karibuni George Weah alishindwa na kukabidhi madaraka bila kelele)hazipo Afrika?Wacha inferiority complex. Uzi ulisema wazungu unapobanwa na kupewa mifano unakimbilia Western Europe.Nchi ya Spain miaka sio mingi ilikuwa kwenye udikteta wa General Franco.
 
Mbona nchi za magharibi hakuna hata tume za uchaguzi na watu hawaibiani kura na pia kama kuna matatizo yoyote yanamalizwa kwa ustaarabu mkubwa na amani tele kupitia vyombo mbalimbali na mahakama??
Hakuna tume za uchaguzi?, Mfumo imara wa kiutawala unakupa kila unachokitaka bila shida!. Kusema hakuna tume za uchaguzi sio sawa sema wana taasisi imara zinazotoa haki.
"Hatuwezi kuendelea Kama hatuwezi kubadili fikra na namna ya kufikiria". Viongozi wa ulaya wanawaza namna gani ataisaidi jamii kimaendeleo wakati huo viongozi wa kiafrika wanawaza namna gani ataiba Mali za umma atajirike.
 
Uzi unalenga lenga hasa wazungu wa West (Marekani na Ulaya/EU) hao wengi wa mashariki kama Serbia, Russia, Belarus wako mbali sana kiutamaduni na West.

Wewe unaona mashiko yoyote Rais aliyeopo madarakani analalamika kuibiwa kura katika majimbo yanayoongozwa na chama chake?

Mambo ya Trump kusema ameibiwa kura ni ujinga na ujuha mtupu. Waliosimamia uchaguzi anakosema aliibiwa ni Republicans wenzake, bunge la seneti lililothibitisha matokeo ya urais lilikuwa linaoongozwa na Republicans wenzake, makamu wa Rais ambaye ni mtu wa mwisho kuthibitisha matokeo alikwa makamu wake, mwanasheria wake mkuu aliyemteua mwenyewe alisema Trump ameshindwa kihalali, mahakama zote za chini mpaka mahakama kuu iliyojaa Republicans wote walisema uchaguzi haukuwa na shida yoyote na listi bado inaendelea. ., sasa wewe utapata wapi mfumo wa haki na wa huru zaidi ya huo hapa duniani??!
Sasa wewe unataka wazungu gani au hao wa west sio wazungu?
 
Back
Top Bottom