Pre GE2025 Tatizo la chaguzi za Afrika ni nini hasa? Kwa nini wazungu wanaheshimiana sana kwenye chaguzi zao?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuitwq mpuuzi sio tusi Basi naomba nikuite wewe ni "mpuuzi". Nimekwambia nitajie Nchi ambayo kiongozi wake ametajirika kupitia uongozi wa kisiasa unaleta ngonjera..
 
Honestly hata sijui huwa unaongeaga utoto gani?! Na si ajabu ukakomaa hapa kwenye huu uzi na utoto huo huo!
Kavae akili wewe gaidi. kawadanganye wajinga wenzako huko Ugaidini. Kama huna akili siwezi kukusaidia. Kanuni ni kwamba huelewi unauliza ueleweshwe.
Zaidi ya hapo ulegee tu
 
Msingi wa chaguzi yoyote unaanza kwa kuaminiana. Kama hakuna kuaminiana lazima kelele ziwe nyingi.

Tena ikiletwa na teknolojia ya kupiga kura kupitia mitandao kama wazungu, ndio kabisa lazima kuna hati hati ya kuchinjana kisa fulani analaumu mwenzake kamchezea faulo kwa kuhack system ya kielektroniki🄱 na kuiba kura.
 
Kwanza nashangaa mnapozungumzia Afrika mnaweka Bara lote kwenye kikapu kimoja.Hamzitenganishi kama ulivyo fanya kwa Amerika Kaskazini na Ulaya Magharibi.
Pili Trump hakuwa wa kwanza kupinga na kuelezea wasiwasi wake juu ya chaguzi.
Nitakupa mifano miwili 1960 Richard Nixon alipinga ushindi wa JF Kennedy .Alidai kuwekuwa na wizi kwenye states 9.Illinois,Texas,Delaware Michigan Minnesota,Missouri,New Jersey New Mexico,Nevada,Pennsylvania na South Carolina.
Mwaka 2000 Al Gore alipinga ushindi wa George Bush Senior na ikabidi ushindi uamuliwe na Mahakama.
 
Honestly hata sijui huwa unaongeaga utoto gani?! Na si ajabu ukakomaa hapa kwenye huu uzi na utoto huo huo!
Mbowe, Zitto, Lema na wengine wengi tu walikuwa masikini.
Kuitwq mpuuzi sio tusi Basi naomba nikuite wewe ni "mpuuzi". Nimekwambia nitajie Nchi ambayo kiongozi wake ametajirika kupitia uongozi wa kisiasa unaleta ngonjera..
Sasa kama unaniambia nikujibu vipi tena? Uliuliza?

Usijiondoe Ufahamu.
 
Ingawa yote uliyoandika ni uongo, upotoshaji na yako mbali kabisa na muktadha wa uzi lakin hata kama ingekuwa ni kweli huoni kwa kipindi karibia cha miaka 250 ya uhai wa Marekani kama una matatizo ya uchaguzi mkuu yasiyofika hata 10 kumi huo mfumo uko vizuri sana na uchaguzi ni jambo la kuheshimika?!
 
Uzi unalenga lenga hasa wazungu wa West (Marekani na Ulaya/EU) hao wengi wa mashariki kama Serbia, Russia, Belarus wako mbali sana kiutamaduni na West.

Wewe unaona mashiko yoyote Rais aliyeopo madarakani analalamika kuibiwa kura katika majimbo yanayoongozwa na chama chake?

Mambo ya Trump kusema ameibiwa kura ni ujinga na ujuha mtupu. Waliosimamia uchaguzi anakosema aliibiwa ni Republicans wenzake, bunge la seneti lililothibitisha matokeo ya urais lilikuwa linaoongozwa na Republicans wenzake, makamu wa Rais ambaye ni mtu wa mwisho kuthibitisha matokeo alikwa makamu wake, mwanasheria wake mkuu aliyemteua mwenyewe alisema Trump ameshindwa kihalali, mahakama zote za chini mpaka mahakama kuu iliyojaa Republicans wote walisema uchaguzi haukuwa na shida yoyote na listi bado inaendelea. ., sasa wewe utapata wapi mfumo wa haki na wa huru zaidi ya huo hapa duniani??!
 
Mimi ninazungumzia uchaguzi, mbona hata huko nchi za Africa ambako wagombea wote wanapinga ushoga bado matatizo ya uchaguzi ni makubwa mno kupeleka migogoro mikubwa ya kisiasa na hata vita vya wenyewe??
 
Mbona nchi za magharibi hakuna hata tume za uchaguzi na watu hawaibiani kura na pia kama kuna matatizo yoyote yanamalizwa kwa ustaarabu mkubwa na amani tele kupitia vyombo mbalimbali na mahakama??
 
sasa mbona kama mifumo yao imekufa, mbona hawafikii hatua ya kuuana, vita na vurugu kama kwetu afrika ambako uchaguzi ukiisha tu ni taharuki!yaani hata kabla ya uchaguzi nchi zinakua ktk taharuki ambayo ni ya kijinga hvi!
Swali la msingi, yani uchaguzi Africa hadi mawasiliano yatakatwa mpaka uchaguzi uishe na hadi vifaru vya kijeshi vitazagaa mitaani, taharuki tupu!
 
Kwa nini Waafrika hawaaminiani katika uchaguzi? Tatizo hasa ni nini??
 
Katika nchi 54 za Africa Unafikiri nchi zipi za zina afadhali na za mfano linapokuja swala la uchaguzi ??
 
Mbona nchi za magharibi hakuna hata tume za uchaguzi na watu hawaibiani kura na pia kama kuna matatizo yoyote yanamalizwa kwa ustaarabu mkubwa na amani tele kupitia vyombo mbalimbali na mahakama??
Sababu ya kuwepo kwa Strong institutions kikatiba !!
 
Lini waliingilia chaguzi zetu ? Hizi ndio shida ambazo mtoa mada anazisema kuwa Waafrica tuna tatizo sehemu
 
Botswana,Namibia,Seychellerna,Mauritius,Ghana Liberia(hivi karibuni George Weah alishindwa na kukabidhi madaraka bila kelele)hazipo Afrika?Wacha inferiority complex. Uzi ulisema wazungu unapobanwa na kupewa mifano unakimbilia Western Europe.Nchi ya Spain miaka sio mingi ilikuwa kwenye udikteta wa General Franco.
 
Mbona nchi za magharibi hakuna hata tume za uchaguzi na watu hawaibiani kura na pia kama kuna matatizo yoyote yanamalizwa kwa ustaarabu mkubwa na amani tele kupitia vyombo mbalimbali na mahakama??
Hakuna tume za uchaguzi?, Mfumo imara wa kiutawala unakupa kila unachokitaka bila shida!. Kusema hakuna tume za uchaguzi sio sawa sema wana taasisi imara zinazotoa haki.
"Hatuwezi kuendelea Kama hatuwezi kubadili fikra na namna ya kufikiria". Viongozi wa ulaya wanawaza namna gani ataisaidi jamii kimaendeleo wakati huo viongozi wa kiafrika wanawaza namna gani ataiba Mali za umma atajirike.
 
Sasa wewe unataka wazungu gani au hao wa west sio wazungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…