Tatizo la gear kwenye Harrier 3.0L

Tatizo la gear kwenye Harrier 3.0L

muuza ubuyu

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
3,539
Reaction score
3,551
Wanabodi,

Nina gari langu sasa ambalo linatembea ila lina shida inayonisumbua leo miezi mitatu tangu lianze na kila ninapolitatua halitatuliki.

Taa ya check engine huwa inawaka hasa nikiendesha speed walau ya 80 kwa kama km 30.
Nikiendesha pia zaidi ya speed ya 70 gear number 4 inagoma ku engage!

Nimeshafanya diagnosis kila mara inasema tatizo ni knock sensor ya bank 2. Je, matatizo ya knock sensor na ku-engage gear number 4 yanauhusiano? Je matatizo haya yanatatulika?

Msaada jamani!
 
Pia ww ni mvivu wa service unaiendesha hiyo gari kimazoea ili mradi uwe barabarani
 
Umetumia kigezo gani kujua mimi ni mvivu wa service? Oil ya gear box nabadirisha kila baada ya 15,000km, engine oil baada ya 4,000km. Na kila ninapohisi ina tatizo naenda garage! Tatizo nililojifunza ni kwamba haya magari hakuna mafundi wazuri, waliopo walio wengi wanabahatisha!

Jifunze kutokukurupuka!
 
Nunua gearbox tofauti na hapo ni wizi!
Thanks, nilishafuatilia online forums moja kuna mtu yeye ilikuwa inaruka gear namba 2, jamaa mmoja akasema kuna tatizo la selenoid (hope nimepatia spelling) inagoma kufunguka ili gear husika i engage.
Na issue ya knock sensor ndiyo inaleta shida kwani garage nyingi ambazo ni nzuri kabisa hawakupi solution.
 
Ipeleke Evolution Garage, jamaa wapo vizuri sana
 
Umetumia kigezo gani kujua mimi ni mvivu wa service? Oil ya gear box nabadirisha kila baada ya 15,000km, engine oil baada ya 4,000km. Na kila ninapohisi ina tatizo naenda garage! Tatizo nililojifunza ni kwamba haya magari hakuna mafundi wazuri, waliopo walio wengi wanabahatisha!

Jifunze kutokukurupuka!
Kwa harrier 3.0L naamini ni moja ya matoleo mazuri sana ya harrier yanayo vumilia kwenye mazingira magumu!! Kwa ujumla harrier ya toleo hilo ni moja kati ya magari niliyo wahi tumia muda! Hizi gari za auto-trans ni tofauti kabisa na manual trans na nyingi hata ukifanya service zina specify aina ya oil na nyingine utakua hata hizo oil zinazo taka hapa kwetu hamna na hata ukazingatia kutafuta utazipata kwa shida na ndio maana nika kwambia change gearbox nenda ilala kama una nguvu kidogo ila wakisha igusa VALVE CHACE kwenye gear box ni mtihani bora kununua used japan
 
Thanks, nilishafuatilia online forums moja kuna mtu yeye ilikuwa inaruka gear namba 2, jamaa mmoja akasema kuna tatizo la selenoid (hope nimepatia spelling) inagoma kufunguka ili gear husika i engage.
Na issue ya knock sensor ndiyo inaleta shida kwani garage nyingi ambazo ni nzuri kabisa hawakupi solution.
Sio knock sensor tu hata air flow metre kwa haria na baadhi ya nissan bado ni mtihani!? Kikubwa uijue gari unayo miliki inatakaje na uta ihudumiaje!
 
Kwa harrier 3.0L naamini ni moja ya matoleo mazuri sana ya harrier yanayo vumilia kwenye mazingira magumu!! Kwa ujumla harrier ya toleo hilo ni moja kati ya magari niliyo wahi tumia muda! Hizi gari za auto-trans ni tofauti kabisa na manual trans na nyingi hata ukifanya service zina specify aina ya oil na nyingine utakua hata hizo oil zinazo taka hapa kwetu hamna na hata ukazingatia kutafuta utazipata kwa shida na ndio maana nika kwambia change gearbox nenda ilala kama una nguvu kidogo ila wakisha igusa VALVE CHACE kwenye gear box ni mtihani bora kununua used japan
Oil ya gear box ninayotumia ni ile ya Toyota T-IV, kama walivyo specify, engine oil GTX. Air flow meter haina shida kabisa! Hata air cleaner nipo very sensitive kiasi kwamba nishanunua tatu kama nina safari ndefu barabara ya vumbi nabadirisha njiani!
 
My take:! Ukienda ilala kanunue gearbox used japan ila sio kingine utaikimbia hiyo gari kwa gear tu na si utani pale ilala wameni7bbsha mpaka leo nikiona gari yoyote ya automatic naona kama ni kichwa cha kuku!!: yalinikuta kwenye hiyo hiyo harrier tulipambana na gear mwishoe waka ua na diff ya four-wheel kwenye test na baada ya miaka kadhaa nikakumbana nao kwenye subaru legacy ya 1999 na cc1999 auto_manual kwa ujumla mpaka leo kila nikiona mtu ana iendesha naona kama ni jini kumbe nilikuja kubaini hizi gari haziitaji mafundi wa ilala ila kwa bahati mbaya sikuwafahamu mafundi husika kabla
 
Thanks! Nipo mikoani ngoja nipambane! Ikibidi kununua gear box basi hamna namna!
 
pole mkuu, hili gari ni miongoni mwa magari niyapendayo, vipi ina changamoto gani nyengine zaidi ya hizo, na vipi ulaji wake wa mafuta?
 
Harrier ina gear 4, unategemea kweli uipate gia namba 4 ukiwa na spidi 70? possibly gia namba 4 inapatikana spidi around 120
Mkuu, ninachokiongea ni uzoefu wa gari ambalo nimekaa nalo nearly miaka miwili sasa! Ni gari ninalolijua! Gear namba 4 inapatikana kuanzia 70 kuendelea. Nishajaribu kwa sasa unaweza ukafika hata 140kph upo tatu. Ninachofanya sasa nina drive over drive button ikiwa off ili nicheze na gear 1-3 tu. Kwa hiyo tatizo lipo!
 
pole mkuu, hili gari ni miongoni mwa magari niyapendayo, vipi ina changamoto gani nyengine zaidi ya hizo, na vipi ulaji wake wa mafuta?
Thanks kaka, ni gari zuri sana na kifupi halina changamoto kuubwa, sema changamoto ya Magari haya ya kisasa ni mafundi. Kiufupi mafundi wazuri ni ngumu sana kuwapata lakini kiuhalisia haya matatizo ni ya kawaida kabisa.
Kitu kingine pia spear zake ziko juu kidogo na ulaji wa mafuta inategemea uendeshaji wako ila ina range 8-10km/Ltr. Hii ni sisi wa mikoani sasa mijini nasikia wanaziogopa sana gari hizi unapoongelea foleni! Hasa foleni kama za Dar!
 
hasante kwa mrejesho.
 
Back
Top Bottom