Tatizo la gear kwenye Harrier 3.0L

Tatizo la gear kwenye Harrier 3.0L

My take:! Ukienda ilala kanunue gearbox used japan ila sio kingine utaikimbia hiyo gari kwa gear tu na si utani pale ilala wameni7bbsha mpaka leo nikiona gari yoyote ya automatic naona kama ni kichwa cha kuku!!: yalinikuta kwenye hiyo hiyo harrier tulipambana na gear mwishoe waka ua na diff ya four-wheel kwenye test na baada ya miaka kadhaa nikakumbana nao kwenye subaru legacy ya 1999 na cc1999 auto_manual kwa ujumla mpaka leo kila nikiona mtu ana iendesha naona kama ni jini kumbe nilikuja kubaini hizi gari haziitaji mafundi wa ilala ila kwa bahati mbaya sikuwafahamu mafundi husika kabla
Nikweli kabisa hapo dawa ni kununua gear box tu na bahati siyo bei mbaya
 
Vipi kaka
Hiyo diagnosis uliyofanyiwa bado haijaweza kuwasiliana na transmission! Knock sensor ipo kwenye engine (block to be specific) na kazi yake uhusiana na dynamic ignition timing.
Kuifanyia diagnosis kamili unahitaji Toyota Techstream na sio mashine za code reader. Techstream itakupa information na data yote ya mifumo YOTE ya gari. Hii ndio system wanatumia wakala na mafundi stadi wa Toyota.
Kulingana na maelezo yako, transmission oil unabadilosha ikiwa bado sawa; 15000km ni mapema sana kwa transmission oil. Engine oil inayofaa kutumia ni SYNTHETIC, GTX ni jina tu la mauzo na sio aina wala quality ya juu. Linganisha na Total Quartz 9000 ambayo ni synthetic base oil na utajionea tofauti kw bidhaa yenyewe na pia kw matumizi yake.
Back to your problem; hiyo transmission first yafaa kufanyiwa diagnosis na solution itapatikana hapo. Usijaribu kuwapa 'wasanii' wajaribu kuifungua! Ukitaka ushauri zaidi au huduma ya kiufundi wasiliana nami kw inbox!
Mkuu kwa maelezo yako naona una kitu unacho,naomba unisaidie tatizo la kagari kangu RAV4 3s tatizo ni pale unapo engage gear inalia sana ama inastuka tatizo ni lipi?
 
Makosa
  1. Gear Box hubadilishwa kila baada yaa km 6000
  2. Engine oil kila baada ya km 3000.
Hao mafundi wako ni kimeo. Na je upo Dar? Kama upo Dar basi ujue unapofanyia service walishakuloga na kukufanya ukubali kila wanachokuambia.
Ndugu kubadilisha oil yoyote inategemea na ubora wa oil
 
Umetumia kigezo gani kujua mimi ni mvivu wa service? Oil ya gear box nabadirisha kila baada ya 15,000km, engine oil baada ya 4,000km. Na kila ninapohisi ina tatizo naenda garage! Tatizo nililojifunza ni kwamba haya magari hakuna mafundi wazuri, waliopo walio wengi wanabahatisha!

Jifunze kutokukurupuka!
Kama mafundi wanabahatisha jaribu kwa waganga wa kienyeji maana mafundi hawaaminiki kabisa.
 
Mkuu, ninachokiongea ni uzoefu wa gari ambalo nimekaa nalo nearly miaka miwili sasa! Ni gari ninalolijua! Gear namba 4 inapatikana kuanzia 70 kuendelea. Nishajaribu kwa sasa unaweza ukafika hata 140kph upo tatu. Ninachofanya sasa nina drive over drive button ikiwa off ili nicheze na gear 1-3 tu. Kwa hiyo tatizo lipo!
Sasa 140 inafikaje wakati gear mwisho ni 4 na 4 haingii?
 
Sasa 140 inafikaje wakati gear mwisho ni 4 na 4 haingii?
Kwani wewe mkuu unadhani kama 4 haifiki ukawa umekanyagia mafuta speedometer itasoma mwisho ngapi? Gear 3 inafika hata 160kph.

Tatizo utakuwa unahatarisha gari lako kwani inafika speed hiyo rpm zikiwa juu mno, na hii itakusababisha uue engine!

Ukitaka experience muone mtu yoyote wa auto (maximum gear no. 4) aweke off over drive uone kama hiyo number 3 haiwezi fika 140kph!
 
Umetumia kigezo gani kujua mimi ni mvivu wa service? Oil ya gear box nabadirisha kila baada ya 15,000km, engine oil baada ya 4,000km. Na kila ninapohisi ina tatizo naenda garage! Tatizo nililojifunza ni kwamba haya magari hakuna mafundi wazuri, waliopo walio wengi wanabahatisha!

Jifunze kutokukurupuka!
ni kweli mkuu, harrier ni gari complicated, ikipata hitilafu inatakiwa apatikane fundi mzuri sana wa kurekebisha. nina experience na harrier
 
Duh hapa nimejifunza kitu. Kumbe watu tunaendesha tu magari lakini kuna vitu vingi hatujui.
 
Mkuu kwa maelezo yako naona una kitu unacho,naomba unisaidie tatizo la kagari kangu RAV4 3s tatizo ni pale unapo engage gear inalia sana ama inastuka tatizo ni lipi?
Lazima ifanyiwe diagnosis ili tujue mbona pressure haiko sawa!
 
Thanks kaka, ni gari zuri sana na kifupi halina changamoto kuubwa, sema changamoto ya Magari haya ya kisasa ni mafundi. Kiufupi mafundi wazuri ni ngumu sana kuwapata lakini kiuhalisia haya matatizo ni ya kawaida kabisa.
Kitu kingine pia spear zake ziko juu kidogo na ulaji wa mafuta inategemea uendeshaji wako ila ina range 8-10km/Ltr. Hii ni sisi wa mikoani sasa mijini nasikia wanaziogopa sana gari hizi unapoongelea foleni! Hasa foleni kama za Dar!
Samhani mkuu...naomba namba yako kuna kitu nataka nikuulize kuhusu harrier
 
Back
Top Bottom