Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

HII YA KUNYWA MAJI MARA KWA MARA inatafasirika vipi? Maana kuna watu tunakunywa maji sana ili kuweka mwili sawa. Na ukinywa maji sana maana yake ni kwamba utakojoa sana pia!

Kwa mgonjwa Wa kisukari inakuwaje? Anaskia kiu Mara kwa Mara au nini hufanya anywe maji sana?
Anasikia kiu mara kwa mara.
 
Mimi pia ni mhanga wa kisukari type 1, aisee asikuambie mtu kinatesa ni balaa
 
Wakuu wa nchi naombeni kwa mtu anayejua clinic ya watu wenye matatizo ya diabetes, kisukari , kwa mkoa wa Arusha mjini au Moshi mjini .

Maana nimechoka na hawa watu wasiokuwa na ujuzi wanakuambia usile tunda lolote labda tangoo tuu ,usinywe maziwa yeyote, usile mayai kabisa wali ,sembe ,machalariiii ,nyama hapana kabisa , mafuta ya aina yeyote ya kupikia.

Na wamesema kama ni ugali uwe wa mtama ,na mboga za majani basi.

Kama kuna mtu anafahamu diet ya mgonjwa wa diabetes please ashushee menu please.
Kula kila kitu unachopenda kwa utaratibu wa balanced diet BUT sharti lazima kupima kila siku na usiache kunywa dawa Huo ndio utaratibu mpya japo mm sio daktari, nahii ni baada yakugudua masharti ya chakula yalikuwa yanawadhoofisha wagonjwa sana,
 
Kula kila kitu unachopenda kwa utaratibu wa balanced diet BUT sharti lazima kupima kila siku na usiache kunywa dawa Huo ndio utaratibu mpya japo mm sio daktari, nahii ni baada yakugudua masharti ya chakula yalikuwa yanawadhoofisha wagonjwa sana,
Mmojawapo mimi ilibaki kidogo nipoteze maisha yangu kwa masharti magumu ya kisukari. Baada ya kuambiwa nile kila kitu sfya yangu imerudi na ni ngumu kujua kama naumwa kisukari
 
Punguza kula vyakula vya uwanga km mihogo,viaz
Juice ya ukwaju kwa sana sambamba na dawa
 
Salaam,
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari imeongezeka mara NNE zaidi na kufikia watu milioni 422 mwaka 2014 kutoka watu milioni 108 waliokuwa na ugonjwa huo katika miaka ya 80.

Kisukari Ni Nini?
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati. Matokeo ni kuharibiwa kwa viungo muhimu na hitilafu ya mzunguko wa damu.

Aina za kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo:
Kisukari Namba Moja
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans,katika
tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.
Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa kwa tezi hiyo.
Mashambulizi katika kongosho huweza kufanywa na magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga ya mwili.
Uharibifu katika tezi kongosho hupelekea kukosekana kabisa kwa homoni(kichocheo) cha insulin au huifanya insulin kuzalishwa kwa kiwango kidogo.
Wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za insulin kwa njia ya sindano katika maisha yao yote ili waweze kuishi. Ndiyo maana aina hii ya kisukari huitwa pia kisukari kinachotegemea Insulin au Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM)
2. Aina ya Pili ya Kisukari
(Hujulikana kama ugonjwa wa mtindo wa maisha kwani huchangiwa zaidi na ULAJI MBAYA NA KUTOFANYA MAZOEZI)
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.
Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi wa utendaji kazi wake.
Wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Ndiyo maana aina hii hujulikana pia kama kisukari kisichotegemea insulin au Non-Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM)


Dalili za Kuwa na Kisukari
kiu ya maji isiyoisha, kwenda haja ndogo mara kwa mara na vidonda au michubuko kuchukua muda mrefu kupona.
Nyingine ni ngozi kuwa kavu na kuwasha, mgonjwa kupoteza uzito bila sababu, kuwa na ukungu machoni, kuchoka kusiko kwa kawaida, hisia kupungua katika vidole na viganja
mikononi na miguuni na kuwa na ukungu katika fizi, ngozi na kibofu cha mkojo.
Hatua za mwanzo za kisukari huwa na dalili chache sana, hivyo inawezekana kabisa mtu asifahamu kuwa ana kisukari, ingawaje madhara yanaweza kuwa yameshatokea katika macho, figo na mfumo wa usukumaji damu mwilini.

Hatua Tatu Zinazoweza Kukusaidia Usipatwe na Kisukari
1. Pimwa kiwango cha sukari kwenye damu ikiwa una uwezekano mkubwa wa kupata kisukari. Mara nyingi aina ya pili ya kisukari huanza baada ya hatua inayoitwa prediabetes, yaani, ongezeko la kiwango cha sukari kwenye damu. Hatua hiyo ni hatari kama tu kisukari, lakini kuna tofauti: Ingawa ugonjwa wa kisukari unaweza kudhibitiwa, hauwezi kutibiwa. Kwa upande mwingine, watu walio na kiwango cha juu cha sukari kwenye damu wamefaulu kukipunguza. Huenda mtu asitambue dalili za ongezeko la sukari kwenye damu. Kulingana na ripoti mbalimbali, karibu watu milioni 316 duniani pote wana kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu; ingawa wengi wao hawajui wana kiwango hicho. Kwa mfano, nchini Marekani pekee asilimia 90 ya watu wenye sukari nyingi kwenye damu hawatambui kama wana tatizo hilo.
Ingawa hivyo, ongezeko la sukari kwenye damu ni hatari. Mbali na kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo imehusianishwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa akili uitwao dementia. Kama wewe ni mnene kupita kiasi, hufanyi mazoezi kwa ukawaida, au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Unaweza kujua kiwango chako cha sukari ukipimwa damu.

2. Kula vyakula vyenye lishe. Unaweza kufaidika ukifanya mambo yafuatayo: Punguza kiasi cha chakula unachokula. Badala ya kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi au vinywaji vyenye kaboni kama vile soda, kunywa maji,juisi uliyoandaa wewe(ya sukari kidogo). Kula vyakula vya nafaka ambayo haijakobolewa(kama dona badala ya sembe). Epuka vyakula vilivyoungwa na mafuta mengi(ktk nyama,chipsi n.k)mbadala uwe samaki, njugu, karanga, na maharagwe.
3. Fanya mazoezi. Kufanya mazoezi kunaweza kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu na kukusaidia uwe na uzito unaofaa. Mtaalamu fulani anapendekeza kupunguza muda unaotumia kutazama televisheni ili uwe na muda wa kufanya mazoezi.
Huwezi kubadili chembe zako za urithi, lakini unaweza kubadili maisha yako, Utafaidika

N.b Kwa ambao tayari wana kisukari na wapo tayari kutumia DAWA YA ASILI YA KISUKARI tunaweza kuwasiliana kwa maelezo zaidi.0656871878,
 
Chanzo cha kisukari mamba moja ni kipi? Nini kinasababisha seli husika kushambuliwa?
 
Chanzo cha kisukari mamba moja ni kipi? Nini kinasababisha seli husika kushambuliwa?
1. Visababishi vya aina ya kwanza ya kisukari
Aina ya kwanza ya kisukari ina uhusiano mkubwa sana na kurithi. Aidha aina hii pia husababishwa na maambukizi ya
Coxsackie virus type B4.
Visababishi vingine ni pamoja na sumu inayotokana na kemikali za baadhi ya vyakula (food borne chemical toxins ), na kwa baadhi ya watoto wachanga maziwa ya ng’ombe yanaweza kuchochea kinga ya mwili wa mtoto kuushambulia mwili wenyewe (autoimmune reaction ) na hivyo kupelekea uharibifu katika tezi kongosho.
 
Chanzo cha kisukari mamba moja ni kipi? Nini kinasababisha seli husika kushambuliwa?
kwa kuongeza tu type 1 DM inasababisha na vitu vingi kama ifuatavyo
1.magonjwa yanashambulia kongosho ambayo husababishwa na virusi kama congenital rubella,coxsackievirus B.
2.sababu za kurithi
3.madawa mfano glucocorticoids
4.autoimune disease..*(ii ndio sababu kuu)
 
Wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za insulin kwa njia ya sindano katika maisha yao yote ili waweze kuishi.

Ingawa ugonjwa wa kisukari unaweza kudhibitiwa, hauwezi kutibiwa.

Kwa ambao tayari wana kisukari na wapo tayari kutumia DAWA YA ASILI YA KISUKARI tunaweza kuwasiliana kwa maelezo zaidi.0656871878,

Umesema Kisukari hakitibiki, hii dawa ya asili kazi yake ni nini?
 
Umesema Kisukari hakitibiki, hii dawa ya asili kazi yake ni nini?
Hiyo ni ripoti ya Kidaktari na inajulikana hospitali hakuna dawa inayotibu kisukari, lakini dawa za asili pamoja na kuwa hazipewi umuhimu kwa kizazi hiki cha leo hasa kizazi cha mijini, dawa asili zinatibu magojwa makubwa ajabu!
Hiyo dawa ni ya asili ndugu,kisukari hakitibiki hospitali
 
Kwa ulaji wa vyakula vyetu vya siku hizi na hasahasa mijini,upo uwezikano mkubwa sana takwimu kuongezeka hata mara tatu ya takwimu iliyo tolewa kwa takwimu itakayo fuata.
 
Kwa ulaji wa vyakula vyetu vya siku hizi na hasahasa mijini,upo uwezikano mkubwa sana takwimu kuongezeka hata mara tatu ya takwimu iliyo tolewa kwa takwimu itakayo fuata.
Ni kweli maana vijana ni mwendo wa viepeyai na azamMango,starehe bila mazoezi na wataalamu wa afya kuchoka kutoa elimu ya afya,ni kuandika dawa tu!
 
chanzo ni ulaji mbovu
Nisahihishwe kama nimekosea, kisukari cha kwanza (Type 1 diabetes) kinatokana na genes na mara nyingi huwapata watu tangia wakiwa wadogo au umri wa balehe. Type 2 diabetes ndiyo huwapata watu kutokana na life style.
 
Nisahihishwe kama nimekosea, kisukari cha kwanza (Type 1 diabetes) kinatokana na genes na mara nyingi huwapata watu tangia wakiwa wadogo au umri wa balehe. Type 2 diabetes ndiyo huwapata watu kutokana na life style.
Ndicho nilichoandika mkuu,kuwa 1DM huwapata watoto,vijana lakini nimemjibu mrs milas kuwa hutokana na kurithi(genes),virusi, maziwa ya ng'ombe na baadhi ya madawa kama alivochangia carcinoma

Nisahihishwe kama nimekosea, kisukari cha kwanza (Type 1 diabetes) kinatokana na genes na mara nyingi huwapata watu tangia wakiwa wadogo au umri wa balehe. Type 2 diabetes ndiyo huwapata watu kutokana na life style.
 
Back
Top Bottom