Salaam,
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari imeongezeka mara NNE zaidi na kufikia watu milioni 422 mwaka 2014 kutoka watu milioni 108 waliokuwa na ugonjwa huo katika miaka ya 80.
Kisukari Ni Nini?
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati. Matokeo ni kuharibiwa kwa viungo muhimu na hitilafu ya mzunguko wa damu.
Aina za kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo:
Kisukari Namba Moja
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans,katika
tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.
Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa kwa tezi hiyo.
Mashambulizi katika kongosho huweza kufanywa na magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga ya mwili.
Uharibifu katika tezi kongosho hupelekea kukosekana kabisa kwa homoni(kichocheo) cha insulin au huifanya insulin kuzalishwa kwa kiwango kidogo.
Wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za insulin kwa njia ya sindano katika maisha yao yote ili waweze kuishi. Ndiyo maana aina hii ya kisukari huitwa pia kisukari kinachotegemea Insulin au Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM)
2. Aina ya Pili ya Kisukari
(Hujulikana kama ugonjwa wa mtindo wa maisha kwani huchangiwa zaidi na ULAJI MBAYA NA KUTOFANYA MAZOEZI)
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.
Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi wa utendaji kazi wake.
Wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Ndiyo maana aina hii hujulikana pia kama kisukari kisichotegemea insulin au Non-Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM)
Dalili za Kuwa na Kisukari
kiu ya maji isiyoisha, kwenda haja ndogo mara kwa mara na vidonda au michubuko kuchukua muda mrefu kupona.
Nyingine ni ngozi kuwa kavu na kuwasha, mgonjwa kupoteza uzito bila sababu, kuwa na ukungu machoni, kuchoka kusiko kwa kawaida, hisia kupungua katika vidole na viganja
mikononi na miguuni na kuwa na ukungu katika fizi, ngozi na kibofu cha mkojo.
Hatua za mwanzo za kisukari huwa na dalili chache sana, hivyo inawezekana kabisa mtu asifahamu kuwa ana kisukari, ingawaje madhara yanaweza kuwa yameshatokea katika macho, figo na mfumo wa usukumaji damu mwilini.
Hatua Tatu Zinazoweza Kukusaidia Usipatwe na Kisukari
1. Pimwa kiwango cha sukari kwenye damu ikiwa una uwezekano mkubwa wa kupata kisukari. Mara nyingi aina ya pili ya kisukari huanza baada ya hatua inayoitwa prediabetes, yaani, ongezeko la kiwango cha sukari kwenye damu. Hatua hiyo ni hatari kama tu kisukari, lakini kuna tofauti: Ingawa ugonjwa wa kisukari unaweza kudhibitiwa, hauwezi kutibiwa. Kwa upande mwingine, watu walio na kiwango cha juu cha sukari kwenye damu wamefaulu kukipunguza. Huenda mtu asitambue dalili za ongezeko la sukari kwenye damu. Kulingana na ripoti mbalimbali, karibu watu milioni 316 duniani pote wana kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu; ingawa wengi wao hawajui wana kiwango hicho. Kwa mfano, nchini Marekani pekee asilimia 90 ya watu wenye sukari nyingi kwenye damu hawatambui kama wana tatizo hilo.
Ingawa hivyo, ongezeko la sukari kwenye damu ni hatari. Mbali na kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo imehusianishwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa akili uitwao dementia. Kama wewe ni mnene kupita kiasi, hufanyi mazoezi kwa ukawaida, au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Unaweza kujua kiwango chako cha sukari ukipimwa damu.
2. Kula vyakula vyenye lishe. Unaweza kufaidika ukifanya mambo yafuatayo: Punguza kiasi cha chakula unachokula. Badala ya kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi au vinywaji vyenye kaboni kama vile soda, kunywa maji,juisi uliyoandaa wewe(ya sukari kidogo). Kula vyakula vya nafaka ambayo haijakobolewa(kama dona badala ya sembe). Epuka vyakula vilivyoungwa na mafuta mengi(ktk nyama,chipsi n.k)mbadala uwe samaki, njugu, karanga, na maharagwe.
3. Fanya mazoezi. Kufanya mazoezi kunaweza kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu na kukusaidia uwe na uzito unaofaa. Mtaalamu fulani anapendekeza kupunguza muda unaotumia kutazama televisheni ili uwe na muda wa kufanya mazoezi.
Huwezi kubadili chembe zako za urithi, lakini unaweza kubadili maisha yako, Utafaidika
N.b Kwa ambao tayari wana kisukari na wapo tayari kutumia DAWA YA ASILI YA KISUKARI tunaweza kuwasiliana kwa maelezo zaidi.0656871878,