Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

Pole sana, usile nyama nyekundu zote, usile sugar au vyenye asili ya sugar. Chakula unachokula kiwe plated ya mfano ugali/wali uwe kidogo ila mboga za majani kwa wingi. Na mboga ule kila siku. Matunda kama nanasi, miwa usile. Ule samaki, maziwa kama alivyochangia hapo juu. Pia usile sana ule kidogo kidogo.
 
pamoja na msosi tafuta kitu inaitwa bio disk itakusaidia sana kutibu kisukari
 
Mimi kama mtu mwenye kisukari kwa miaka 13 napenda kukupa ushauri ufuatao zamani kulikuwa kuna masharti mengi lakini baada ya elimu kuongezeka tumeambiwa tule vyakula vyote vya kawaida lakini unapunguza wali/ugali/mikate myeupe,meza dawa kwa wakati fanya mazoezi,kunywa maji mengi na ULALE MAPEMA.Sijawahi kupata tatizo lolote na watu wengi wanashangaa nikiwaambia na kisukari kwa muda wote huu na nina afya nzuri nashukuru Mungu.
 
Maji hukinga na kuponya ugonjwa wa kisukari:
Maji-ni-uhai.jpg

Kisukari ni ugonjwa wa kongosho, wakati uzarishaji wa Insulini au utolewaji wake haufanyi kazi vizuri, na ikiwa hali hii haitadhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye macho, figo, neva, mishipa ya damu, Ini na moyo.

kuna aina kuu mbili za kisukari:


Kisukari aina ya kwanza, ambapo Insulini inakuwa tegemezi (insulin-dependent); hapa kongosho halitengenezi kabisa insulini au linaitengeneza kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba mgonjwa analazimika kuchomwa sindano ya insulini au kutumia pampu za insulini.


Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo Insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.


Aina ya kwanza ya kisukari inaweza kutokea kwa watu kuanzia utotoni mpaka kwa watu wa umri wa miaka 30. Aina hii ya kisukari hushambulia kwa haraka sana, kwa kawaida ndani ya majuma mpaka miezi kadhaa. Kwakuwa kongosho halifanyi kazi vizuri, usawa wa damu sukari lazima upewe uangalizi wa karibu. Watu wenye kisukari aina hii ya kwanza pia huwa na uzito pungufu (underweight).


Aina ya pili ya kisukari huanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 40 na kinachosababisha ni miaka mingi ya kula chakula kisicho sahihi, kutofanya mazoezi au sababu za kurithi (genetics). Kwa bahati mbaya, nyakati hizi tunashuhudia hata watoto wadogo wakipatwa na aina hii ya kisukari. Watu wenye kisukari cha aina hii ya pili pia huwa na uzito uliozidi (overweight).


Baadhi ya dalili kuu za kisukari ni:


  • Kiu iliyozidi
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kupatwa na ganzi kwenye miguu na mikono
  • Kujisikia mchovu
  • Kutoona vizuri
  • Kuongezeka njaa
  • Kushindwa kuhimili tendo la ndoa

Ikiwa daktari atakuona una dalili za kuwa na kisukari, ata kutaka ufanye jaribio la kuiandaa glukozi katika usawa wake wa chini kabisa kwenye damu (fasting plasma glucose test – fpgt), kwa sababu hiyo, atakutaka ubaki bila kula kitu chochote kwa muda usiopungua masaa nane kabla ya kukupima, ambapo kwa kawaida huwa ni asubuhi ili kupata uwezekano wa damu sukari kuwa katika usawa wake wa chini kabisa.


Kisha atachukua damu toka kwenye mkono na kuipima na kulinganisha matokeo na uwiano ufuatao:


  • Chini ya 99 mg/dl ni kawaida
  • 100 – 125 mg/dl ni hatua za mwanzo za kisukari
  • Zaidi ya 126 mg/dl ni kisukari.

Kisukari ambacho hakikudhibitiwa kinaweza kusababisha mwili kulazimika kuanza kuchoma mafuta ili kuzarisha nishati/nguvu (diabetic ketoacidosis), hii kwa kawaida hutokea kwa watu wenye kisukari cha aina ya kwanza ambapo glukozi inaweza kuingia kwenye seli bila insulini.


Kitendo cha mafuta kutumika kuzarisha nishati huzarisha taka nyingi za asidi zilijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘Ketones’.

Taka hizi (Diabetic ketoacidosis – DKA) hujijenga kwenye mzunguko wa damu na kusababisha pumzi fupi, mauzauza na kutapika na mwishowe kukuwekea koma na hata kusababisha kifo.


DKA haijitokezi sana siku hizi ahsante kwa insulini na vifaa rahisi kutumia kufuatilia damu sukari.


Wakati damu sukari inapokuwa nyingi na damu inapokuwa imetulia, nene na hafifu (hyperosmolar syndrome), husababisha kukojoa mara nyingi ili kuilazimisha sukari iliyozidi kutoka nje. Ikitokea hivyo, utapatwa na upungufu mkubwa wa maji na unaweza kushikwa na mikakamao ya miguu, mapigo ya moyo kwenda mbio, mauzauza, msukosuko, au hata kuelekea kwenye koma. Hii huwatokea watu wenye kisukari aina ya pili ambao hawafuatilii kujuwa kiasi cha damu sukari yao mwilini.


Moja kati ya matatizo makubwa ya kisukari ni kitendo cha kushuka kwa kiasi kikubwa cha damu sukari mwilini (hypoglycemia), hii hutokea wakati damu sukari inazarishwa kidogo kutokana na kutumia kiasi kingi cha insulini au kukaa muda mrefu bila kula chochote na huku ukiwa umetumia insulini au ulinusa harufu ya chakula fulani.


Zifuatazo ni dalili za kushuka kwa damu sukari mwilini:


  • Kichwa kuuma
  • Mauzauza
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio
  • Kutokwa na jasho jingi
  • Kuona vitu viwili katika kimoja.

Ikiwa damu sukari itashuka kufikia usawa wa 50 – 70 mg/dl, unaweza kujisikia kuwa na hali zifuatazo:



  • Kuishiwa nguvu
  • Kusinzia na kizunguzungu
  • Kuona nukta nukta kabla ya macho yako
  • Mwili unaweza kuwa kama uliopooza.

Wakati damu sukari imeshuka kufikia 30 – 45 mg/dl, unaweza kwenda kwenye koma (deep sleep) na kufa ikiwa hautapewa sukari ya haraka kama inayopatikana kwenye juisi ya chungwa (ambayo huitwa muokoaji kwenye uwanja wa madawa), sukari halisi au peremende ya sukari ili kupandisha kiwango cha damu sukari mwilini.

Namna moja ambayo kisukari kinaweza kujipenyeza taratibu kwenye miili ya watu, ni pale insulini inapofanya ukaidi bila wao kujua, ukaidi huu wa insulini ukitokea, kuna uwezekano mkubwa wa wewe kupatwa na kisukari wakati fulani katika safari yako ya kuishi.


Ukaidi wa insulini (insulin resistance) ni wakati ambapo mwili unazarisha insulini lakini hauitumii ipasavyo.

Insulini ni homoni inayotengenezwa na kongosho ili kuusaidia mwili kuitumia glukozi kwa ajili ya kuzarisha nishati. Glukozi ni aina ya sukari ambayo ni chanzo kikuu cha nishati ya mwili.


Mfumo wa umeng’enyaji wa chakula, hukimeng’enya chakula na kuwa glukozi ambayo kisha husafiri kwenye mkondo wa damu mwili mzima. Glukozi inapokuwa kwenye damu huitwa damu glukozi, pia hujulikana kama damu sukari. Wakati damu sukari inapopanda juu baada ya kula, kongosho huitoa insulini ili kuziwezesha seli za mwili wako kuitumia glukozi.

Mtu anapokuwa katika hali ya ukaidi wa insulini, mishipa, mafuta na Ini lake vinakuwa haviitiki vema kwa insulini, kwa sababu hii, mwili wake utaihitaji insulini zaidi ili kuiwezesha glukozi kuziingia seli.

Kongosho litajaribu kukidhi ongezeko la uhitaji huo wa insulini kwa kuizarisha insulini nyingi zaidi. Hatimaye kongosho nalo halitaweza kuendelea kumudu kuzarisha kiasi hicho kingi cha insulini. Insulini na Glukozi iliyozidi, vitajijenga ndani ya mkondo wa damu vikiandaa ngazi kuelekea kisukari.


Katika kitabu cha dr.Batmanghelidj kiitwacho ‘Your Bodies Many Cries For Water’ anasema ikiwa mwili una kiasi kidogo cha maji na chumvi, ubongo utakuwa unajiendesha kwa karibu ya aslilimia 100 kwa kutumia sukari.

Ubongo pia utapandisha juu kiwango cha sukari kwenye damu ili kuuwezesha kufanya kazi zake vizuri. Cha kushangaza ni kuwa, mwili unaihitaji insulini ili kuuwezesha kuitumia sukari kama chanzo cha nishati, lakini kamwe ubongo hauihitaji insulini ili kuupelekea mahitaji yake ya nishati.


Katika kisukari, ubongo unajipa moyo wenyewe kama vile daktari ampavyo moyo muathirika wa kisukari kwa kutumia dripu zenye sukari na chumvi (intravenous fluid treatment).


Watu wengi wenye kisukari huwa hawaelewi ni kwanini wanakuwa na damu sukari nyingi wakati waamkapo asubuhi ikiwa hawakula kitu chochote kabla ya kwenda kulala. Sababu ni kuwa, usiku unapokuwa umelala, mwili hufanya kazi kwa bidii kujiripea wenyewe, katika kufanya hivyo, mwili hutumia sukari. Kwakuwa haukula chochote kabla ya kwenda kulala, mwili lazima ujile wenyewe (cannibalize off itself) ili kuliwezesha Ini kutengeneza sukari kwa ajili ya nishati.


Ubongo, ambao ni kituo kikuu cha udhibiti wa kazi zote za mwili, utagunduwa kuwa hakuna kiasi cha kutosha cha sukari kwenye damu kwa ajili ya matumizi yake, na kwa sababu hiyo utaliamuru ini kutoa mara mbili mpaka tatu ya kiasi cha sukari ikiwa damu itaihitaji. Hii ndiyo sababu ya kupanda kwa kiwango cha sukari asubuhi kama hukula chochote kabla ya kwenda kulala.


Inashauriwa kwa watu wenye kisukari kula gramu 25 mpaka 30 za maharage machanga ya kijani kibichi au njegere (green beans), siagi halisi na chumvi dakika 15 kabla ya kwenda kulala, hii itasaidia kushusha damu sukari waamkapo asubuhi. Maharage haya yana kiasi kidogo cha wanga (carbs), na kiasi kingi cha protini, magnesiamu na asidi amino iitwayo ‘tryptophan’ ili kuubeba mwili usiku mzima.


Katika kuepuka sukari, baadhi ya watu wenye kisukari huamua kutumia viongeza sukari visivyo vya asili (artificial sweeteners). Unapoweka sukari ya kutengenezwa ulimini, ulimi utauambia ubongo kuwa sukari inakaribia kuja, ubongo utaliambia Ini liache kuendelea kutengeneza sukari bali liihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadaye na lijiandae kuishughurikia sukari iliyopo njiani kuja.


Ubongo upo makini sana (very smart), baada ya muda utagundua kuwa hakuna sukari iliyoliwa bali ulilaghaiwa. Dakika hii mzunguko wa damu unakuwa katika udharura wa uhitaji wa sukari.


Fikiri:
Kila siku unaenda dukani kununua sembe kilo moja. Siku moja unafika dukani mwenye duka anakuambia sembe limebaki kilo tatu na hajuwi lini atapata mzigo mwingine. utafanya nini?. Utafanya kila uwezalo uzichukuwe hizo kilo tatu zilizopo kama tahadhari kesho usishinde bila kula.


Ndicho kinachotokea mwilini. Ubongo ukishagunduwa kuwa iliyoliwa haikuwa sukari na ulishaliamuru Ini kupumzika kuitengeneza sukari kwenye mzunguko, utaliamuru Ini kuipatia damu mara mbili mpaka tatu ya kiasi cha sukari zaidi ya inavyohitajika!. Sasa unapoenda kupima kiasi cha damu sukari, unajikuta huelewi nini cha kufanya kwa sababu kipo juu mno. Na sasa lazima uchomwe insulini ili kuishusha damu sukari.


Dr.Batman, anasema; ‘kwa sehemu kubwa, kisukari ni matokeo ya kukosa maji, chumvi, magnesiamu, asidi amino (tryptophan) ipatikanayo kwenye mayai, maharage, vyakula jamii ya karanga na jibini, vitamini B6, zinki na mazoezi’.

Unapokuwa katika upungufu wa maji (haunywi ya kutosha) na unakula vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi kabisa, ‘automatikali’ ubongo utapandisha kiwango cha sukari kwenye damu yako.

Jitibu kwa kutumia maji
 
Kumekuwa na makala nyingi kwenye magazeti zinazoonesha ongezeko kubwa la wagonjwa wa Kisukari Tanzania, kwa aina zote. Ninaandika makala hii kwa ajili ya wale ambao tayari wanaugua Kisukari (aina ya I na ya II) hasa nikijikita katika umuhimu wa kujipima (BGL testing).


Moja ya changamoto kubwa aliyonayo mgonjwa wa Kisukari ni kupima na kuhakikisa kuwa kiasi cha sukari katika mfumo wake wa damu kipo katika kiasi kinachokubalika. Ugumu wa kutimiza hili mara nyingi unakuja kutokana na gharama za kupata kifaa cha kupimia (blood glucose meter) na mahitaji yake (test strips n.k.). Hii ni kwa wale wanaotaka kujipima wao wenyewe wakiwa majumbani mwao, kwa wale wanaotegemea kwenda kupima kwenye hospitali kuna tatizo la gharama (naamini sehemu nyingi si chini ya sh 2,000 kwa kipimo), umbali kutoka aliko mgonjwa na kituo cha afya, na kupangiwa tarehe iliyo mbali sana (mara nyingi huwa ni mara 1 kwa mwezi)hivyo kushindwa kufanya ufuatiliaji wa namna sukari katika damu (blood glucose) inavyobadilika-badilika.

Tangu kugundulika kuwa nina kisukari aina ya I (IDDM) miaka 12 iliyopita, nimepata uzoefu kuwa, pamoja na gharama na usumbufu wa kujidunga na kujitoboa mara nyingi kwa siku, kupima kiwango cha sukari katika damu na kuhifadhi kumbukumbu kunasaidia sana mgonjwa kuweza kuwa “daktari wake mwenyewe.” Mara nyingine mginjwa unajikuta unaendelea kuchoma sindano (insulin shots) kwa dozi ile ile kila siku hata kwa wakati ambako dozi ya kiwango kile si ya lazima na kupelekea matukio ya kushuka sana au kupanda sana kwa kiwango cha sukari katika damu. Pia uwekaji wa taarifa hizi kunasaidia kumpa daktari wako wakatii wa kliniki picha bora zaidi ya namna kisukari chako kinavyoendelea na hivyo kuweza kukupangia dozi ya dawa kwa ufasaha zaidi.

UFANYEJE?

Kwanza hakikisha unajiwekea malengo (goal), hii unaweza kufanya pweke yako au kwa kumshirikisha daktari wako. Mara nyingi wagonjwa huwa tunatakwa kuweza kuwa na wastani wa kiwango cha 180 mg/dL. Jiwekee lengo lako na uwekaji wako wa kumbukumbu uwe unaangalia ni kwa kiwango gani umeweza kufikia lengo lako.



  1. Namna ya kwanza ni kwa kutumia kijitabu (kwa wale ambao wamenunua mashine za kupimia watajua kuwa ndani yake huwa wanaweka na mfano wa LOGBOOK kwa ajili ya kuweka kumbukumbu zako)
  2. Namna ya pili kwa wale wanaoweza kununua mashine ambazo ni za kisasa zaidi ambazo zinakuja bundled na computer software and connecting accessories ambazo zinaweza kuhamisha taarifa kutoka kwenye mashine yake kwenda kwenda kwenye kompyuta yako.
  3. Namna nyingine ni kujitengenezea wewe mwenyewe logbook yako – kwa kutumia daftari ya kawaida au kwa kutumia spreadsheet kwa wale wenye access na kompyuta. Nimeambatanisha mifano ya spreadsheets za kompyuta amabo unaeza kutumia kuweka kumbukumbu ya vipimo vyako na kiwango cha insulin (au dawa nyinginezo) unazotumia.
  4. Namna ya nne ni kutumia application za simu za mkononi (hasa smart phones). Nikiwa mtumiaji wa simu za Android nimeona katika Play Store kuna apps nyingi, nzuri (za bure na za kulipia) ambazo zinaweza kutumika ili kufikia malengo haya. Kwa siku za hivi karibuni nimekuwa nikitumia app iitwayo GLUCOSE BUDDY ambayo ninaweza kui-recommend kwako pia.


Hadi wakati mwingine, JIPENDE, JITUNZE na USIJUTIE!

Notes:

  1. BGL - blood glucose level
  2. IDDM - insulin dependent diabetes mellitus
  3. Spreadsheet yenye jina BGL.xlsx nimetoa hapa

View attachment BGL.xlsxView attachment BGL spreadsheet example.xls


ANGALIZO:


Mwandishi siyo mtaalamu wa afya au wa masuala yanayohusiana na ugonjwa wa Kisukari bali ni mgonjwa wa kisukari ambaye anataka ku-share uzoefu wake na wagonjwa wengine. Mawazo haya yasichukuliwe kama yalivyo, consult daktari wako kwa ufafanuzi na maelekezo yenye utaalamu zaidi.
 
Mkuu Uporoto hayo mazoezi ni yale sirias kabisa au ya ki-lessure tu?
Ni ya kawaida tu mara 3 kwa wiki natembea 2km kwa nguvu na siku sijatembea nafanya pushups,pullups,situps na stretches kwa nusu saa nyumbani.
 
vilevile nimepata kusikia vyakula kama magimbi ndizi mbichi za kupika, ugali wa mtama kwa tulio nyumbani ni vitu unavyoweza kula bila matatizo
 
Naomba msaada
1. Habasoda na Mvuje ndo kitu gani na inapatikana wapi?
2. Tiba hii kwa ajili ya kisukari anina ipi (IDDM au NIDDM)?
3. Endapo unatumia insulin, je wakati wa matumizi ya dawa hii unawea kuendelea na dozi yako?
4. Kuna madhara yoyote (side effects) mtumiaji anazopaswa kuzijua?

Natanguliza shukrani.
 
Naomba msaada
1. Habasoda na Mvuje ndo kitu gani na inapatikana wapi?
2. Tiba hii kwa ajili ya kisukari anina ipi (IDDM au NIDDM)?
3. Endapo unatumia insulin, je wakati wa matumizi ya dawa hii unawea kuendelea na dozi yako?
4. Kuna madhara yoyote (side effects) mtumiaji anazopaswa kuzijua?

Natanguliza shukrani.
Habasoda kwa lugha ya kiingereza inaitwa (Nigella Sativa) na Mvuje waulize akina mama watakufahamisha zote hizo dawa zinapatikana kwenye Maduka ya Dawa za kiarabu au Maduka ya Wapemba hapo Kariakoo zinapatika hizo dawa zote na hazina Madhara waweza kutumia dawa za kizungu na hizo za kienyeji. Hizi Dawa za kienyeji hazina (Side effects) tumia zitakusaidia inshallah.
 
Naomba msaada
1. Habasoda na Mvuje ndo kitu gani na inapatikana wapi?
2. Tiba hii kwa ajili ya kisukari anina ipi (IDDM au NIDDM)?
3. Endapo unatumia insulin, je wakati wa matumizi ya dawa hii unawea kuendelea na dozi yako?
4. Kuna madhara yoyote (side effects) mtumiaji anazopaswa kuzijua?

Natanguliza shukrani.

Tambuwa pia kuwa kisukari ni ishara za mwili kupungukiwa maji sababu ya mazoea yetu ya kunywa maji baada ya kusikia kiu tena tunakunywa ya baridi hivyo tunaweza sema ni kama vile hatunywi maji!!. angalia pia chumvi unayotumia, ile ya mawe ya baharini ambayo haijapita kiwandani ndiyo bora zaidi (unrefined sea salt) sababu ya madini tofautitofauti zaidi ya 80 ndani yake. ukifanikiwa kuurudishia mwili maji unayoyahitaji kwa sasa wakati huu unapokuletea ishara za kisukari utafanikiwa pia kuacha kutumia insulini, unaweza kujisomea zaidi katika: maajabuyamaji2.artisteer.net/kisukari
 
Mama yangu anazidiwa na kisukari hivi sasa licha ya kuendelea kupata matibabu katika hospitali ya amana, anapoteza uzito kwa kasi sana sana. Anayefahamu lolote tafadhali - nakwama.
 
DAWA YA UGONJWA WA KISUKARI

>>>>Upate aina za dawa zifuatazo, kila moja
kiasi cha gram 100, saga
>>>>pamoja na dawa zifuatazo:
>>>>1. Shubiri
>>>>
>>>>2. Ubani
>>>>
>>>>3. Mvuje
>>>>
>>>>4. Ukwaju
>>>>
>>>>5. Habasoda
>>>>
>>>>(kiasi cha dawa hizi hazijatwangwa, hivyo jaribu kukadiria
>>>>mwenyewe) baada ya kusaga vizuri, gawanya katika mafungo matatu
>>>>yaliyosawa. Changanya fungu moja na maji kiasi cha chupambili na
>>>>uchemshe kwa dakika kumi. Ipua na iwache ipoe, chuja na hifadhi
>>>>katika chupa nadhifu.
>>>>
>>>> MATUMIZI YA DAYA YENYEWE
>>>>
>>>>Tumia kila siku kikombe kimoja cha kahawa kabla ya kula chochote
>>>>asubuhi kwa muda wa siku 13. Ikiisha dawa hii basi chukua fungu
>>>>la pili na uchemshe kama ulivofanya kwa fungu la mwanzo. Tumia
>>>>daya hii tena kwa muda ule ule wa siku 13.
>>>>
>>>>Itakapokwisha dawa hii basi chukua fungu la tatu na uitayarishe
>>>>kamaUlivyofanya mafungu mawili ya mwanzo. Tumia dawa hii kama
>>>>dawa hizo mbili za mwanzo ila tu kwa muda wa siku 14 , hii
>>>>itafanya jumla ya siku za kunywa daya kuwa siku 40.
>>>>
>>>>Baada ya siku hizo 40 utajisikia kuwa ugonjwa wa kisukari
>>>>umekwisha na unaweza kuanza kula vitu vyote ulivyokuwa
>>>>umekatazwa. Inshallah kwa kudra zake Mwenyezi Mungu utakuwa
>>>>umepona maradhi hayo

Mpe Pole sana mwambie azitumie hizi dawa kwa muda wa siku40 kisha unipe Feedback.@
ITSNOTOK
 
Kuna watu wengi wamepona sukari kuna mzee anajua dawa ya kienyeji yupo boga ni baba wa rafiki yangu kama unaiitaji fika mwenge vinyagoni duka no 58 uliza mudi raisi anaweza kukusaidia.
 
Wanajamvi,

Hii ni maalum kwa wale ambao tunaishi na ugonjwa wa Kisukari (Diabetes Mellitus) na pia wale wanaotunza/kuishi na wagonjwa wa Kisukari. Tupeane moyo, ushauri na mbinu. Pia tufahamishane namna bora za kujitunza (conventional and alternatives) na upatikanaji wa dawa na supplies na taarifa nyingine mbalimbali.

Karibu!

NB: Mimi nina IDDM since teens.
 
Wanajamvi,

Hii ni maalum kwa wale ambao tunaishi na ugonjwa wa Kisukari (Diabetes Mellitus) na pia wale wanaotunza/kuishi na wagonjwa wa Kisukari. Tupeane moyo, ushauri na mbinu. Pia tufahamishane namna bora za kujitunza (conventional and alternatives) na upatikanaji wa dawa na supplies na taarifa nyingine mbalimbali.

Karibu!

NB: Mimi nina IDDM since teens.

habari,
nami pia ni victim wahiyo maneno. Ila nimegundua tangu 2009, natumia dawa, nafanya mazoezi hasa ya kutembea mwendo mrefu kwa angalau saa moja nzima kwenda na kurudi,pia najitahidi kufuata masharti ya chakula. Pia nakunywa mafuta ya ubuyu daily kijiko kimoja kikubwa cha chakula.
Kazi ni kwetu.
 
Back
Top Bottom