Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
'Mwanangu usiwe na matarijio makubwa utakayoshindwa kuyatimiza na kuumuza moyo wako', ni nukuu ya maneno kutoka kwa wazazi wangu wakinisihi juu ya jambo. Ingali kauli hiyo ilitolea zamani sana lakini bado naikumbuka mpaka kesho I we usingizin au penginepo. Kutokana na usia huo naweza kusema Mimi ni mmoja wa watu wenye furaha na amani sana.
Kabla sijaenda kwenye mada kuu, tutafakari kwa ufupi sana uzito wa kauli hiyo na kinachoendelea mahakamani katika kesi ya Mbowe kupitia kwa shahidi Luten Urio. Toka shahidi huyu ameanza kutoa ushahidi kumeibuka kupinga mitandaoni. Kwa nini? Shahidi urio ndio anatufumbua macho kwamba CHADEMA walitaka kutwaa madaraka kwa nguvu yoyote hata wakishindwa. Tukirejelea kwenye nukuu, CHADEMA walikuwa na matarajio makubwa sasa hawawezi kuyatimiza sasa wanaumizwa mioyo.
Bwana Polepole ni mtu mwenye bahati , hilo sikatai lakini kujiona alikuwa "the chosen one" hapo ndipo penye ukakasi. Polepole aliibuliwa mtaani akiwa ni mwanaharakati tu na kuwa katibu mwenezi wa CCM taifa. Nafasi ambayo ilimfanya akae na wakubwa wa nchi, nafasi ambayo ilitambua uwepo wake hata katikati ya umati, nafasi ambayo ilitosha kukaa meza kuu ya sherehe au shughuli yoyote. Sasa yote hayo hana akiyakumbuka anaumia na kuvurugwa.
Siasa si shilingi ambayo ina pande mbili ila karata ambayo upande mmoja hautumiki. Mkiwa mnacheza karata ukawa mbele ya mwenye karata nzuri ya ushindi na anapotoa tabasamu wewe unabaki kuumia na kunyong'onyea na ndicho kinachomtokea polepole.
Polepole anaamini kwa kazi aliyofanya CCM hakustahili kuachwa bila uwepo wake kufikiriwa. Ndipo hapo kauli ya bahati kwa Polepole inakuja lakini bahati ina ukomo, unaweza kubahatisha Leo kesho unashindwa.
Tatizo la Polepole ni la kisaikolojia ,kafika sehemu ni kama anaongea mwenyewe. Apewe tiba haraka apone